Kocha mkuu wa Yanga amelalamika juu ya waandishi ambao wamekuwa
wakiandika vitu ambavyo yeye hajazungumza kwasababu vinamletea matatizo
na waajiri wake.
Hans amesema hivyo baada ya gazeti moja kutoa habari ambayo
inasababisha mazingira magumu, anasema yeye ni mwajiriwa hivyo anatarati
zake za kazi na badala yake amewaomba waandishi kuchukua na kufanyia
kazi kile ambacho anakuwa amekizungumza mwenyewe
“Mimi huwa zizungumzi kuhusu kuhusu makocha, timu nyingine wala TFF,
kuna gazeti linasema mimi nilienda TFF kujaribu kubadilisha tarehe za
baadhi ya mechi lakini kulikuwa hakuna uwezekano juu ya hilo kwahiyo
nikawa nimekasirishwa na TFF na kuanza kuwashutumu kwamba hawajui
kufanya mambo yao, sijawahi kuzungumza kuhusu federation watu wanatakiwa
kujua hilo”, amesema Hans ambaye anaonekana kuchukizwa na habari hiyo.
Kuhusu mchezo wao wa kiporo dhidi ya Mtibwa Sugar ambao Yanga
walishinda kwa bao 1-0 na kukwea hadi kileleni mwa ligi, Hans
amekimwagia sifa kikosi chake kuwa kimecheza vizuri kwenye mchezo huo
licha ya kupoteza nafasi nyingi za kufunga magoli.
“Tulicheza vizuri sana kitu kimoja kilichotuangusha ni kutotumia
nafasi tulizozipata, na wakati mechi inaelekea kumalizika kulikuwa na
‘tension’ kubwa kwa wachezaji wangu na hiyo ilisababishwa na kuwa na
goli moja tu mkononi lakini kama unamagoli zaidi ya mawili unakuwa huna
presha”.
“Tumecheza dhidi ya timu ngumu na tulilijua hilo kabla ndiyo maana
mwanzoni tulianza na mfumo wa 3-5-2 lakini kwasababu tupo nyumbani na ni
lazima tushinde mechi ndiyomaana tukamtoa beki mmoja nje na kuongeza
mshambuliaji mwingine”.
No comments:
Post a Comment