Wednesday, 31 August 2016

Sheria tata za mtindo wa nywele katika shule za sekondari A.Kusini zasitishwa

Maandamano ya wanafunziWanafunzi katika shule ya sekondari ya Pretoria wanasema kuwa mara kwa mara waalimu huwaambia wanyooshe nywele zao na hawaruhusiwi kuzitengeneza katika mtindo wa Afro.
Sheria kuhusu namna wasichana wa shule za sekondari wanavyochana nywele nchini Afrika Kusini zimesitishwa baada ya maandamano ya kupinga ubaguzi wa rangi yaliyofanywa na wanafunzi weusi, ameleza waziri nchini humo.

Bodi inayochunguza viwango vya filamu Kenya kuchunguza ''kipindi cha ngono''

Waandaaji Kaz na NiniWaandaaji Kaz na Nini hutangaza kipindi hicho kila Ijumaa kuanzia saa sita mchana
Bodi inayofuatilia inayofuatilia ujumbe wa filamu nchini Kenya imeonya kwamba itachukua hatua dhidi watengenezaji wa vipindi vya mazungumzo ya ngono ,vilivyozinduliwa mwezi Aprili, ikiwa uchunguzi utabaini kwamba wamekuwa wakivunja sheria.
Taarifa iliyotolewa na mkurugenzi mkuu wa Bodi ya Filamu ya kenya Ezekiel Mutua inahusu kipindi kinachofahamika kama " cha kwanza cha wapnzi wa jinsia moja wa kike cha TV kinachoongozwa na wapenzi wa jinsia moja maarufu wa kike ".