Mwana wa kiume wa
kiongozi wa upinzani nchini Uganda Dkt Kizza Besigye amechaguliwa kuwa
rais wa chama cha mijadala chuo kikuu cha Oxford.
Anslem Besigye alikuwa ametengeneza video fupi ya kuomba
wanafunzi wenzake wampigie kura.Mamake Winnie Byanyima amefurahia ushindi wa mwanawe na kuandika kwenye Twitter: “Ameshinda! Anslem amechaguliwa rais wa chama cha mijadala katika bewa lake. Najionea fahari kama mamake.”
Kwenye video aliyokuwa ameitengeneza alikuwa amesimulia mambo ambayo amefanyia chama hicho na uzoefu wake katika mijadala.
Mwisho wa video mamake Bi Byanyima, alionekana na kusema “huna budi kushinda uchaguzi huu, nimekusaidia sana!”.
Babake Anslem, Dkt Kizza Besigye, amewania urais mara nne dhidi ya kiongozi wa muda mrefu wa Uganda Yoweri Museveni bila mafanikio.
No comments:
Post a Comment