Mshambuliaji wa
klabu ya Chelsea Diego Costa ameongezewa marufuku ya mechi ambazo
hataruhusiwa kucheza pamoja na kutozwa faini zaidi kwa sababu ya utovu
wa nidhamu.
Mshambuliaji huyo ameongezewa marufuku ya mechi moja
na pia akapigwa faini ya £20,000 baada ya kukiri shtaka la utovu wa
nidhamu.Mchezaji huyo wa miaka 27 ameadhibiwa kutokana na vitendo vyake baada ya kuonyeshwa kadi nyekundi wakati wa mechi ya Kombe la FA dhidi ya Everton tarehe 12 Machi.
Mhispania huyo alikorofishana na Gareth Barry na alionekana kana kwamba alitaka kumuuma shingo, ingawa Barry baadaye alisema Costa hakumgusa kwa meno.
Costa awali alikuwa amepigwa marufuku mechi mbili lakini sasa atakosa mechi tatu.
Mechi ya kwanza aliyokosa ilikuwa dhidi ya West Ham tarehe 19 Machi ambayo iliisha 2-2 na pia hataruhusiwa kucheza mechi ya Jumamosi ugenini dhidi ya Aston Villa.
Costa sasa atakosa pia mechi ya ugenini dhidi ya Swansea tarehe 9 Aprili.
Aidha, ameonywa kuhusu tabia yake siku za usoni.
No comments:
Post a Comment