Wednesday 30 April 2014

Bunge la Libya lashambuliwa

bunge-la-libya-lashambuliwaUchaguzi wa serikali ya muda uliokuwa ukifanyika katika bunge la Libya wakatizwa.

Uchaguzi wa serikali ya muda uliokuwa ukifanyika katika bunge la Libya wakatizwa.
Watu wasiotambulika walitekeleza mashambulizi ya silaha katika bunge la Libya na kukatiza uchaguzi huo.
Washambuliaji waliingia katika uwanja wa bunge uchaguzi ulipokuwa ukiendelea na kuanza kufyatua risasi na kuwajeruhi watu kadhaa.
Awamu ya kwanza ya uchaguzi ilimalizika huku ya pili ikiahirishwa hadi siku iliyofuata.
Waziri mkuu wa Libya Abdullah El Tani alijiuzulu baada ya kulengwa katika mashumbulizi hayo.
Katika tukio jingine, hakimu wa zamani Ahmad Bu Acile el-Mansuri alivamia na kuuawa katika mji wa Derane lililoko katika jimbo la el-Kubbe Mashariki mwa nchi hiyo. Mansuri alihudumu katika mahakama kuu kabla ya mapinduzi yaliyotekelezwa tarehe 17 mwezi Fubruari. Kufikia sasa hakuna taarifa rasmi iliyotolewa kuhusiana na mauaji hayo

Maandamano dhidi ya serikali ya Nigeria

Maandamano kuhusu wasichana waliotekwa
Maandamano makubwa ya kwanza yanatarajiwa kufanyika katika mji mkuu wa Nigeria- Abuja baadaye leo watu wakiitaka serikali kuchukua hatua zaidi kuwanusuru wasichana 200 wa shule waliotekwa nyara na wanamgambo wa kiislam .
Wasichana hao walichukuliwa kutoka shule yao ya malazi iliyopo katika eneo lisiloweza kufikiwa kwa urahisi kaskazini mashariki mwa nchi zaidi ya wiki mbili zilizopita.
Waandalizi wa maandamano hayo wanaita serikali kuelekeza juhudi zao kwa wasichana waliopotea .
Mpango ni kuandamana hadi bungeni na kwa mshauri wa taifa wa masuala ya usalama na kuwasilisha barua ya kutoa wito wa kufanyika kwa juhudi zaidi kuwanusuru wasichana hao.
Mwanaharakati mmoja wa kijamii amesema katika nchi nyingine yoyote ile suala la kutekaji nyara wa wasichana hao wengi lingekuwa ni mjadala wa kila siku .
Lakini serikali ya Nigeria imekuwa ikikabiliwa na ukosoaji mkubwa kwa kukaa kimwa huku wazazi wenye shauku wakisailia kuwa gizani kuhusu nini kinachoendelea kuhusiana na wasichana wao.
Huenda kwa kuhisi hilo rais wa Seneti , David Mark, sasa amezungumza. Amewatolea wito watekaji kuawaachilia mara moja wasichana bila masharti na akasema bila shaka taifa letu liko vitani .

Watoto 9,000 walitumiwa vitani Sudan kusini

Navi Pillay akiwa ziarani Sudan Kusini

Zaidi ya watoto 9,000 wamekuwa wakitumiwa kama wanajeshi katika vita vivayoendelea nchini Sudan Kusini.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa mkuu wa haki za binadamu katika umoja wa Mataifa Navi Pillay.
Pande zote kwenye mgogoro huu , wanajeshi na waasi wamedaiwa kuwasajili watoto kupigana.
Bi Pillay amesema kuwa Sudan Kusini inakabiliwa na tisho la njaa , lakini viongozi wake hawaonekani kuliona hilo kama swala muhimu la kushughulikiwa.
Alikuwa anazungumza mwishoni mwa ziara yake nchini Sudan Kusini ambako mgogoro wa wenyewe kwa wenyewe umewaacha mamiioni ya watu bila makao.
Vita vilizuka mwezi Disemba kati ya wanajeshi wa serikali wanaomtii Rais Salva Kiir na hasimu wake kiongozi wa waasi, Riek Machar ambaye anatuhumiwa kwa kuanzisha mgogoro huu kwa kuwa na njama ya kumuondoa mamlakani.
Riek Machar pia wakati mmoja alikuwa makamu wa Rais wa Salva Kiir.
Machar amekanusha madai hayo lakini amekuwa akiongoza waasi wanaopigana dhidi ya serikali.
Pande zote mbili zimekuwa kwenye meza ya mazungumzo kujaribu kusitisha vita lakini hakuna mabadiliko katika hali inayokumba nchi hiyo, Vita vingali vinaendelea.

Chelsea uso kwa uso na Atletical Madrid

mpinzani-wa-real-madrid-kubainikaTimu ya pili itakayochuana katika fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya itabainika leo Chelsea watakapochuana na Atletico Madrid.

Awamu ya pili ya nusu fainali itasakatwa katika uga wa Stamford Bridge saa 21:45 saa za Afrika Mashariki.
Wasiwasi wa Chelsea
Timu ya Chelsea itakosa huduma za wachezaji muhimu kutokana na majeraha na adhabu ya kutocheza mechi ya leo. Petr Cech aliyepata jeraha la bega na John Terry watakosa mechi ya leo kutokana na majeraha huku John Obi Mikel na Frank Lampard wakikosa idhini ya kucheza kutokana na adhabu ya kati ya Manjano. Mohamed Salah na Nemanja Matic hawakujumuishwa katika orodha ya wachezeja na hivyo basi hawataweza kuvalia jezi usiku huu.
Je Atletico wataandika historia mpya?
Atletico Madrid inatazamia kuandika historia mpya ya kufika katika fainali ya ligi ya Mabingwa kwa mara ya kwanza. atletico watamkosa mchezaji wao machachari ambaye alionyeshwa kadi ya manjano ya pili katika awamu ya kwanza. Arda Turan hatarajiwi kuwa katika timu itakayoanza kutokana na majeraha.
Je Diego Simeone atafanikisha ndoto ya Atletico au Mourinho ataonyesha ubabe wake?

Tuesday 29 April 2014

Marubani nchini Ufaransa wafanya mgomo

Ili kufanya mgomo wenye ufanisi mkubwa, rubani wa Ufaransa watasita kufanya kazi kwa masaa kadhaa kati ya Mei tarehe 3 na Mei tarehe 30.
mgomo-wa-rubani-nchini-ufaransa
Kufuatia likizo ya mwisho wa wiki, usitisho mkubwa na uchelewsho wa safari za ndani na za nje unasubiriwa kutokana na mgomo wa rubani.
Kutokana na shria ya mwaka 2012, rubani wanatakiwa kutoa taarifa au kuwajulisha waajiri wao masaa 48 kabla ya kufanya mgomo. Sheria hiyo itawezesha ratiba nzuri ya safari na kuwaonya abiria ipasavyo iwapo kutakuwa na mgomo wa makampuni ya ndege.
Muungano wa French Pilot Union umesema kuwa sheria hiyo ya kutoa onyo masaa 48 kabla ya mgomo itawezesha makampuni ya ndege kuleta rubani kutoka nchi za nje na hivyo basi madhumuni ya mgomo wao kutochukuliwa ipasavyo.
Muungano huo ulieleza kuwa licha ya asilimia 85 ya rubani kufanya mgomo hivi karibuni, hakuwa na usitisho wala uchelewesho wowote wa ndege kutokana na makampuni ya ndege kuwaleta rubani hasa kutoka katika mashariki ya bara Ulaya.

Kimbunga cha Mississippi


Nchini Marekani Kimbunga kimepiga jimbo la Mississippi
kimbunga-cha-mississippi
Baada ya kupiga majimbo ya Arkansas na Oklahoma, kimbunga kimepiga jimbo la Mississippi.
Katika mji wa Tupelo iliyoko Kaskazini mwa jimbo hilo kimbunga kilipiga na kukata nyaya za stima, kungoa miti na kusababisha uharibifu wa nyumba.
Maafisa wahusika pamoja na wale wakujitolea walitoa msaada kwa walioathiriwa na kimbunga hicho.
Wataalam wametoa tahadhari kwa wakaazi wa majimbo ya kati na kusini kuwa huenda kimbunga kikapiga tena kutokana na mabadiliko katika hali ya anga.
Watu 17 walifariki katika majimbo ya Arkansas, oklahoma na Iowa kutokana na Vimbunga.

Wanajeshi wa Israel wabomoa msikiti

Wanajeshi wa Israel walivunja msikiti mmoja na nyumba 4 za wapalestine mjini Nablus.

wanajeshi-wa-israel-wabomoa-msikitiKulingana na taarifa iliyotolewa na mwanachama wa Kamati ya Upinzani cha Umma wa Palestine, Yusuf Deyriyye, Wanajeshi wa Israeli walivamia na kubomoa msikiti huo uliojengwa miaka sita iliyopita na nyumba nne huku wakidai kuwa zilikuwa zimejengwa bila idhini.
Deyriyye alisema kuwa wanajeshi wa Israel walikua wametoa onyo kuhusiana na msikiti huo na nyumba hizo. Aliongezea kusema kua " kwa miaka mingi Israel imekuwa ikitumia kisingizio hicho kuharibu nyumba za Wapalestine."
Israel bado haijatoa taarifa rasmi kuhusiana na shambulizi hilo.
Mashambulizi kama haya yaliwahi kutendeka katika kijiji hicho cha Et-Tavil yenye wakaazi wanaojishughulisha na kilimo na ufugaji.

Cech, Hazard na Eto'o kuivaa kesho Atletical Madrid

Inashangaza: Petr Cech akitembea na Nathan Ake (katikati) na Marco van Ginkel kuelekea katika mazoezi.
article-2615784-1D71825C00000578-532_634x495JOSE Mourinho ameanza maandaliza ya mechi ya kesho ya nusu fainali ya pili ya UEFA dhidi ya Atletico Madrid, huku ikishangaza kumuona mlinda mlango namba moja wa Chelsea, Petr Cech akifanya mazoezi.
Cech aliteguka beka katika mchezo wa kwanza uliomalizika kwa suluhu ya bila kufungana Vicente Calderon na Mourinho alithibitisha wiki iliyopita kuwa kipa huyo anahitaji upasuaji ili kurudisha bega katika hali yake.
Nyota wa samba: Willian, David Luiz, Ramires na Oscar wakielekea katika uwanja wa Coham tayari kwa mazoezi.
article-2615784-1D71868C00000578-845_634x454Haikuwa rahisi kumouna Cech leo hii ambaye alitakiwa kukaa nje ya uwanja kwa miezi mitatu, hivyo imeshangaza kumuona mchezaji huyo akiwa miongoni mwa wachezaji waliofanya mazoezi leo hii.
Alipoulizwa kama yuko imara kwa mechi ya kesho, alitabasamu na kusema “Ndiyo”, lakini alienda zake na kujiunga na wenzake.
Cech alionekana akifanya mazoezi mepesi leo hii, na makipa wenzake Mark Schwarzer, Henrique Hilario na Mitchell Beeney walipoanza mazoezi na kocha wa makipa, Christophe Lollichon, Cech alikaa pembeni.
Mbali na Cech, wachezaji wengine waliokuwa majeruhi, Samuel Eto`o, nahodha, John Terry, na Eden Hazard nao wamefanya mazoezi leo hii kujiandaa na kipute cha kesho.

Kavumbagu Atua AZAM FC


Mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi aliyekuwa anakipiga kwenye klabu ya Dar Young African Didier Kavumbagu amesaini kuichezea klabu bingwa ya Tanzania bara Azam FC.
KAVUMBANGU-1Taarifa rasmi zilizothibitishwa na mtandao huu kupitia meneja wa klabu ya Azam FC Jemedari Said ni kwamba Kavumbagu ambaye inaaminika amemaliza mkataba wake wa miaka miwili na klabu ya Yanga aliosaini wakati akitokea kwao Burundi miaka miwili iliyopita, amesaini mkataba wa mwaka mmoja tu kuitumikia klabu ya Azam FC.
“Kavumbagu is a done deal! Tumemalizana nae na amesaini rasmi mkataba wa mwaka mmoja, so tutakuwa nae msimu ujao kwenye kampeni ya kutetea ubingwa wetu pamoja na michuano ya klabu bingwa ya Afrika,” alifunguka Jemedari

Wanafunzi waliotekwa nyara Nigeria walipelekwa nchi jirani


Jamaa wa wasichana waliotekwa nyara Nigeria
Baadhi ya wasichana waliotekwa nyara na watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa kiisilamu wa Boko Haram, wanaaminika kupelekwa katika nchi jirani.
Kiongozi mmoja katika eneo la Chibok ambako wasichana hao walitekwa nyara wiki mbili zilizopita, Pogo Bitrus, ameambia BBC kuwa watu kadhaa wamewaona watu waliojihami wakiwa wanavuka mpaka na washichana hao na kuingia Cameroon na Chad.
Baadhi ya wasichana walikuwa wamelazimishwa kuolewa na wapiganaji hao.
Bwana Bitrus alisema kuwa wasichana 230 bado hawajapatikana tangu tukio la utekaji nyara katika shule ya mabweni mjini Chibok katika jimbo la Borno wiki mbili zilizopita.
Kundi la wapiganaji wa Boko Haram limelaumiwa kwa tukio hilo ingawa bado halijasema chochote.
Bwana Bitrus, ambaye ni kiongozi mmoja wa eneo hilo, alisema kuwa wasichana 43 walifanikiwa kutoroka, wakati wengine 230 bado wanazuiliwa.
Idadi hii bila shaka ni kubwa kuliko taarifa za awali zilizvyosema ingawa hakuwa na uhakika ikiwa idadi hiyo ni sawa.
Wanafunzi hao walikuwa wanajiandaa kufanya mitihani yao ya mwisho wa muhula na kwamba wako kati ya umri wa miaka 16 na 18.
''Baadhi yao wamepelekwa nchini Chad huku wengine wao wakipelekwa nchini Cameroon,'' alisema bwana Bitrus.
Bwana Bitrus alisema kuwa kulikuwa na ripoti kwamba baadhi ya wasichana hao wamefanywa kuwa wake za wapiganaji hao.

Mama awaua wanawe 3 walemavu


Baba ya watoto hawa alikuwa safarini nchini Afrika Kusini wakati mauaji yalipofanyika.
Mama anayetuhumiwa kwa mauaji ya watoto wake watatu nchini Uingereza amewekwa rumande kwa ukaguzi wa kiakili kubaini ikiwa alikuwa timamu wakati wa mauaji hayo.
Tania Clarence, mwenye umri wa miaka 42, alihudhuria kikao cha mahakama kwa njia ya video akiwa gerezani akituhumiwa kwa mauaji mapacha wake wawili wenye umri wa miaka mitatu na mwanawe msichana mwenye mwiri wa miaka minne.
Watoto hao walemavu, walipatikana nyumbani kwao katika mtaa wa New Malden wakiwa wamefariki Aprili 22.
Mahakama pia ilisikia kuwa watoto hao walikuwa na ulemavu uliosababishwa na ugonjwa wa uti wa mgongo.
Mahakama iliambiwa kuwa watoto hao walifariki katika hali ya kuzuiwa kupumua.
Jaji Judge Brian Barker, alisema Bi Clarence anaweza kuondolewa jela na kuwekwa rumande kufanyiwa uchunguzi na kupokea matibabu ya kiakili kwa sababu tukio hilo sio la kawaida
''Hio sio dhamana , lakini ninachoamrisha ni aweze kufanyiwa ukaguzi wa kiakili kuambatana na kifungu cha 35 cha sheria. Baada ya hapo anaweza kuwekwa rumande ili achunguzwe zaidi hali yake, '' alisema jaji.
Wendesha mashitaka waliambia mahakama kuwa polisi walikuwa wanasubiri matokeo ya uchunguzi wa maiti za watoto kabla ya kubaini chanzo cha vifo vyao.
Mahakama iliambiwa kuwa babake watoto hao alikuwa nchini Afrika Kusini na mwanao mkubwa wakati wa mauaji hayo.
Mahakama itasikia baadaye utetezi wa Bi clarrence ikiwa anakiri au kukana mauaji tarehe 15 mwezi ujao.

Sketi yamtia matatani Polisi nchin kenya


Afisa Linda Okello akiwa kazini
Afisaa mmoja wa polisi mwanamke nchini Kenya amepewa onyo kali kwa kuvalia sketi iliyokuwa imembana kiasi cha kuonyesha umbo lake.
Wakuu wake walichukua hatua ya kumuonya polisi huyo baada ya picha yake kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii na kupigiwa gumzo kubwa.
Alipigwa picha akiwa amevalia sketi yake fupi na yenye kumbana akiwa anashika doria katika eneo ambako mashindano ya magari yalikuwa yanafanyika eneo la Kati mwa Kenya.
Afisaa huyo kwa jina Linda Okello, alitakiwa kufika mbele ya mkuu wake James Mugeria na kuonywa vikali dhidi ya kuvalia hivyo kwa mara nyingine, kitendo ambacho alifahamishwa kuwa ni utovu wa nidhamu kwa kuvalia nguo isiyo ya heshima kwa polisi
Maafisa mjini Kiambu walisema kuwa kupewa onyo kwa afisa Linda na kuonywa dhidi ya kuvalia sketi yake iliyokuwa imembana sana ni jambo la kawaida na kwamba ameruhusiwa kuendelea na majukumu yake.
Waliongeza kuwa afisa huyo ameamrishwa kuanza kuvalia kiheshima.
Alipigwa picha na mwanahabari mmoja wa gazeti moja maarufu nchini Kenya akiwa na wenzake kazini mjini Kiambu. Lakini punde si punde picha hiyo ikaanza kusambazwa kwa mitandano ya kijamii na baadhi wakiikejeli.
Taarifa ya polisi huyo kuonywa ilizua hasira kwenye mitandao ya kijamii baadhi wakihoji ikiwa ni makosa kwa afisaa wa polisi kuvalia sketi ya kumbana. Nini Kauli yako?

Monday 28 April 2014

Serikali mpya imeingia mamlakani nchini Serbia.

serikali-mpya-nchini-serbia
Bunge la Serbia limepitisha serikali yenye mawaziri 16 iliyochaguliwa na mkuu wa chama cha "Serbian Progressive Party" (SNS) Aleksandar Vuçiç.
Wabunge 198 kati ya wabunge 228 waliokuwepo bungeni walipiga kura kukubali orodha iliyowasilishwa bungeni.
Katika hafla ya kuapishwa iliyohudhuriwa na Rais wa jamhuri ya Serbia, Waziri mkuu Vuçiç alisema kuwa wataongoza nchi hiyo kwa njia ya uadilifu.
Serikali hiyo mpya itawajumuisha Ivitsa Daçiç mkuu wa chama cha "Serbian Socialist Party" (SPS) ambaye atachukua wadhfa wa waziri wa mambo ya nje na Rasim Lyayiç ambaye ni mkuu wa chama cha "social Democratic Party" (SDPS) atakayechukua wadhfa wa waziri wa Biashara, Mawasiliano na Utalii. Waziri Rasim Lyayiç aliwahi kuhudumu katika wizara hii hapo awali.
Chama cha "Serbian Progressive Party" (SNS) kinachoongozwa na Aleksandar Vuçiç kilitwaa ushindi katika uchaguzi wa mapema uliofanyika tarehe 17 mwezi Machi nchini Serbia.

Mzozo wa kidiplomasia kati ya Kenya na Somalia

Afisa wa ubalozi wa Somalia nchini Kenya Siyad Mohamud
Mzozo wa kidiplomasia unanukia kati ya Kenya na Somalia baada ya polisi kumkamata kimakosa mmoja wa maafisa wakuu wa ubalozi wa Somalia nchini Kenya Siyad Mohamud Shire .
Tayari balozi wa Somalia nchini Kenya Mohamed Ali Nur ameitwa na serikali yake kueleza matukio yanayoambatana na kukamatwa kwa raiya wa asili ya kisomali ambao serikali inasema baadhi yao hawana vibali vya kuishi nchini.
Maafisa wa polisi nchini Kenya wamekuwa wakiendelea na msako wao dhidi ya wahamiaji haramu na wale wanaoshukiwa kushiriki matendo ya kigaidi na uhalifu.
Hata hivyo serikali ya Somalia imesikitishwa nao kwa kumkamata afisa wa ubalozi wa Somalia anayeshughulikia masuala ya kisiasa Siyad Mohamud Shire .
Kwa sababu hiyo Somalia imetuma taarifa katika vyombo vya habari ikisema kuwa waziri mkuu Abdiweli Sheikh Ahmed amefanya mazungumzo na balozi wa Somalia nchini Kenya aliyefika Mogadishu hapo Jumapili kumweleza hatma ya raiya wa Somalia wanaoishi Kenya katika msako unaoendelea
Japokuwa serikali ya Kenya kupitia kwa wizara ya usalama wa kitaifa imekuwa ikishikilia kuwa hailengi jamii yoyote katika kuwakamata raiya wa kigeni na kuwarejesha katika nchi zao ama kambi za wakimbizi.
Taarifa hiyo imeanusha hilo na kusema maafisa wa polisi wamekuwa wakiwazuilia wasomali wengi na kuwatesa.
Tukio la kumnasa, Bwana Siyad Mohamud Shire limechukuliwa na serikali ya Somali kuwa ukiukaji mkubwa wa mkataba wa kidiplomasia.
Inasemekana kuwa bwana Shire alikamatwa na kuzuiliwa na polisi kwa muda licha ya kuwa na kitambulisho cha kazi.
Mkutano kati ya waziri mkuu wa wa Somali na balozi wa Kenya ulifanyika baada ya baraza la mawaziri kuandaa kikao kisichokuwa cha kawaida kujadili hali ilivyo Kenya.
Juhudi za kumpata waziri wa mambo ya nje wa Kenya balozi Amina Mohamed kueleza msimamo wa serikali hazikufaulu ila maafisa wa polisi walikataa kuzungumzia suala hilo wakisema kuwa litashughulikiwa na ngazi ya juu.
Polisi nchini Kenya walianza msako kote nchini wiki tatu zilizopita baada ya matukio mengi yanayoambatanishwa na ugaidi ama uhalifu kutokea huku zaidi ya watu kumi wakifariki baada ya milipuko kadhaa kutokea katika mtaa wa Eastleigh na maeneo jirani jijini Nairobi.
Kisichojulikana kwa sasa ni namna nchi zote mbili zitakavyoendelea kushirikiana kidiplomasia katika mazingira yaliyopo.

Chelsea yaichinjia mbali Liverpool



Demba Ba mfungaji wa bao la kwanza la Chelsea dhidi ya Liverpool
Chelsea vijana wa darajani Stanford, jijini London, wamewanyamazisha vinara wa ligi kuu ya England, Liverpool baada ya kuwachakaza mabao 2-0 katika uwanja wao wa Anfield.
Liverpool ikiwa imeuanza mchezo huo kwa kasi na kwa dhamira ya kupata ushindi ilishuhudia jahazi lake likitota katika dakika ya 45 ya kipindi cha kwanza.
Alikuwa ni Demba Ba aliyeanza kupeleka kilio kwa majogoo wa Liverpool pale alipounasa mpira kufuatia nahodha wa Liverpool Steven Gerrard kuteleza na Ba kupata mwanya wa kumfunga kirahisi Mignolet.
Liverpool hawakukubali kusalimu amri kwa wageni,kwani waliendelea kupeleka mashumbulizi ya hatari langoni mwa wapinzani wao wakiishia kwa kosa kosa. Liverpool wanapigania ubingwa wa ligi kuu ya England kwa mara ya kwanza katika miaka 24 iliyopita.

Willian mfungaji wa bao la pili la Chelsea dhidi ya Liverpool
Joe Allen na Luis Suarez walizidisha mashambulizi katika lango la Chelsea, kabla ya Willian aliyeingia kipindi cha pili kufunga bao la pili kwa timu yake ya Chelsea baada ya Fernando Torres bila uchoyo akiwa katika nafasi ya kufunga alimpasia Willian na kuwaachia kilio wenyeji wao Liverpool.
Chelsea katika mchezo huo ilikuwa ikipewa nafasi finyu ya kuibuka washindi. Lakini ni Jose Mourinho aliyeibuka na kicheko, huku Brendan Rodgers akiugulia kipigo cha kwanza kwa timu yake tangu kuanza kwa mwaka huu.
Kwa ushindi huo sasa, Chelsea inaachwa pointi mbili nyuma ya Liverpool ambayo inaoongoza ikiwa na pointi 80, baada ya michezo 36. Msimamo wa timu hizo ni Liverpool pointi 80, Chelsea 78, Manchester City 74, itakuwa na pointi 77 iwapo itaifunga Crystal Palace katika mchezo wao, huku Arsenal ikichukua nafasi ya nne ikiwa na pointi 70. Manchester City na Arsenal zimecheza mechi 35 kila moja huku Liverpool na Chelsea zikiwa zimecheza mchezo mmoja zaidi.

Kiongozi wa Brotherhood ahukumiwa kifo

Baadhi ya jamaa wa watuhumiwa waliohukumiwa kifo walizirai baada ya kupokea taarifa
Jaji wa mahakama nchini Misri, amewahukumu kifo watu 683 akiwemo kiongozi wa kundi la Muslim Brotherhood Mohammed Badie.
Mawakili wa watuhumiwa wanasema kuwa wateja wao walikabiliwa na makosa mengi yakiwemo, kushambulia kituo cha polisi mjini Minya mwaka 2013 ambapo polisi mmoja aliuawa.
Jaji huyo pia alibatilisha hukumu ya kifo iliyotolewa kwa watu 492 kati ya watu 529. Hukumu hiyo ilipitishwa mwezi Machi na sasa watahudumia kifungo cha maisha jela.
Kesi na kasi ya kuzisikilizwa kwa kasi hizo, imesababisha hasira na kukosolewa na shirika la kutetea haki za binadamu la Umoja wa Matifa UN.
Kadhalika shirika la Huma Rights Watch limelalamika kuwa kesi hizo zilisikilizwa tu kwa saa chache huku mahakama ikiwazuia mawakili kuwawakilisha washitakiwa.
Duru zinasema kuwa jamaa wa watuhumiwa waliokuwa wanasubiri nje ya mahakama walizirai baada ya kupokea taarifa za hukumu hiyo.
Mwezi jana shirika la kutetea haki za binadamu la Umoja wa Mataifa, lililaani kesi hizo likisema kuwa zinakiuka sheria ya kimataifa ya haki za binadamu.
Msemaji wa shirika hilo, Navi Pillay, alisema kuwa kesi hiyo ilikumbwa na makosa mengi ya utarataibu.
Maafisa wa utawala nchini Misri wamekuwa wakiwasaka na kuwakamata wapiganaji wa kiisilamu na wanachama wa vuguvugu la Muslim Brotherhood ambao walimuingiza mamlakani aliyekuwa Rais Mohammed Morsi ambaye baadaye aliondolewa na Julai.
Mamia wameuawa huku maelfu ya raia wakikamatwa

Sunday 27 April 2014

Afrika Kusini Yaadhimisha Miaka 20 ya Demokrasia

Wananchi wa Afrika Kusini wanasherehekea leo hii miaka 20 tangu kufanyika uchaguzi uliozishirikisha jamii zote za nchi hiyo katika uchaguzi uliomaliza utawala wa ubaguzi wa rangi.
Nelson Mandela akipiga kura mwaka 1994 Nelson Mandela akipiga kura mwaka 1994
Siku hiyo inaadhimishwa kwa maandamano mitaani, hotuba, sala, matamasha ya muziki na gwaride la kijeshi. Sherehe kuu itaongozwa na rais Jacob Zuma katika majengo ya Ikulu mjini Pretoria yajulikanayo ka Union Buildings, ambako viongozi wa serikali za ubaguzi walizitia saini sheria nyingi za kibaguzi ambazo rais wa kwanza mweusi wa nchini hiyo marehemu Nelson Mandela alizipinga karibu wakati wote wa uhai wake.
Siku hiyo ya uchaguzi wa kwanza wa kidemokrasia, tarehe 27 Aprili, 1994 imefanywa siku ya mapumziko, ikijulikana kama Siku ya Uhuru. Kwa raia wengi wa Afrika Kusini inaambatana na kumbukumbu ya furaha, wakati ambapo kwa mara ya kwanza watu weusi, wahindi, machotara na wazungu walichanganyika katika mistari mirefu mbele ya vituo vya kupigia kura.
Matumaini sambamba na kukata tamaa
Raia wengi weusi walifurahia uhuru baada ya miongo mingi ya ubaguzi wa rangi Raia wengi weusi walifurahia uhuru baada ya miongo mingi ya ubaguzi wa rangi
Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel askofu mstaafu Desmond Tutu amesema siku hiyo ilikuwa na mihemko ya mapenzi, huku rais wa mwisho wa serikali ya kibaguzi, FW de Klerk ameielezea kuwa siku ya fahari kuu kwa Afrika Kusini.
Hata hivyo, miaka 20 baadaye, msisimko huo umemalizika, na watu wanakitathmini kipindi hicho cha utawala wa demokrasia kuwa chenye mchanganyiko wa mafanikio na kushindwa.
Miongoni mwa mambo mengine, Afrika Kusini inajivunia katiba ambayo ni mojawapo ya bora kabisa duniani, mahakam huru na kuwa nchi ambayo pengine inaongoza kiuchumi barani Afrika. Lakini mafanikio hayo yametiwa doa na matumizi mabaya ya fedha za umma na lawama za ufusadi zinanoelekezwa kwa viongozi wa chama Tawala-ANC.
Changamoto zinaongezeka
Askofu Desmond Tutu ambaye anazingatiwa kuwa Nuru ya uadilifu nchini Afrika Kusini, ameelezea miongo miwili iliyopita kama kipindi cha mafanikio makubwa, lakini anaapa kuwa hatakiunga mkono chama cha ANC katika uchaguzi mkuu ujao.
Licha ya mafanikio makubwa, bado umaskini ni tatizo sugu nchini Afrika Kusini Licha ya mafanikio makubwa, bado umaskini ni tatizo sugu nchini Afrika Kusini
Maadhimisho haya ya miaka 20 ya uhuru yanafanyika katika mwaka ambamo pia kuna uchaguzi mkuu, tarehe 7 Mei. ANC inatarajiwa kushinda uchaguzi huo wenye ushindani mkubwa, licha ya shutuma ubadhirifu na kupanuka kwa pengo kati ya matajiri na maskini ambavyo vilishuhudiwa chini ya utawala wake.
Kuendelea kupendwa kwa chama cha ANC ni ushahidi kwamba wananchi wengi wa Afrika Kusini wanahisi hali ni bora zaidi ikilinganishwa na wakati wa utawala wa ubaguzi wa rangi ulioendeshwa na wazungu walio wachache nchini humo.
Mazingira bora ya maisha
Serikali imeamua kuadhimisha miaka 20 ya uhuru chini ya kauli mbiu isemayo, ''Afrika Kusini-mahali bora pa kuishi''.
Katika kipindi hicho, uchumi umeongezeka mara tatu, na serikali imesema imejenga nyumba zipatazo milioni 3.7, kwa watu ambao hapo nyuma hawakuwahi kuishi katika nyumba za kisasa. Vile vile, watu milioni 15 katika ya milioni 51 wa nchi hiyo wanapokea msaada wa serikali.
Raia wengi weusi sasa wanao uhuru wa kuishi na kufanya kazi watakako katika nchi yao, na weusi ambao wanahesabiwa katika daraja la kati wameongezeka sana.
Hata hivyo bado kupishana kwa kipato kumewafanya maskini wengi kuandamana mitaani, wakilalamikia ukosefu wa huduma za msingi kama vile maji safi, umeme na makazi. Na Afrika Kusini bado ni miongoni mwa nchi zenye pengo kubwa sana kati ya matajiri na maskini.

Rais wa Ujerumani azuru Uturuki

Rais wa Ujerumani Joachim Gauck, alianza ziara yake ya siku 4 nchini Uturuki.
rais-wa-ujerumani-azuru-uturuki
Gauck kwanza alizuru mji wa hema  ambayo imehifadhi kumbukumbu za umoja ya askari wa Syria na Ujerumani  kisha  akaenda Kahramanmaras.
Rais wa Ujerumani Joachim Gauck, alianza ziara yake ya  siku  4 nchini Uturuki kwa kuzuru Kahramanmaras.Rais mgeni alikaribishwa na mkuu wa mkoa na meya wa mji huo.
Kahramanmaras , ambayo ni maarufu kwa utengenezaji  wa  barafu  ulimkaribisha Rais huyo  kwa maonyesho na kumpa fursa ya kujaribu barafu  iliyoipa mjii huo umaarufu.
Rais Gauck, siku ya mwisho ya wiki atawazuru Washami  wanaokaa katika mji  ya hema na  kisha kukutana na viongozi wa  ulinzi ya  askari wa Kijerumani.

Helikopta yaua watano Afghanistan:

Lynx helikopta ya Uingereza
Ajali ya helikopta nchini Afghanistan ambayo imeua askari wote watano wa Uingereza waliokuwa ndani ya helikopta hiyo ni "ajali ya kusikitisha", Wizara ya Ulinzi ya Uingereza imesema.
Helikopta hiyo, aina ya Lynx ilianguka chini kusini mwa Afghanistan, Jumamosi.
Kamanda wa Kamandi ya Pamoja ya Helikopta, Meja Jenerali Richard Felton, amesema ajali hiyo ni kuyakumbusha majeshi ya Uingereza ambayo yanaondoka nchini Afghanistan kuwa bado yanakabiliwa na hatari.
Waziri Mkuu David Cameron ametoa rambirambi kwa askari hao, ambao familia zao zimekwishaarifiwa kuhusu mkasa huo.
Askari watatu kati yao na mwanaanga mmoja wanatoka kambi ya kijeshi ya Hampshire. Askari wa tano, ambaye alikuwa katika kikosi cha jeshi la akiba, anatoka jijini London.
Hii ni ajali ya kwanza mbaya kusababisha vifo vya askari wote ikihusisha helikopta ya kijeshi ya Uingereza katika mgogoro wa Afghanistan lakini ni tukio la tatu kubwa kabisa kwa askari wa Uingereza kupoteza maisha katika tukio moja la ajali nchini Afghanistan tangu nchi hiyo ivamiwe na majeshi ya washirika mwaka 2001.

Papa atangazwa mtukufu


Papa Francis, kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani
Umati mkubwa wa watu wamekusanyika mjini Vatican kushuhudia tukio la kihistoria ambapo viongozi wawili wa zamani wa Kanisa Katoliki, Papa John Paul II na Papa John XXIII wametangazwa watakatifu.
Ibada iliyoendeshwa kwa pamoja kati ya Papa Francis na mtangulizi wake Papa Benedict XVI imeangaliwa na karibu mahujaji milioni moja na wengine mamilioni ya watu kupitia matangazo ya televisheni na redio.
Karibu ujumbe wa wageni 100 wamehudhuria sherehe hiyo, wakiwemo kutoka koo za kifalme na wakuu wa nchi na serikali.
Hii ni mara ya kwanza kwa papa wawili kutangazwa kwa wakati mmoja kuwa watakatifu.
Waandishi wa habari wanasema hatua hii inachukuliwa kama njia ya kuziunganisha kambi mbili za wapenda mageuzi na wasiotaka mabadiliko ya sheria katika Kanisa Katoliki.

Nyumba ya teketea kwa moto Iringa

mali zilizoteketea kwa  moto
Askari  wa  kikosi  cha  Zimamoto Iringa  wakiwajibika
MOTO  mkubwa  umezuka  katika  nyumba  ya mkazi  mmoja  wa  eneo la Zizi la Ng'ombe katika Halmashauri ya  Manispaa ya  Iringa na kupelekea mtu mmoja kupoteza  fahamu  baada ya  nyumba yake  kuwaka  moto majira ya  saa 8 mchana  wa leo.
Mashuhuda wa  tukio   hilo  wameueleza mtandao Huu kuwa  moto  huo  chanzo chake  kimesababishwa na mtoto mdogo  ambae  alikuwa  ndani ya  nyumba  hiyo akichezea  moto ndani ya  nyumba  hiyo na  kusababisha  moto  huo kushika makochi yaliyokuwemo ndani ya  nyumba  hiyo.

Nyumba  hiyo  mali ya  Bi Grace  Mpewa  imenusurika  kuteketea  yote  baada ya  wananchi  wa  eneo hilo kuendelea  kuzima  moto  huo bila ya  kutoa taarifa  jeshi la  zima moto na uokoaji mjini hapa  kiasi cha  moto  huo kuteketeza  sehemu kubwa ya  nyumba  hiyo .

Balozi  wa  eneo  hilo la  Zizi la Ng'ombe  Edmundi Kikula  alisema  kuwa  baada ya  kuzuka  moto  huo  walifika  kutoa msaada  na  kuanza  kuzima  moto  huo  huku mmiliki wa  nyumba  hiyo bila kuwepo na kuwa mtoto  huyo baada ya  kuulizwa alidai kuwa mama  yake  ndie  aliacha  jiko la moto huo .

Alisema  kuwa  mali mbali mbali  zimeteketea kwa  moto  huo huku baadhi ya  vitu  vikiokolewa  na  kuwa walishindwa  kutoa taarifa kwa  wakati  zimamoto kutokana na kukosa  namba  zao .

Hata  hivyo  aliwataka  wananchi  wenzake  kuhifadhi namba  za Zimamoto  ili  kutoa  taarifa  kwa wakati  pindi majanga kama  hayo yanapojitokeza badala ya  kuelekeza lawama  kwa kikosi  hicho.
Kwa  upande  wake  stafu  Sajenti  wa kikosi  cha zimamoto na uokoaji mjini  Iringa ambae  alikuwepo  eneo la  tukio Bw Juma Joseph Mkuvalo  alisema  kuwa  kufika kwao  eneo hilo  ni baada ya  kuitwa na jeshi la  polisi  kufuatia  mtandao huu   kufikisha  taarifa  za  tukio  hilo.
Mkuvalo  alisema  jamii  inapaswa  kukabiliana na  matukio ya moto  pale  yanapojitokeza na kuwa huduma  hiyo haina malipo  yoyote na kuwataka  wananchi  kutumia namba  za zimamoto ambayo ni 114 ili  kutoa taarifa.

CCM yafanya mikakati kumng´oa Lowassa

Dk. Migiro atumiwa kumdhibiti LowassaCHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimepanga mkakati mpya wa kuengua wataka urais wanaume kwa kuingiza hisia za kijinsia kama walivyofanya kumdhibiti aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa, Samuel Sitta, alipotaka kugombea tena nafasi hiyo mwaka 2010.
Wachunguzi wa masuala ya kisiasa wameliambia waandishi wetu Jumapili kuwa mkakati huo unalenga zaidi kumng’oa Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, ambaye anaonekana tishio kwa wenzake wanaotajwa kutaka urais.
Kwa mkakati huo, kundi la wana CCM walio karibu na Rais Jakaya Kikwete, wameanza kuzungumzia jinsi ya kumpitisha Dk. Asha-Rose Migiro agombee urais katika uchaguzi mkuu ujao 2015.
Kisingizio wanachotumia katika kampeni yao ya siri, ni kusaka kura za wanawake.
Katika mkakati huo, wanamwandaa Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe, kuwa Waziri Mkuu. Tayari Membe ameshatangaza kuwa hatagombea ubunge mwaka 2015.
Kwa mujibu wa vyanzo vyetu, Membe ndiye alikuwa akipigiwa chapuo zaidi miongoni mwa makada wa CCM ili kurithi mikoba ya Rais Kikwete, lakini kutokana na uhusiano wa kifamilia uliopo baina ya wawili hao, sasa ameshawishiwa kuwa atakuwa waziri mkuu endapo Dk. Migiro atashinda.
Wiki hii,  Jumatano iliripoti mkakati wa kumzima Lowassa asigombee urais, ambao unaendeshwa na mtoto wa kigogo akishirikiana na Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM).
Dk. Migiro ambaye kwa sasa ni Waziri wa Katiba na Sheria, na pia Mkurugenzi wa Idara ya Mahusiano ya Nje wa CCM, tayari ameanza kuzungushwa mikoani ili kumjengea uwezo na uzoefu wa kisiasa.
Miongoni mwa wana CCM wanaotajwa kuutaka urais 2015 mbali na Lowassa na Membe, ni Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano), Stephen Wasira, William Ngeleja na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba.
“Ukiwalinganisha Membe na Lowassa kwa nguvu na umaarufu ndani ya CCM, hata vigogo wengine wanaotajwa kuutaka urais, utaona hakuna wa kumshinda Lowassa, sasa ndani ya chama wameamua kumchezea rafu.
“Kwa vile ana mtandao mrefu ndani ya CCM, wanafahamu wakikata jina lake itakuwa balaa, hivyo wameona waibuke na hoja ya zamu ya wanawake kama walivyomzima Samuel Sitta asigombee uspika wakampa Anne Makinda,” alisema mtoa habari wetu.
Chanzo hicho kinaongeza kuwa mlengwa ni mtoto wa kigogo ambaye anaendesha mkakati wa kumchafua Lowassa ili 2025 ndiye awe mgombea urais baada ya Dk. Migiro kumaliza uongozi wake endapo atachaguliwa kwa vipindi viwili.
Pamoja na mkakati huo, kundi la Membe limeshauriwa kuendelea na harakati za kujiimarisha ili kuhadaa makundi mengine ndani ya chama yaamini kwamba naye ni miongoni mwa watakaochukua fomu za kuomba kuteuliwa kuwania urais.
Hata hivyo, wakati CCM ikiendesha mkakati huo dhidi ya Dk. Migiro ambaye amewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, baadhi ya wasomi wamemchambua mwanamama huyo wakisema hana uwezo huo.
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, alisema kuwa Dk. Migiro haonekani kubadilika licha ya kuwa na elimu kubwa.
“Nilimtembelea ofisini kwake akiwa UN kama Naibu Katibu Mkuu, nilikuwa na kazi za kitaifa kabisa kwa masuala yaliyoshirikisha mabalozi wa Ulaya, lakini aliponiona aliniuliza kwanini sitaki kurejea CCM.
“Huyu hawezi hata kubaini hapa tunazungumzia masuala ya kitaifa au kimataifa, yeye akili yake inawaza CCM tu kila wakati, hajaonyesha kutofautisha u-CCM wake na taaluma ili aweze kusaidia katika nyanja za kitaifa na kimataifa,” alisema.
Dk. Slaa aliongeza kuwa aliposikia kuwa Dk. Migiro ndiye aliyeandaa rasimu ya kwanza na ya pili ya katiba kwa upande CCM ambazo zinaleta shida kwa wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba zikikinzana na rasimu ya Tume ya Jaji Warioba, amedhihirisha kabisa udhaifu wake.
“Ukiangalia rekodi zake akiwa UN, huwezi ukaona matokeo yoyote, ndiyo maana Ban Ki moon hakutaka tena asaini mkataba kwa awamu nyingine kwani hakuwa na msaada kwake,” alisema Dk. Slaa.
Dk. Azavery Lwaitama ni mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Bukoba ambaye alisema kuwa Dk. Migiro sio mtu mwenye umaarufu wowote ambao unaweza kumfanya amweke katika orodha ya watu wanaoweza kuwa viongozi wa nchi hii.
“Aliteuliwa kuwa Waziri wa Jamii, Jinsia na Watoto, akafanya kazi kipindi kifupi na baadaye akafanywa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wakati wa awamu ya Rais Kikwete.
“Kutokana na kunong’onezana kati ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki moon na Rais Kikwete, Dk. Migiro aliteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na baadaye kwa utaratibu huo huo wa kunong’onezana akarejeshwa tena nchini,” alisema.
Dk. Lwaitama aliongeza kuwa vyombo vya habari vya nje viliandika vizuri kuhusu uwezo wa Dk. Migiro wakati akiwa Umoja wa Mataifa, lakini Watanzania hawakujishughulisha kuangalia yaliyoandikwa.
“Nilitarajia kuwa yeye atakuwa na mawazo tofauti katika mjadala wa rasimu iliyopo bungeni, lakini amerudi kwa wana CCM wenzake, anafikiri kama wao, analeta ushabiki wa makundi ya kisiasa, kwa utaratibu huo hawezi kuwa kiongozi anayefaa,” alisema.
Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (CHADEMA) ambaye ni mwanafunzi wa Dk. Migiro, alisema haoni dalili au uwezo wowote wa yeye kuwa kiongozi katika wadhifa huo mkubwa wa urais.
“Huyu hajawahi kushiriki uchaguzi wowote akashinda, ukiwemo hata ubunge, isipokuwa nafasi za kuteuliwa ambazo hupewa na marais.
“Angalia kwa mfano katika Bunge hili la katiba ametoa mchango gani wa kukumbukwa na wananchi licha ya kuchangia na kubaki katika Bunge linalotoa matusi na kuacha kujadili rasimu?” alisema Lissu.

BURUNDI ya haribu maadhimisho ya miaka Hamsini ya uhuru

Stars mpya majangaTIMU ya soka ya Tanzania, Taifa Stars, jana ilitibua furaha ya sherehe za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, baada ya kuchapwa mabao 3-0 na Burundi katika mechi ya kirafiki iliyopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Hadi mwamuzi Anthony Ogwayo wa Kenya anapuliza filimbi ya mapumziko, Burundi ilikuwa mbele kwa bao 1-0, likifungwa dakika ya 45 na mshambuliaji Didier Kavumbagu anayecheza soka ya kulipwa nchini katika klabu ya Yanga, akiunganisha kwa ustadi pasi ya Cedric Amisi.
Bao hilo liliwagawa mashabiki wa Yanga, ambao baadhi walishindwa kujizuia kushangilia.
Nje ya mgawanyiko huo wa mashabiki wa Yanga, wengine kushangilia bao la Kavumbagu huku wengine wakimzomea kwa kumtungua kipa wao kipenzi Deogratius Munishi ‘Dida’, zomeazomea nyingine ilikuwa ikimuandama kocha Salum Mayanga wa Stars.
Mayanga alikumbana na kadhia ya kuzomewa mwanzo mwisho kutokana na mashabiki kukerwa na kikosi alichokipanga, ambacho kilijumuisha nyota watano waliotokana na programu ya maboresho ya Stars, huku akiwaacha wanaoshabikiwa na mashabiki.
Bao la Kavumbagu lilikuja dakika moja baada ya kukosa bao jingine, kutokana na juhudi binafsi za Said Moradi, aliyeokoa mpira uliokuwa ukienda nyavuni baada ya Dida kupotezwa maboya akijaribu kudaka.
Mashambulizi hayo yalikuja baada ya Stars kupoteza nafasi mbili huku Burundi ikipoteza moja, katika mechi ambayo ilikuwa na mashabiki wachache, licha ya Rais Jakaya Kikwete kuamuru waingie bure kama sehemu ya kusherehekea miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Mapema dakika ya 20, Yosso aliyetokana na programu ya maboresho ya Stars, Mohammed Seif, alikosa bao la wazi, akishindwa kabisa kupiga kichwa kumalizia krosi ya winga Simon Msuva, ambaye alikuwa mwiba kwa mabeki wa Burundi.
Intamba Mu Rugambaa, ikalipa shambulizi hilo dakika 10 baadaye, kwa kulifikia lango la Stars, lakini Cedric Amisi akashindwa kufunga, baada ya shuti lake kumbabatiza kipa na mabeki kuondoa hatari langoni mwao.
Mapema kabla ya pambano kuanza, mashabiki wa soka waliokuwa tayari na tiketi mkononi walikuja juu wakitaka warejeshewe pesa zao, hasa baada ya Rais Kikwete kuamuru waingie bure uwanjani hapo.
Baada ya mashabiki hao kuja juu, ndipo walipotakiwa kujikusanya ndani ya uzio wa uwanja ili kuonyesha tiketi zao tayari kwa kurudishiwa pesa zao, lakini katika namna ya kustajabisha, dereva wa gari lililodaiwa kubeba fedha za marejesho aliwasha gari hiyo na kutoweka uwanjani hapo bila kurejesha fedha.
Uamuzi wa dereva huyo kukimbia na ‘haki za watu’ uliwakera mashabiki, ambao walianza vurugu ndogo zilizokuwa zikitulizwa na askari polisi, ambao walikabiliwa na upinzani kutoka kwa mashabiki hao, wakiwaambia; “tuueni, tuueni, tunataka haki zetu. Rais karuhusu tuingie bure uwanjani.”
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi Stars wakisaka bao la kusawazisha, lakini walikuwa ni Burundi tena, ambao iliwachukua dakika 12 kupata bao maridadi, likifungwa na mshindi wa kiatu cha dhahabu cha Ligi Kuu ya Vodacom, Amisi Tambwe, baada ya Dida na mabeki wake kuokoa shuti la Kavumbagu.
Bao hilo liliamsha shangwe uwanja mzima, kana kwamba limefungwa na Stars, kutokana na mashabiki wa Simba nao kushangilia bao la nyota wao huyo, huku Yanga nao wakiendeleza ushangiliaji wao kwa wageni waliouanza mapema.
Wakati wachezaji wa Stars wakitafakari kilichotokea, huku kocha Mayanga akifanya mabadiliko matatu kwa mkupuo, Burundi walijipatia bao la tatu, likiwekwa kimiani na Ndikumana Yusuf dakika ya 62 kwa shuti la mbali alilopiga akiwa katikati ya duara la kuanzishia mpira na kumtundua Dida aliyetoka langoni.
Baada ya mabao hayo, Stars walipoteana mchezoni kiasi cha ‘kuwapa kusema’ mashabiki ambao waliwazomea mwanzo mwisho, huku wakiwashangilia Burundi waliokuwa kama wako dimba la nyumbani.
Hadi filimbi ya mwisho, Stars ilitoka bila kutikisa nyavu za Burundi, huku wageni hao wakifunga mara tatu na kutibua sherehe za muungano miongoni mwa Watanzania.
Stars: Deogratius Munishi ‘Dida’, Omari Kindamba, Edward Peter, Aggrey Morris, Said Moradi, Said Juma/Himidi Mao, Simon Msuva, Frank Domayo, Ayoub Lipati/Haruna Chanongo, Mohamed Seif/Jonas Mkude na Ramadhani Singano.
Burundi: Arthur Arakaza, Kiza Fataki, Rugonumugabo Stephane, Issa Hakizimana/Nkurukiye Leoprd, Rashid Leon/ShabanHussein, Ndikumana Yusuf, Steve Nzigamasabo/Idd Jumapili, Cedric Amis, Didier Kavumbagu, Pascal Hakizimana na Amisi Tambwe.
Katika hatua nyingine, askari polisi Raphael Maganga, jana aliibiwa pikipiki namba T 454 CUP, aliyokuwa ameipaki ndani ya uwanja.

JB afungua kasino Babu kubwa

KAKA mkubwa anayeongoza kwa mvuto kwenye sinema, Steven Jacob ‘JB’ ndiye msanii pekee kati ya wasanii wa filamu za Kibongo aliyealikwa kwenye uzinduzi wa Casino kubwa la kisasa la Princess lililopo katikati ya Jiji la Dar es Salaam.
JB alialikwa na wageni wengine maarufu akiwemo Balozi wa Uturuki nchini, Ali Davutoglu aliitumia fursa hiyo kutanua mtandao wa kufahamiana na watu wengi mashuhuri.
Balozi Davutoglu alisema Casino hiyo ni sehemu muhimu kwa wasanii, wanamuziki na watu wanaopenda sanaa na utamaduni wa Tanzania na nchi nyingine kukutana na kubadilishana mawazo.
Naye JB aliliambia gazeti hili kwamba amefurahia mwaliko huo na kuongeza kuwa sehemu hiyo ni muhimu sana kwa wasanii wa filamu, wanamuziki na watu wengine kujumuika pamoja na kupata uzoefu wa kimataifa.

Wazee wamchagua JK

Wastaafu wamteka JKRAIS Jakaya Kikwete amehujumiwa na viongozi wakuu wastaafu waliomlazimisha kuachana na msimamo wa muundo wa muungano wa serikali tatu na kukumbatia serikali mbili zilizopendekezwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Taarifa kutoka kwa baadhi ya vyanzo vya habari vilivyo karibu na rais, Ikulu na makao makuu ya CCM, zimelithibitishia gazeti hili kwamba hadi Bunge Maalumu la Katiba linaanza, Rais Kikwete alikuwa na msimamo ule ule wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Baadhi ya viongozi wastaafu, wakiwamo marais na viongozi waandamizi wa CCM, walishinikiza rais aachane na serikali tatu, kwa vitisho kwamba zitaua muungano.
Baadhi ya wastaafu hao walimficha Rais Kikwete kwamba kwa kuwa yeye aliingia madarakani akiwa rais wa muungano wa serikali mbili, halikuwa jambo la busara kwake kujiingiza kwenye historia ya kuwa rais aliyevunja muungano.
Kwa mujibu wa vyanzo vyetu, shinikizo hilo liliambatana na jingine la kumtaka asizindue Bunge kabla ya rasimu ya pili ya katiba mpya kuwasilishwa bungeni, ili apate fursa ya kudhoofisha hoja ya serikali tatu.
Mara baada ya Rais Kikwete kukubaliana na “washauri wake”, serikali ililazimika kuingilia kati ili Mwenyekiti wa Bunge, Samuel Sitta atengue kanuni, Mwenyekiti wa Tume, Jaji Joseph Warioba awasilishe rasimu kabla ya rais kuzindua Bunge, jambo ambalo limesababisha mvurugano unaotishia kuvuruga kabisa mchakato wa katiba mpya.
Hata hivyo, hali hiyo inasemekana kumnyima amani Rais Kikwete ambaye ndiye aliyepokea na kusaini rasimu hiyo, kwa maana kwamba aliridhia.
Uamuzi huo umefanya rais aonekane kiongozi asiye na msimamo thabiti katika masuala muhimu.
Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanadai hatua hii imemfanya ashindwe kuacha urithi makini na muhimu katika utawala wake wa miaka 10, kama ambavyo alikuwa amedhamiria.
Wadadisi wanasema wastaafu walimzuia rais kutekeleza azima yake kwa sababu ya hofu tu, wakidhani kwamba katiba mpya yenye mfumo mpya inaweza kufumua mambo yaliyofichika na kuwaingiza matatani.
Wanadai kwamba muungano wenye mfumo mpya una kila dalili za kuiondoa CCM madarakani, na kuhatarisha maslahi ya watawala waliopo na waliopita.
Hoja hii, kwa mujibu wa vyanzo vyetu, ndiyo ilimkuna Rais Kikwete hata akabadili msimamo.
Kwa hali halisi ilivyo, na mchakato unavyoendelea, ahadi ya Rais Kikwete kuwapa Watanzania katiba mpya mwezi huu imeshindikana.
Alipohutubia taifa na kutangaza kuanzisha mchakato wa katiba mpya miaka mitatu iliyopita, alisema kwamba lengo lake lilikuwa kuzindua katiba mpya katika maadhimisho ya sherehe za miaka 50 ya muungano iliyofanyika jana.
Hadi Bunge Maalumu la Katiba linaahirishwa juzi, zilikuwa zimepita siku 68 kati ya 70 zilizotengwa kwa ajili ya Bunge hilo, huku kukiwapo mgawanyiko mkubwa wa wajumbe na kutishia uhai wa muungano, hasa baada ya wajumbe wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kususia Bunge baada ya kukerwa na hujuma na matusi kutoka kwa wajumbe wenzao wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Hadi sasa Bunge la Katiba limefanikiwa kujadili sura mbili za rasimu bila ya kuzipigia kura. CCM imekataa maoni ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba yanayopendekeza mfumo wa muungano wa serikali tatu, wakatetea mfumo wa serikali mbili.
Mapendekezo hayo ni kinyume kabisa cha yaliyomo kwenye rasimu ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyowasilishwa ili ijadiliwe na wajumbe hao na kisha kutunga katiba mpya.
UKAWA wanadai kuchoshwa na vitisho na matusi kutoka kwa wajumbe wa CCM na viongozi wa serikali, wakisema kuwa kwa hali ilivyo katiba bora ya wananchi haiwezi kupatikana kwa shinikizo la muundo wa serikali mbili.
Katika hili, Rais Kikwete analalamikiwa kuwa ndiye mvurugaji wa kwanza wa mchakato ambao aliuasisi na kuahidi kuwapatia wananchi katiba bora kabla ya kuondoka madarakani.
Wakati akilihutubia Bunge la Katiba na kulizindua rasmi Machi mwaka huu, Rais Kikwete aliibeza rasimu ya Tume ya Jaji Warioba, akisema takwimu zao kuhusu watu waliotoa maoni ya muundo wa muungano zinatiliwa shaka.
Alisema kuwa muundo wa serikali tatu unaopendekezwa hautekelezeki kwani rais wa dola hiyo hatakuwa na mamlaka kwa vile hana ardhi, rasilimali na hivyo hataweza kukopa.
Kwa mujibu wa Rais Kikwete, katika hali kama hiyo, jeshi linaweza kupindua serikali na hivyo ukawa mwanzo wa kuvunjika kwa muungano, huku akisisitiza kwamba wao kama CCM muundo ambao unaweza kutatua kero zilizopo ni ule wa sasa wa serikali mbili.
Kauli hiyo ya rais iliibua mjadala mkubwa, na hivyo kufifisha ndoto za kupatikana kwa katiba bora kwani ilionyesha wazi kwamba mapendekezo ya wananchi ya serikali tatu yaliyomo kwenye rasimu hayatazingatiwa.
Hali hiyo imeendelea kujitokeza kwenye Bunge Maalumu la Katiba baada ya wajumbe wote wa CCM kuendeleza msimamo wa rais wa serikali mbili na kumshambulia Jaji Warioba binafsi kwa matusi mazito wakidai ana ajenda ya kuvunja muungano kwa kupendekeza serikali tatu.
Hatua ya Rais Kikwete kubadilika na kuvuruga mchakato aliyouasisi na kuusimamia kwa mafanikio makubwa, imeelezwa kusababishwa na mambo makubwa mawili, likiwemo hilo la kuburuzwa na viongozi wastaafu.
Duru nyingine za kisiasa katika suala hilo la kukwama kwa mchakato wa katiba, zinahusisha na rasilimali ya gesi na mafuta zilizopatikana nchini, ambapo inadaiwa mataifa makubwa yanayotaka kuwekeza ndiyo yanaishinikiza serikali isibadili muundo wa muungano uliopo.
Vyanzo vyetu vya habari vinaeleza kwamba mataifa hayo tayari yameweka msimamo wa kuisaidia CCM kifedha ili kuhakikisha inapigana kufa au kupona kutobadili muundo wa muungano katika katiba mpya.
Inaelezwa kuwa muundo wa shirikisho la serikali tatu unaopendekezwa kwenye rasimu ya katiba mpya, unatoa fursa ya wazi kwa wananchi wa serikali washirika kusimamia rasilimali zao tofauti na ilivyo katika muundo wa sasa ambapo mambo mengi yamefanywa siri na serikali.
Hadi sasa majaliwa ya kupatikana kwa katiba mpya yametoweka baada ya UKAWA kujiondoa, na hivyo kulifanya Bunge la Katiba kushindwa kufanya maamuzi ya kupitisha ibara na sura za rasimu kutokana na theluthi mbili ya wajumbe kutoka Zanzibar kushindikana.

Morgan Tsvangirai asimamishwa uongozi MDC


Morgan Tsvangirai
Chama cha upinzani nchini Zimbabwe cha Movement for Democratic Change MDC kimesema kimemsimamisha kiongozi wake Morgan Tsvangirai kwa kukiuka kanuni za kidemokrasia.
Taarifa hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa MDC Tendai Biti kufuatia mkutano wa chama hicho uliofanyika katika mji Mkuu Harare.
Tangu mwaka 2009 hadi 2013 Bwana Tsvangirai alitumikia taifa la Zimbabwe katika nafasi ya Waziri Mkuu katika serikali ya umoja wa kitaifa iliyoundwa kwa pamoja na Rais wa sasa Robert Mugabe.
Serikali ya Umoja wa Kitaifa ilifikia kikomo mwezi julai mwaka 2013 baada ya Rais Mugabe kushinda kwa wingi wa kura katika uchaguzi wa rais na Tsvangirai kususia uchaguzi kwa madai ya udanganyifu.
Kushindwa kwake kulipunguza nguvu yake kama kiongozi ambaye alikuwa mshindani mkuu wa Rais Mugabe.
Waangalizi wanasema ndani ya MDC kumekuwa na mgogoro wa kiuongozi kwa miezi kadhaa.
Viongozi wengine wa ngazi za juu wameripotiwa kusimamishwa katika mkutano huo uliofanyika siku ya jumamosi na wanachama wengine wa chama hicho watachukua nafasi zao.

Saturday 26 April 2014

Jaydee anapiga karate hatari

WAKATI sherehe za miaka 41 ya Chuo cha Karate cha Okinawa Goju Ryu cha Dar es Salaam zikifanyika leo Jumamosi, mmiliki wa Bendi ya Machozi, Lady Jaydee atatunukiwa mkanda mweupe baada ya kufanya vyema katika mafunzo.
Kwa mujibu wa mkuu wa chuo hicho, Sensei Wilfred Malekia, shehere za chuo hicho zimepangwa kuanza saa 12 jioni Shule ya Zanaki, Dar es Salaam.
Malekia alisema katika sherehe hizo mambo mbalimbali yatafanyika ikiwamo kuadhimisha kumbukumbu za muasisi wa chuo hicho, marehemu Camara Bomani Goju Ryu Jundokan aliyefariki mwaka 2009.
“Hii ni sherehe muhimu kwetu, itawakutanisha watu mbalimbali waliopitia mafunzo katika chuo hiki ambao wanafanya shughuli zao nyingine,” alisema Malekia.
Akimzungumzia Lady Jaydee, Malekia alisema kuwa mwanamuziki huyo amejiunga na chuo hicho  miezi sita iliyopita na amekuwa akifanya vyema katika mafunzo yake.
Mbali na Lady Jaydee ambaye pia anafahamika kwa jina la Komando, wanawake wengine watatu nao watavishwa mkanda mweupe.
“Mafunzo haya ni muhimu sana katika maisha ya kila siku, ndiyo maana katika chuo chetu, kuna wanafunzi wa rika mbali mbali ambao wanafanya mafunzo hapa,” alisema.
Kwa upande wake, Jaydee alisema kuwa ameamua kujiunga na mafunzo hayo kwa sababu mbalimbali ikiwamo kumpa stamina katika kazi yake ya kuimba na kujilinda.
Alisema kuwa mazoezi hayo yanamfanya awe na uwezo wa kufanya shoo zake mbali mbali tokea mwanzo hadi mwisho bila kuchoka.

Tunaweza Lierpool

MERSEYSIDE, LIVERPOOL
KAMA Barrack Obama alivyowaambia Wamarekani katika harakati za kampeni za uchaguzi wao mwaka 2008 kuwa wanaweza kumaliza matatizo yao, ndivyo kocha, Brendan Rodgers, alivyowaambia mashabiki wa Liverpool kuwa wanaweza kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu England.
Juzi Jumapili usiku, harufu ya ubingwa wa ligi hiyo ilianza kunukia katika viunga vya Anfield huku pia mashabiki wengine wa timu hiyo duniani wakianza kuingiwa na kiwewe baada ya Liverpool kuichapa Tottenham mabao 4-0.
Wana nafasi kubwa ya kuwa mabingwa kama wakishinda mechi zao sita zilizobaki ambapo mbili kati ya hizo watacheza na wapinzani wao katika mbio hizo Chelsea na Manchester City.
Rodgers ana uhakika kuwa timu yake hii ina uwezo mkubwa wa kuhimili presha na kutwaa ubingwa hasa katika kipindi hiki ambacho wanaongoza msimamo wa ligi hiyo.
“Bado kuna pointi nyingi za kuzisaka na lazima kuna pointi zitakazopotezwa na timu zote kabla ya mwisho wa msimu. Hatuna presha yoyote na tuna uhakika kwa jinsi tunavyocheza,” alisema Rodgers ambaye alitua Anfield akitokea Swansea.
“Ndoto ya mashabiki wetu ni kutwaa ubingwa. Imekuwa muda mrefu sana tangu walipotwaa, lakini mimi haipo katika mawazo yangu. Tunahitaji kujiandaa tu na kufanya vizuri na kama tukifanya hivyo tutashinda mechi zetu.
“Chelsea na Manchester City wanajua kwamba Anfield itakuwa sehemu ngumu kuja. Tunapenda kucheza hapa, tunapata sapoti kubwa na hilo linasababisha tuongeze ari. Tunawaheshimu Chelsea, wana kocha wa kiwango cha juu sana na wana timu ambayo wameikusanya kwa ajili ya kushinda Ligi ya Mabingwa na Ligi Kuu.
“Manchester City ni miongoni mwa wababe wapya wa soka duniani, lakini tunadhani tunaweza kushinda mechi yoyote kwa sababu sisi ni timu. Tuna njaa na mbinu zetu za kisoka zinaimarika kila siku.”

Samatta apiga ‘ hat trick’ TP Mazembe

straika wa TP Mazembe, Mbwana Samatta akiokota mpira kwenye nyavu za timu pinzani

 
NYOTA ya straika wa Mbwana Samatta imezidi kung’aa klabuni TP Mazembe baada ya juzi Jumatano kuifungia mabao matatu ‘Hat Trick’ timu yake na kuisaidia kushinda mabao 4-1 dhidi ya AS Vita.
Katika pambano hilo la watani wa jadi kuwania ubingwa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) lililochezwa kwenye Uwanja wa Stade TP Mazembe huko Kamalondo, Lubumbashi, Mtanzania huyo alionekana kuwa mwiba mkali kwa AS Vita yenye makao makuu yake Kinshasa.
Samatta aliyekuwa anaichezea Simba kabla ya kujiunga na TP Mazembe, alifunga mabao hayo katika dakika za 51, 71 na 85 huku Rainford Kalaba akiwa wa kwanza kuifungia timu hiyo katika dakika ya nane. Bao la AS Vita lilifungwa na Patou Ebunga dakika ya 16.
Tangu alipojiunga na TP Mazembe mwaka 2011, Samatta amekuwa mmoja kati ya wachezaji tegemeo wa timu hiyo kiasi cha kujizolea mashabiki wengi katika kila pembe ya Lubumbashi na kuipeperusha vizuri Bendera ya Tanzania.
Samatta sambamba na Mtanzania mwingine anayechezea timu hiyo, Thomas Ulimwengu waliitwa katika kikosi cha Taifa Stars kitakachocheza mechi ya kirafiki na Burundi kesho Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, lakini wameshindwa kuja kutokana na majukumu yao katika klabu hiyo.
Keshokutwa Jumapili, Samatta anatarajiwa kuichezea tena TP Mazembe dhidi ya Don Bosco katika mwendelezo wa michuano hiyo.

Tambwe ahamishia nguvu ufukweni

LIGI Kuu Bara msimu wa 2013/14 imemalizika huku straika wa Simba, Amissi Tambwe, akiibuka Mfungaji Bora baada ya kufunga mabao 19. Lakini mchezaji huyo amekaa siku chache tu nje ya uwanja na sasa anafanya mazoezi katika ufukwe wa Coco jijini Dar es Salaam.
Akiwa ufukweni hapo, Tambwe hufanya mazoezi ya kukimbia ili kuongeza pumzi za kupambana uwanjani na yale ya kujenga stamina ili aweze kuwapenya kwa nguvu mabeki wa timu pinzani.
Yote hayo anajiandaa kwa msimu mpya unaotarajiwa kuanza Agosti. Kwa mabao hayo 19 aliyofunga, Tambwe alimzidi straika wa Azam FC, Kipre Tchetche aliyefunga mabao 14 huku Didier Kavumbagu wa Yanga na Elius Maguli wa Ruvu Shooting,
kila mmoja akifanya hivyo mara 13. Akizungumza na Mwanaspoti, Tambwe ambaye alitarajiwa kuungana na kikosi cha Burundi kilichotarajiwa kuwasili jana jijini Dar es Salaam tayari kwa mechi ya kirafiki dhidi ya Taifa Stars ya kesho Jumamosi, alisema ameamua kufanya mazoezi ufukweni ili kujiweka vizuri kwa msimu ujao wa ligi.
Mechi hiyo itakayochezwa Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam pia ni sehemu ya maadhimisho ya sherehe za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
“Kwa sababu kwa sasa mazoezi ya timu yamesimama kwa muda, huwa naenda kwenye fukwe wa Coco na kufanya mazoezi yangu binafsi kama kukimbia na mambo mengine,” alisema.
“Huwa sifanyi kila siku, ila sina siku maalumu, inategemea na siku hiyo nahitaji kufanya mazoezi yangu kwa namna gani.
“Hii yote nafanya kwa sababu maisha yangu yanategemea soka hivyo lazima nihakikishe nipo vizuri muda wote ili mambo yasiniharibikie, si unajua mpira sasa ni ushindani? Hakuna anayekubali kuachwa kirahisi uwanjani.”
Tambwe ni miongoni mwa wachezaji wa kigeni walioonyesha uwezo mkubwa katika kuzifumania nyavu na kuongeza msisimko wa ligi kuu, raia wa kigeni wengine waliofanya vizuri katika ligi hiyo ni Tchetche raia wa Ivory Coast, Mrundi Kavumbagu wa Yanga na Mganda Hamis Kiiza pia wa Yanga aliyefunga mabao 12.
Tambwe alijiunga na Simba mwanzoni mwa msimu uliopita akitokea Vital’O ya Burundi sambamba na beki Gilbert Kaze. Hata hivyo Kaze hakucheza mechi za mzunguko wa pili kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya goti.

Okwi atimka kimya kimya

Emanuel Okwi akisubiria nyaraka zake kukaguliwa ili aweze kuanza safari yake ya kuelekea Uganda                            
 WACHEZAJI wa Yanga washambuliaji Emmanuel Okwi na Hamis Kiiza wameondoka jana Jumatano jijini Dar es Salaam lakini cha kushangaza ni usiri wa safari yao.
Okwi ambaye hadi anaondoka jana saa tatu usiku alikuwa katika mgomo wa kutoichezea timu yake kutokana na madai ya fedha kiasi cha dola 40,000 (Sh 64 milioni) ndiye alikuwa wa kwanza kufika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akimtangulia Kiiza.
Mara baada ya kumuona mwandishi wa Mwanaspoti huku akipigwa picha za kutosha alionekana kushangazwa akiuliza nani ametoa siri ya safari yake.
Akiwa katika mshangao kuhusu kuvuja kwa siri ya safari yao ya usiku, Okwi ambaye aliletwa na gari aina ya Noah yenye namba za usajili T367 CJC alisema kwa kifupi kwamba anaondoka akirudi kwao Uganda kupumzisha akili yake kufuatia msimu wa Ligi Kuu Bara kumalizika.
Hata hivyo aligoma katakata kueleza undani wa mgomo wake ingawa Mwanaspoti lina uhakika kwamba anaidai Yanga fedha hizo ikiwa ni mabaki ya dau lake la usajili na hajalipwa.
“Nani amewaambia naondoka saa hizi? Hebu nitajie, Ok kifupi narudi nyumbani kupumzika ligi imekwisha hilo ndilo ninaloweza kusema, nimechelewa jamani naomba mniache nitaachwa na ndege,” alisema Okwi.
Na ingawa alificha kinachoendelea kati yake na Yanga, mmoja wa rafiki zake ameliarifu Mwanaspoti kuwa mchezaji huyo ameondoka lakini hajamalizana na uongozi wa klabu hiyo ambao umemuwekea ngumu kummalizia fedha zilizosalia huku akidaiwa kushindwa kuonyesha uwezo uliotarajiwa katika kipindi cha miezi sita ya usajili wake.
Dakika 20 baadaye Kiiza naye alitua uwanjani hapo na alipoulizwa kuhusu kuondoka kwake alisema anarudi kwao lakini hajajua siku ya kurudi.
“Foleni zimenimechelewesha jamani, narudi nyumbani ligi imekwisha nakwenda kupumzika ingawa nitakuwa na timu ya Taifa ya Uganda, sijui nitarudi lini kutokana na ratiba ya mechi za timu ya taifa,” alisema Kiiza.

Simba yatema kikosi kizima

Wachezaji wa Simba wakipewa maelekezo na Kocha Logarusic.

Kocha wa Simba, Zdravko Logarusic amesema analazimika kutema wachezaji wasiopungua 11 ambao ni sawa na kikosi kizima kinachoweza kucheza mechi ya ushindani.
0Share
UKITAKA mafanikio lazima uchukue uamuzi mgumu ambao hakuna anayeweza kufikiria kabla.
Kocha wa Simba, Zdravko Logarusic amesema analazimika kutema wachezaji wasiopungua 11 ambao ni sawa na kikosi kizima kinachoweza kucheza mechi ya ushindani.
Lengo la Logarusic kufanya hivyo ni ili aweze kujenga upya timu ya ushindani msimu ujao.
Logarusic sasa ana uhakika wa kubaki Simba, baada ya kuhakikishiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya klabu hiyo, Zacharia Hans Pope kwani awali hakuwa na uhakika wa kuendelea kubaki katika timu hiyo kutokana na mkataba wake kumalizika.
Kocha huyo atasaini mkataba wa miaka miwili baada ya ule wa miezi sita kufikia tamati.
Katika ripoti yake kwa uongozi wa timu hiyo, Logarusic amewaeleza wazi viongozi wake kuwa, ili Simba iwe na ushiriki mzuri msimu ujao wa Ligi Kuu Bara lazima nyota 11 wa timu hiyo waachwe ili wapatikane wengine watakaoisaidia timu kufikia mafanikio.
Akizungumza na Mwanaspoti usiku wa kuamkia jana Ijumaa dakika chache kabla ya kupanda ndege kwenda kwao Croatia kwa mapumziko, Logarusic alisema wachezaji anaotaka kuwaacha si kwamba hawana viwango vizuri, tatizo hawana nafasi kikosi cha kwanza.
“Simba inahitaji ubingwa, unawezaje kuupata bila ya kuwa na wachezaji wenye uwezo? Nimekabidhi ripoti yangu tayari kwa uongozi sioni sababu ya kuficha mambo yaliyo wazi ni kwamba nataka kubaki na wachezaji 13 tu katika kikosi cha sasa.
“Nimewaambia viongozi nataka kurudi kuanzia Juni kufanya kazi moja ya kurudisha heshima ya timu hii, katika hilo hao niliowaona hawana nafasi Simba watajua kwa kuwapeleka, chini yangu hawana nafasi, nataka wachezaji wenye uzoefu mkubwa na wanaozitumikia timu za taifa.
“Tazama benchi nina wachezaji wengi kuliko kikosi cha kwanza na ikitokea mchezaji mmoja anaumwa napata presha sina mtu wa uhakika wa kumpanga,’’ alisema Logarusic.
Amemaliza kazi
Logarusic ameshapiga mstari mwekundu katika orodha ya wachezaji 24 walioichezea Simba mzunguko wa pili wa msimu uliopita na kubaki na 13 tu hivyo 11 wataachwa kwa makubaliano maalum au kupelekwa kwa mkopo timu nyingine. Kabla hajaanza kuiongoza Simba, Logarusic alikuwa na wachezaji 36 ambao aliwapunguza na kubaki 24 tu.
 
 
Sababu kubwa ya kupunguza wachezaji hao ambao hakukuwa na hata mmoja aliyesajiliwa na kocha huyo ni uwezo mdogo huku wengi wakionekana kutoweza kupambana uwanjani.
Hata hivyo inadaiwa kwamba baadhi ya wachezaji wenye umri mdogo kati ya 11 wasiotakiwa na Logarusic watarudishwa Simba B ili kukuza viwango vyao.
Wanaobaki
Ingawa nyota watakaochwa imekuwa siri nzito lakini tathimini ya Mwanaspoti imebaini kuwa wenye nafasi kubwa ya kubaki ni Joseph Owino, Donald Mosoti, Nassoro Masoud ‘Chollo’, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’ na William Lucian ‘Gallas’ wakati viungo ni Jonas Mkude, Said Ndemla, Ramadhan Singano, Awadh Juma, Amri Kiemba, Haroun Chanongo na mshambuliaji ni Amissi Tambwe pekee.
Watakaoachwa.
Wachezaji walio katika hatari ya kuachwa ni kipa Yaw Berko, Uhuru Seleman, Henry Joseph ambao mikataba yao imeisha. Wengine ni Abuu Hashim na Bertam Mwombeki ambao inadaiwa hawana maelewano mazuri na Logarusic huku Hassan Hatib, Ally Badru, Ramadhan Chombo ‘Redondo’, Abduhalim Humud na Zahoro Pazi wakidaiwa kutojituma na kuonyesha uwezo uwanjani.
Katibu Mkuu wa Simba, Ezekiel Kamwaga alikiri kupokea ripoti hiyo na kusema: “Tumepokea ripoti ya kocha, kuna wachezaji amependekeza tuwaache lakini kwa sasa hatuwezi kuweka wazi majina yao.
“Tunataka kwanza kuyafanyia kazi kama viongozi na baada ya hapo tutakutana nao kuzungumza jinsi ya kuachana nao, kazi hiyo tutaifanya Jumatatu (keshokutwa).

wawili mbaroni kwa mauaji ya mwanafunzi

JESHI la Polisi mkoa wa kusini Pemba, linawashikilia vijana wawili marafiki wa karibu wa marehemu  Mohamed Soud Makame (17),  wakidaiwa kuchangia  mauaji yake.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Kamanda wa Polisi mkoani humo, Juma Yuuf Ali, alisema vijana hao wenye umri wa miaka 17 na 21 walishawishika kuwahoji kutokana na ukaribu waliokuwa nao na marehemu kabla ya kifo chake.

Alisema vijana hao wote walikamatwa wakiwa nyumbani kwao shehia ya Wawi wilaya ya Chake Chake na mara watakapomaliza kuwahoji wakihisi wanahusika na kifo cha marehemu huyo watafikishwa mahamani.

Hivyo aliwataka ndugu na jamaa wa marehemu huyo, kuwa watulivu na wastahamilivu, wakati huu jeshi la polisi likendelea na uchunguzi ili haki itendeke.

“Sisi Jeshi la polisi kwetu ni kuwataka wananchi na hasa ndugu na jamaa wa marehemu Mahamed Soud Makame, kuwa wastahamilivu na kutoa ushirikiano na jeshi letu, ili liweze kukamilisha kazi yake kwa ufanisi,’’ alisema.


Katika hatua nyengine Kamanda huyo,alisema juzi mara baada ya kutokezea kifo hicho,  kwa hatua za awali walibaini marehemu alifanyia ukatili kwa kuuliwa eneo la mbali na kisha mwili wake kufikishwa kwenye nyumba ambayo haijahamiwa.

“Unaweza kusema kuwa kifo chake sio cha kawaida, maana uchunguzi wetu ulibaini kuwa alikuwa na michubuko sehemu mbali mbali za mwili wake na wala hakuuliwa kwenye eneo ambalo tulimkuta bali pale aliletwa akiwa ameshakufa,” alisema.

Daktari Ali Hamran Mohamed wa hospitali ya Chake Chake, alieufanyia uchunguuzi mwili wa marehemu, alisema inaonesha kifo chake kilisababishwa na kuekewa kitu kizito shingoni, mithili ya kamba na kusababisha ulimi kutoka nje.

Kerry ashutumu Urusi kwa ghasia Ukraine

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani John Kerry akizungumza na mwenzake wa Urusi Sergei Lavrov.
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani amelaumu Urusi kwa kuchochea mapigano Mashariki mwa Ukraine.
John Kerry alisema ujasusi wa Marekani una hakika kuwa Urusi imetoa silaha na wapiganaji na pia inaendelea kugharamia na kusimamia wapiganaji wa nchini Ukraine kushiriki ghasia hizo.
Katika lugha ya hasira, Bwana Kerry, alishambulia Urusi akisema kuwa taifa hilo limeshindwa kuchukua hatua madhubuti za kujaribu kutuliza uhasama ulioko nchini Ukraine kama ilivyokubaliwa mjini Geneva juma lililopita.
Bwana Kerry alisema kuwa Urusi inasimamia ghasia zinazoendeshwa na watu wanaotaka kujitenga kutoka kwa Ukraine Mashariki mwa taifa hilo na kujaribu kusababisha ghasia ili kuhujumu uchaguzi unaotazamiwa kufanywa mwezi ujao.
Kwa hasira, Bwana Kerry alilaumu Urusi kwa ghasia zote zinazoendelea Ukraine wakati huu. Ingawa hakutangaza vikwazo inavyoweza kuongezewa Urusi Bwana Kerry alisema mwanya wa kuimarisha amani katika Ukraine unaendelea kuziba.

G7 kuiwekea Urusi vikwazo zaidi

wanamgambo wanaeondelea kuyadhibiti majengo ya serikali mashariki mwa Ukraine.

Viongozi wa nchi zenye uwezo mkubwa duniani G7 wamekubaliana kuiwekea vikwazo zaidi Urusi, wanayosema inaendelea kuchochea ghasia mashariki mwa Ukraine.
katika taarifa yao, viongozi hao walionyesha wasiwasi wao kuhusu jitihada za wanaharakati wanaounga mkono Urusi kuendelea kuyumbisha mashariki mwa Ukraine.
Urusi ,wamesema haijachukua hatua zozote kutekeleza makubaliano ya mjini Geneva mbali na kuwaamrisha wanamgambo hao kuondoka katika majengo ya serikali wanayodhibiti.
Hatahivyo viongozi hao wameipongeza Ukraine kwa kujizuia katika kukabiliana na makundi ya wanamgambo yaliojihami.
Wakati huohuo, wanamgambo wanaounga mkono Urusi mashariki mwa mji wa Ukraine wa Slavianski wamelitekanyara kundi moja la wachunguzi 13 wa kimataifa pamoja na wale wa Ukraine ambao walikuwa wanazuru eneo hilo wakiwa miongoni mwa ujumbe unaoshirikishwa na shirika la usalama la muungano wa Ulaya.
Kundi hilo linashirikisha wachunguzi wa kijeshi wa Ujerumani pamoja na wawakilishi wa Denmark,Poland,Sweden na jamhuri ya Czech.
Kiongozi mmoja anayeunga mkono Urusi amesema kuwa wachunguzi hao wamezuiliwa kwa kuwa mpelelezi mmoja wa serikali ya Ukraine alikuwa miongoni mwao.
Ujerumani imesema kuwa itatumia njia zote za kidiplomasia ili kuhakikisha kuwa wamewachiliwa huru.
Na huku hali ya wasiwasi ikipanda,Marekani imesema kuwa imegundua kwamba ndege za kijeshi za Urusi zimekuwa zikiingia katika anga ya Ukraine katika kipindi cha masaa 24 yaliopita.