Thursday 14 April 2016

Wanawake 2 vikongwe wameuawa kinyama wilayani Rorya mkoani Mara.

Wanawake wawilivikongwe wameuawa kinyama kwa kupigwa na kukatwakatwa kwa mapanga kisha miili yao kuchomwa moto katika kijijicha Kenyamsana wilayani Rorya mkoani Mara kwa tuhumu za kujihusisha na ushirikina,tukio ambalo limesababisha hofu kubwa kwa wanawake wengi wenye umri mkubwa katika kijiji hicho.
Wakizungumzia tukio hilo la kwanza kutokea wilayan Rorya, baadhi ya ndugu wa marehemu hao, wamesema kuwa kundi la watu waliwakamata wanawake hao vikongwe    kisha kuwapiga katika sehemu mbalimbali za miili huku wakiwaingiza kwa nguvu ndani ya nyumba zao ambazo zimeezekwa kwa kutumia nyasi na kuwachoma moto. 

Kufutia tukio hilo la kusikitisha na la kikatili Mwenyekitiwa kamati ya ulinzina usalma ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Rorya Bw Felix Lyaniva, amefika    eneo la tukio na kuliagiza jeshi la polisi kuwakata watu wote ambao wamehusika kufanya kitendo hicho cha kinyama kwa kuanzia na viongozi wa vitongoji    katika eneo hilo. 
Tayari Jeshi la Polisi limewakamata watu 13 kwa tuhuma za kuhusika na mauaji hayo ya wanawake hao vikongwe Bi Ghati Ndege na Nyakorema Waryuba wote    wakazi wa k ijiji hicho cha Kenyamsana wilayani Rorya.

CHANZO; ITV HABARI

No comments: