Manchester City
imepanda hadi nafasi ya tatu katika jedwali la ligi ya Uingereza baada
ya kuicharaza Stoke City 4-0 huku ikitarajiwa kumenyana ana Real Madrid
katika kombe la vilabu bingwa Ulaya siku ya Jumanne.
Fernando alifunga kwa kichwa na kuwaweka City kifua mbele kabla ya Sergio Aguerro kufunga kwa njia ya Penalti.
Kwengineko Eden Hazard alifunga bao lake la kwanza na kuisadia timu yake kuishinda Bournemouth.
Vilevile Newcastle iliimarisha matumaini yao ya kusalia katika ligi ya Uingereza baada ya kutoka sare ya 2-2 na wenyeji Liverpool katika uwanja wa Anfield.
Daniel Sturridge na Adam Lalana waliiweka mbele Liverpool kabla ya Newcastle kukomboa kupitia Papis Cisse na Colback .
No comments:
Post a Comment