Inashangaza: Petr Cech akitembea na Nathan Ake (katikati) na Marco van Ginkel kuelekea katika mazoezi.
Cech aliteguka beka katika mchezo
wa kwanza uliomalizika kwa suluhu ya bila kufungana Vicente Calderon na
Mourinho alithibitisha wiki iliyopita kuwa kipa huyo anahitaji upasuaji
ili kurudisha bega katika hali yake.
Nyota wa samba: Willian, David Luiz, Ramires na Oscar wakielekea katika uwanja wa Coham tayari kwa mazoezi.
Alipoulizwa kama yuko imara kwa mechi ya kesho, alitabasamu na kusema “Ndiyo”, lakini alienda zake na kujiunga na wenzake.
Cech alionekana akifanya mazoezi
mepesi leo hii, na makipa wenzake Mark Schwarzer, Henrique Hilario na
Mitchell Beeney walipoanza mazoezi na kocha wa makipa, Christophe
Lollichon, Cech alikaa pembeni.
Mbali na Cech, wachezaji wengine waliokuwa majeruhi, Samuel Eto`o, nahodha, John Terry, na Eden Hazard nao wamefanya mazoezi leo hii kujiandaa na kipute cha kesho.
Mbali na Cech, wachezaji wengine waliokuwa majeruhi, Samuel Eto`o, nahodha, John Terry, na Eden Hazard nao wamefanya mazoezi leo hii kujiandaa na kipute cha kesho.
No comments:
Post a Comment