Friday, 19 June 2015

Hospitali kwa ajili ya wanaume waliobakwa yaanzishwa

Hospitali
Hospitali moja mjini Stockholm nchini Sweden inatarajiwa kufungua kliniki ya kwanza ya wanaume waliobakwa.
Hospitali ya South General Hospital tayari ina eneo linalotoa huduma ya dharura kwa wanawake waliobakwa ama kunyanyaswa kijinsia.
Lakini sasa imetangaza siku ya jumatano kuwa itaanza kuwalaza wavulana na wanaume kuanzia mwezi Octoba.Takriban visa 370 vya unyanyasaji wa kijinsia miongoni mwa wanaume na wavulana viliripotiwa nchini Sweden mwaka uliopita kulingana na vyombo vya habari nchini humo.
nullHospitali
''Kile kinachoaminika ni kwamba wanaume hawawezi kubakwa '',Daktari Lotti Helstrom aliiambia redio ya Sweden.
Amesema kuwa swala la wanaume kubakwa ni miko lakini limeongezeka kwa kiwango kikubwa bila watu kujua.
Daktari huyo amesema kuwa ni muhimu kwa wanaume kupewa huduma za dharura sawa na wanawake.
Post a Comment