Hatua ya mwanamke mmoja msomi ya kuvua nguo nchini Uganda imezua mjadala mkali nchini humo.
Baada
ya kukerwa na hatua ya kufungiwa nje ya ofisi yake na usimamizi wa chuo
kikuu cha Makerere, Stella Nyanzi alivua nguo zote kama njia ya
kupinga.Hata hivyo mwishowe aliruhusiwa kuingia ofisini mwake. Wengi wa wafuasi wake wanasema kuwa alilazimishwa kufanya hivyo kutoka na yake alikuwa akitendewa.
Hata hivyo wale wanaomkosoa wanasema kwa amekiuka maadili na kwamba mwanamke hastahili kuwa uchi hadharani.
Gazeti la the New Vision nchini humo linasema kuwa waziri anayehusika na maadili anataka Nyanzi akamatwe.
No comments:
Post a Comment