Saturday, 9 April 2016

Fatuma Karume: Wanzanzibar wanaishi kama wanyama

Mwanadada jasri na aliyejizolea umaarufu hivi karibuni Fatuma Karume AMELIPUKA, unaweza kusema. Akihojiwa na DW amesema sasa Zanzibar wanaishi kama wanyama maana hawafuati katiba. "Kama wameamu kuondoa utaratibu tuliyojiwekea sasa tuna tofauti gani na wanyama?"
Alipoulizwa kama vitisho vya Ccm havimtishi na kama baba yake hamdhibiti, amesema. "Mimi siyo mbwa wala paka, nina haki yangu ya asili ya kujieleza na kutoa maoni" Amesema babake hawezi kuondoa uhuru wake kisa Ccm."Wanataka baba anidhibiti? (kicheko) "nina miaka 46, tena baba ananihimiza kufanya nachoamini ni haki"

Alipoulizwa maoni yake kuhusu MCC amesema anasikia watu wanasema wazanzibar wako tayari kufa njaa lakini serikali iachwe huru. "Hivi tunahitaji serikali huru au watu huru? hapa tuna wakoloni wengine" Ameuliza "yaani watu wa Zanzibar wafe njaa kisa Shein awe rais?" haiwezekani!
Post a Comment