Wednesday, 6 April 2016

Mapigano ya Kikabila yazuka Kaskazini Mashariki mwa Ivory coast


Mapigano ya kikabila nchini Ivory Coast
Raia 12 wa Burkina Faso wameripotiwa kupoteza maisha kwenye mapigano ya kikabila yaliyozuka katika mji wa Bouma ulioko kaskazini mashariki mwa Ivory Coast.
Serikali ya Ivory Coast ilitoa maelezo na kubainisha kuuawa kwa raia 12 wa Burkina Faso kwenye mapigano huku wengine 1,550 wakilazimika kurudi nchini kwao.
Kwa upande mwengine, serikali ya Burkina Faso imewataka viongozi wa Ivory Coast kuwahakikishia usalama raia wake pasi na kuvunja udugu uliokuwepo kati ya nchi hizo jirani.
Mapigano hayo yanaarifiwa kuanza tangu wiki jana baina ya jamii za Peulhi, Lobi na Koulango mjini Bouna.
Post a Comment