Thursday 17 April 2014

Waasi wa Sudani Kusini wauteka mji wa Bentiu

Rais wa Sudani Kusini, Salva Kiir akiwa katika ikulu mjini Juba.
Rais wa Sudani Kusini, Salva Kiir akiwa katika ikulu mjini Juba.

Jeshi la Sudan Kusini limekiri hapo jana kupoteza mji wenye utajiri wa mafuta wa Bentiu kwa waasi wanaomuunga mkono Riek Machar ambaye ameapa kuipindua serikali ya rais Salva Kiir.

Mji wa Bentiu ni eneo muhimu la mji wenye wa mafuta wa jimbo la Unity ambalo serikali ilikuwa ikilitegemea kama sehemu ya kupanga mashambulizi yao dhidi ya waasi ambao wanaonekana kupata nguvu upya wakilenga kuvamia mji wa Juba katika siku za usoni.

Le vice-président du gouvernement autonome, Riek Machar, exclut toute possibilité d'attentat.
Le vice-président du gouvernement autonome, Riek Machar, exclut toute possibilité d'attentat.
Makamu wa zamani wa rais wa Sudani Kusini, Riek Machar, akiongea na wanahabari mara tu ya waasi wake kuuteka mji wa Bentiu.
(Photo : AFP)
Akizungumza na wanahabari kwenye mji wa Bentiu saa chache baada ya wapiganaji wake kuuchukua na kutembelea mtambo wa kuzalisha mafuta, Riek Machar anasema kuwa sasa wanajipanga kuuondoa madarakani utawala wa kiimla wa rais Kiir.
Katika hatua nyingine, msemaji wa jeshi la Sudan Kusini, Philip Aguer amekiri kuwa sehemu ya wanajeshi wake walijiunga na waasi wa Riek Machar na kuongeza kuwa tayari wamewabaini na wanachokifanya sasa ni kujipanga kuurejesha tena kwenye himaya yao mji wa Bentiu.
“Kilichotokea ni kwamba waasi wameingia mjini kutokea mipakani wakisaidiwa na wanamgambo wapiganaji wa jamii ya kiarabu ya Miseria na wanagambo wa Janjawid. Tayari jeshi limeanza kujipenyeza mjini humo na hivi punde tutawafurusha mjini humo. Kuhusiana na askari waliojiunga na uasi wa Rieck Machar tunawafahamu na tutatangaza majina yao na kinachoendelea kwa muda mwafaka” amesema Aguer.
Wakati wanajeshi wa Serikali wakiendelea kukabiliana na waasi, maelfu ya raia wa nchi hiyo wanaendelea kuikimbia nchi yao kwenda kupata hifadhi kwenye nchi jirani huku Umoja wa Mataifa ukionya kuhusu hali mbaya ya kibinadamu kwenye makambi ya wakimbizi wa Sudan Kusini.

No comments: