Saturday 12 April 2014

Ndege ya Airway nanusurika kuuwa abiria 56

Ndege ya Shirika la Ndege la Kenya(Kenya Airways), Ndege ya shirika hilo siyo hii pichani yenye namba 5Y-FFT aina ya Embrarer 190 yenye uwezo wa kubeba abiria 90 imepata ajali jana mchana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam(JNIA) ikiwa na abiria 49 na wafanyakazi saba.

Dar es Salaam. Watu 56 wamenusurika baada ya ndege ya Shirika la Ndege la Kenya(Kenya Airways) waliyokuwa wakisafiria kupata ajali katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam(JNIA) jana ilipokuwa ikitua.

Kamanda wa Polisi Viwanja vya Ndege, Kamiishna Khamis Selemani alithibitisha kutokea kwa ajali akieleza kuwa ilisababishwa na rubani kupoteza mwelekeo na kushindwa kuona njia sahihi kutokana na mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha uwanjani hapo.

Ndege hiyo yenye namba 5Y-FFT aina ya Embrarer 190 yenye uwezo wa kubeba abiria 90 ilipata ajali hiyo mchana ikiwa na abiria 49 na wafanyakazi saba.

“Tulipata taarifa za kuanguka kwa ndege hiyo majira ya saa 8:26 mchana. Ndege hiyo imepata hitilafu katika injini yake ya upande wa kulia ambayo imebonyea pamoja na kupasuka ubavuni,” alisema Selemani.

Kamanda huyo aliongeza kuwa pia tairi la mbele la ndege hiyo limepasuka baada ya kujigonga, lakini hakuna kifo kilichotokea wala majeruhi waliohitaji matibabu.

“Haitoweza kuruka kabla ya marekebisho kwani hewa itaingia ndani jambo ambalo haliruhusiwi kwa usafiri wa angani katika viwango vya kimataifa,” aliongeza Seleman.

Katika hatua nyingine, ndege ya Shirika la Ndege la Emirates, ilishindwa kutua kwenye uwanja huo jana kutokana na mvua hizo, hivyo kulazimika kwenda kutua Uwanja wa Ndege wa Mombasa nchini Kenya.

No comments: