Monday, 31 March 2014

Waandishi wa Al jazeera wanyimwa dhamana

waandishi walionyimwa dhamana

Kesi dhidi ya wandishi watatu wa shirika la habari la Al Jazeera nchini Misiri imeanza kusikilizwa tena leo nchini Misri .

Watatu hao wanatuhumiwa kwa madai ya kusambaza habari za uongo na kusaidia kundi la kigaidi la Muslim brotherhood lililopigwa marufuku.

Waandishi hao ni pamoja na aliyekuwa mwandishi wa habari wa BBC, Peter Greste na Mohamed Fahmya ambaye alikuwa afisa mkuu wa Al Jazeera mjini Cairo.

Watatu hao waliruhusiwa kuongea na jaji ana kwa ana kwa mara ya kwanza tangu wazuiliwe.

Greste alimwambia jaji kuwa hawezi hata kutamka neno moja la kiarabu na madai dhidi yake kuwa alisaidia kundi la Brotherhood ni ya kushangaza sana.

Wamekuwa kizuizini tangu Disemba mwaka jana na mahakama kwa mara nyingine imewanyima dhamana.

Leo mahakama ilikuwa ichunguze ushahidi wa video, lakini hilo halikufanyika kwa sababu vifaa hivyo havikupatikana

Kesi yao imeahirishwa hadi tarehe 10 Aprili.

Kilimanjaro kuimarisha ulinzi katika nyumba za ibaada

KUTOKANA na tishio la vitendo vya kigaidi katika maeneo ya nyumba za ibada, Jeshi la Polisi Mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro, limeanza mkakati wa kuweka ulinzi katika nyumba za ibada wakitumia dhana ya Polisi Jamii.
Akizungumzia mkakati huo kwa waumini wa Kanisa Katoliki, Parokia ya Kristu Mfalme lililoko Moshi Mjini, mkoani humo, Mkuu wa Polisi Wilaya ya Moshi, (OCD), Deusdedit Kasindo, alisema lengo ni kujihami na matukio hayo kabla hayajatokea.
"Wenzetu katika nchi jirani, magaidi wamevamia Kanisa, kuua watu na wengine kujeruhiwa...nasi tumeona ni bora tukaanza kuchukua hatua kupitia dhana ya Polisi Jamii hivyo tunaomba ushirikiano wetu," alisema.
Aliongeza kuwa, kwa kuanzia jeshi hilo limetoa wito katika madhehebu mbalimbali wilayani humo kuanzisha vikundi vya ulinzi na usalama pamoja na kuviimarisha vilivyopo viweze kushirikiana na polisi kukabiliana na hali hiyo.
"Kumekuwa na vikundi vinavyojihusisha na wizi wa baiskeli, pikipiki na baadhi ya vitu ndani ya magari kwenye nyumba za ibada, lakini kwa hili la uvamizi ambao umeanza kushamiri hatuna budi kujiimarisha zaidi," alisema.
OCD Kasindo alisisitiza kuwa, tayari jeshi hilo limezunguka katika Makanisa na Misikiti mbalimbali mjini humo ili kutoa wito huo ambapo jeshi lipo tayari kutoa mafunzo yanayohusiana na ulinzi kama vikundi hivyo vitaundwa.
Alisema wameamua kusisitiza matumizi ya Polisi Jamii kutokana na jeshi hilo kuwa na askari wachache ukilinganisha na idadi ya wananchi wanaohitaji huduma za polisi maeneo mbalimbali.
"Matokeo ya sensa yaliyotoka hivi karibuni, askari mmoja ana jukumu la kulinda raia kati ya 1,300 na 1,500, hivyo ni muhimu raia wenyewe wakaanza kujichunga kwa asilimia 90 na asilimia 10 iliyobaki, usalama wao utasimamiwa na polisi," alisema.
Kwa upande wake, Paroko wa Parokia hiyo, Padri Crispin Jumanne, alilipongeza jeshi hilo kwa uamuzi huo uliokuja wakati mwafaka.
"Mkakati huu utasaidia kuwaondoa hofu waumini ambao baadhi yao walianza kuogopa na kushindwa kuhudhuria ibada...kwa niabaya Baba Askofu Isaack Amani, tunaahidi kutoa ushirikiano ambao tutauanza mara moja," alisema.
Alitoa wito kwa waumini wa kanisa hilo, kuliunga mkono jeshi hilo kwa kuwapa ushirikiano wao ili waweze kufanikisha azma ya kuhakikisha waumini wanafanya ibada kwa amani bila hofu.

Mtoto azaliwa na vichwa viwili


MADAKTARI wa Hospitali ya Holy Family (HFH) mjini hapa wanapigania maisha ya mtoto aliyezaliwa Septemba 25, mwaka huu akiwa na sura mbili na uzito wa kilo 3.2.
Kwa mujibu wa taarifa za
hospitalini hapo, mtoto huyo mara baada ya kuzaliwa amekutwa ana tatizo la kupumua hivyo kumlisha kupitia mdomo, mpashaji aliliambia Gazeti la The Express Tribune.

Mtoto huyo ni wa tatu kuzaliwa kutoka kwa Bi. Shahida Perveen na mumewe Khalil Ahmed. Msajili wa hospitali hiyo, Dk. Qaisar Aziz ameliambia The Express Tribune kwamba mtoto huyo amehamishiwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (Intensive Care Unit) katika wodi ya watoto na atakuwa katika uangalizi wao.

Hata hivyo, madaktari wameonesha kukata tamaa na kusema kuna uwezekano mdogo kwa mtoto huyo kuendelea kuishi na kukua. “Kumlisha kwa kutumia mdomo haiwezekani kwa sasa, tunamlisha kwa kutumia mipira maalum (Naso-gastric tube). Sura hizi mbili zinafanana,” alisema Dk Qaisar.

Mtoto huyo ana macho manne, pua mbili, midomo miwili na masikio manne, kwa maana kwamba ana sura mbili.
Habari zinasema mama wa mtoto huyo alipopimwa na mashine maalum, (Ultrasound) alionekana hana matatizo yoyote na alikuwa na afya njema.

Baadhi ya wananchi waliotoa maoni yao kufuatia tukio hilo, walisema dunia imetikisika kufuatia kuzaliwa kwa mtoto huyo wa ajabu na kuongeza kuwa hiyo ni ishara kwamba imefika mwisho.

Sunday, 30 March 2014

MBWANA SAMATA AIPELEKA MAZEMBE NANE BORA TP Mazembe


KLABU ya TP Mazembe imefuzu kutinga Hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Sewe Sport ya Ivory Coast 1-0 jana jioni Uwanja wa Kamalondo mjini Lubumbashi.

Mazembe imesonga mbele kwa faida ya bao la ugenini baada ya sare ya jumla ya 2-2 kufuatia awali kufungwa 2-1 mjini Abidjan Jumapili iliyopita.

Alikuwa ni mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta aliyefunga bao hilo pekee dakika za mwishoni kipindi cha pili na kuirudisha timu hiyo ya DRC kwenye hatua ya makundi tangu mwaka 2012 waliposhiriki mara ya mwisho.

Samatta pia ndiye aliyefunga bao la Mazembe Abidjan ikifungwa 2-1 na maana yake yeye ndiye ameibeba kwa mabega yake timu hiyo hadi Nane Bora na sasa itasubiri kujua wapinzani wake watatu katika droo itakayopangwa Aprili 29 mjini Cairo.

SNURA napunguza mauno

MWANADADA anayetamba katika tasnia ya muziki wa mduara pia katika uigizaji wa filamu, Snura Mushi ‘Snura’ amesema ameamua kupunguza kukatika viuno katika video za nyimbo zake kutokana na kukosolewa na hata kutolewa kwenye baadhi ya vipengele vya tuzo za Kilimanjaro Music Awards (KTMA).

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Snura alisema hata kabla Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) hawajapiga stop ushiriki wa nyimbo zake kwenye kinyang’anyiro hicho, alikuwa ameshabadilika kwa kuwa tayari video yake ya ‘Nimevurugwa’ ilikuwa imefungiwa.

Alisema yeye ameshabadilika kabla hata hatujafika huko kwenye Kili kwa sababu ‘Nimevurugwa’ ilifungiwa muda kidogo kabla ya Kili kuikosoa na kwamba wimbo wake wa ‘Ushaharibu’ alikuwa ameshafanya video ikitoka watu watajua ni jinsi gani ameweza kubadilika.

Ameeleza kuwa si kwamba kwenye ‘Ushaharibu’ hakutakuwa tena na uchezaji ule wa kukata viuno bali atapunguza kidogo, akitofautisha na video nyingine zilizotangulia.

“Kweli kwenye video si kwamba hakuna kabisa kiuno ila nimepunguza, nimeacha viuno ambavyo nina uhakika kwamba siwezi kufungiwa jamani, sijakatika kama kwenye ‘Nimevurugwa’, wakati nafanya wimbo wa ‘Nimevurugwa’ sikuhisi kama ninaweza nikafungiwa kiukweli, laiti kama ningejua nisingeweza kufanya vile, mimi nilichukulia kama ni ubunifu na utundu wangu ndiyo maana nikafanya vile,” alisema Snura.

Hata hivyo, amedai kuwa kuna mashabiki wake ambao wangependa kuona anacheza kama alivyokuwa akicheza zamani, hivyo ataendeleza mchezo huo kwenye shoo zake atazofanya kwenye kumbi mbalimbali.

CHELSEA ya lala MAN U yaona mwangaza

Matumaini ya kuchukua ubingwa wa ligi kuu soka nchini England kwa Chelsea yamedidimia baada ya kujikuta wakipoteza mchezo wao dhidi ya Crystal Palace kwenye uwanja wa Selhurst Park.

Crystal Palace maarufu kama The Eagles wameishangaza Chelsea kwa kipigo cha bao moja, bao ambalo nahodha wa Chelsea John Terry alijifunga mwenyewe baada ya klosi ya Joel Ward.

Shukhrani ziende kwa mlinda mlango wa Palace Julian Sperioni ambaye aliokoa michomo miwili ya Edin Hazard na nafasi ya wazi ya John Terry ambaye alikuwa asawazishe.

Cameron Jerome alimanusra afanye matokeo yawe 2-0 baada ya shuti lake kugonga mwamba na kuokolewa.

Ushindi wa Palace ni wa kwanza katika mechi sita za ligi kuu na zinakifanya kikosi cha kocha wake Tony Pulis kusogea kwa pointi tano kutoka katika timu tatu zilizo katika hatari ya kushuka daraja.

Huku chelsea ilkilala 1 0 Manchester United imeona mwanga kwa kuichapa Aston Villa 4 1
Wayne Rooney akifunga bao la kwanza la United ikicheza na Aston Villa.
Kwingineko Manchester United ilishinda katika mechi yake ya mapema kwa mabao 4-1 dhidi ya Aston Villa.

Wayne Rooney alifunga mabao mawili huku Juan Mata na Javier Hernandez wakifunga kuhutimisha ushindi mkubwa wa wiki kwa David Moyes ambaye leo alikumbana na bango nje ya uwanja wa Old Traford kumtaka aondoke.

Manchester United watapambana na Bayern Munich katika mchezo wa robo fainali michuano ya klabu bingwa barani Ulaya hapo siku ya jumanne.

Southampton wakaiadhibu Newcastle kwa mabao manne kwa sinia kwenye uwanja wa St.Marys.

The Saints ambayo ina washambuliaji muhimu wanaotegemewa na kocha wa timu ya taifa ya England,leo kwa mara nyingine walionyesha matumaini ya waingereza kuwa na wachezaji wazuri kwenye safu ya ushambualiaji kwani magoli yote yalifungwa na washambuliaji wa England Jay Rodriguez, Rickie Lambert na Adam Lallana.

Nayo Stoke City waliichapa Hull City 1-0.

Swansea wakaiadhibu Norwich kwa mabao 3-0 huku majirani zao Cardiff City wao wakaponea kwa sare ya 3-3 ugenini walipokuwa wageni wa West Brom kwenye uwanja wa The Hawthorns

Kura ya maoni yailigawa bunge la katiba


Wajumbe wa Kamati ya Maridhiano jana walinusuru Bunge Maalumu la Katiba kuvunjika, baada ya kukubaliana kutumika kwa utaratibu wa upigaji kura wa wazi na siri kama ilivyopendekezwa na Kamati ya Kanuni na Haki za Bunge.

Wajumbe hao walitangaza uamuzi huo bungeni kutokana na makubaliano yaliyofikiwa katika kamati ndogo ya maridhiano iliyofanyika jana asubuhi baada ya kushindwa kuafikiana katika kikao cha awali kilichofanyika juzi kuanzia saa 3:00 usiku hadi usiku wa manane ili kunusuru kukwama kwa Bunge hilo.

Kabla ya uamuzi huo, Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta alisema juzi usiku walikutana hadi usiku wa manane baada ya hapo, walikabidhi kamati ndogo yenye mchanganyiko wa wajumbe kutoka Kamati ya Kanuni na Kamati ya Maridhiano.

“Baada ya kukamilisha kazi, wajumbe wa kamati ndogo watatoa taarifa hapa ambao ni John Mnyika, Profesa Ibrahimu Lipumba, Vual Ali Vual na Askofu Donald Mtetemela,”alisema Sitta.

Akitoa taarifa ya maridhiano hayo, kwa niaba Freeman Mbowe, Mjumbe John Mnyika alisema, alianza kwa kunukuu kitabu kilichoandikwa na Mwalimu Nyerere, mwaka 1962 chenye ujumbe mahususi kwa Chama cha TANU akisema ujumbe huo kwa sasa ni sahihi kwa watu wengi na taasisi ikiwamo CCM.
https://draft.blogger.com/blogger.g?blogID=2790906090840960650#editor/target=post;postID=7370141469061707857
Mnyika pia alisema Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) hawana nia yoyote ya kuvuruga mchakato wa katiba kama ambavyo imeelezwa katika siku za karibuni na viongozi, kwani wazo la kutaka Katiba Mpya imekuwa ni kilio chao cha muda mrefu.

Naye Profesa Lipumba alisema suala ambalo tumekuwa tukisimamia kwa muda mrefu suala ambalo lina utata, kati ambao wanapenda kura za uwazi na wale wa siri.

Alisema: “Tuliletewa mchanganyiko wa uwazi na siri, lakini maana yake ni kura ya uwazi, wenzetu wamekuwa na msimamo mkali hata hili la kufanya uamuzi ilikuwa tufanye kwa siri, lakini hata hivyo hawakukubali.”

“Tulifanya uamuzi ili tusonge mbele, basi tulipendekeza upigaji kura wa kuamua tupige kura kwa mfumo wa siri, lakini pia wenzetu walikataa,”alisema Profesa Lipumba.

Alisema kwa kuzingatia kutokwama kwa zoezi la kuanza kujadili rasimu, wameamua kukubali kutokubaliana.

“Ili kusonga mbele tunahitaji kusonga mbele tuanze kujadili Katiba, natoa wito kwa wenzangu wa chama tawala kwa kuwa mpo wengi mnadhamana kubwa, ni vyema mkawa na utaratibu wa kuwasikiliza wachache,” alisema.

Mjumbe Vuai Ali Vuai alisema, wamefikia maridhiano hayo, ili kuwezesha kuendelea na mchakato wa katiba mpya kwani kila upande uliendelea kutetea msimamo wake hata katika kikao cha maridhiano.

WAnaume wote wa korea lazma wanyoe viduku kama Raisi wao

Pyongyang. Wanaume Korea Kaskazini wanakabiliwa na mtihani mpya katika taifa lao; wa kunyoa nywele kwa mtindo ulioamuliwa na rais wao.

Watake, wasitake kuanzia sasa kila mwanamume atalazimika kunyoa nywele zake kwa mtindo anaoupenda Rais Kim Jong- un.

Kiongozi huyo kijana, aliyerithi wadhifa huo baada ya kifo cha baba yake, hana mzaha hasa kutokana na nia yake ya kujenga mfumo mpya wa utawala ambao matakwa yake tu ndiyo ya kufuatwa.

Ni wiki mbili sasa tangu serikali ya nchi hiyo kutoa agizo linalowataka wanaume kunyoa kama rais wao, huku wanawake nao wakielekezwa kutengeneza nywele zao kwa aina 18 tofauti na si zaidi ya hapo.

Hilo ni moja ya maagizo yenye utata kuwahi kutolewa chini ya utawala wake, ambapo amekuwa akifanya jitihada za kujijengea mizizi, ikiwamo kuwaondoa na kuwaadhibu wale waliokuwa katika utawala wa baba yake wanaoonekana kutokubaliana na aina yake ya uongozi.

Mapokezi tofauti

Hata hivyo, japokuwa staili yake ya unyoaji wa nywele imekuwa sehemu ya utambulisho wake na inafahamika na kila mmoja, agizo hilo limekuwa na mapokeo tofauti.

“Namna ya unyoaji wake wa nywele inavutia, kwa wanaoipenda. Lakini haiwezi kumpendeza kila mmoja atakayeiiga kwa kuwa maumbo ya vichwa yako tofauti kutokana na maumbile,” alieleza raia mmoja akinukuliwa na Radio Free Asia ya Korea Kusini.

Raia mwingine wa Korea Kaskazini ambaye anaishi nchini China, alieleza kwamba aina hiyo ya unyoaji nywele kwa raia waliopo China inaweza kuonekana kama uhuni.

“Hadi katikati ya miaka ya 2000 tulikuwa tukiitaja aina hiyo ya unyoaji wa nywele kama ‘mtindo wa wahuni wa China,” alisema raia huyu alipohojiwa na gazeti la Korea Times.

Hadi sasa, wanaume wa Korea Kaskazini wana aina 10 za unyoaji zilizowahi kuamriwa na Serikali yao.

Wanaume wamekuwa wakitakiwa kuwa na nywele fupi za wastani zenye urefu wa inchi mbili na wametakiwa pia kuzipunguza kila baada ya siku 15.
Kwa wazee, kwa kiasi fulani wamepewa ahueni kwa kuwa wameruhusiwa kuwa na nywele zenye urefu wa angalau inchi tatu na wanaweza kwenda kwa kinyozi mara mojamoja kwa ajili ya kuzipunguza.

Kwa wanawake, wana uhuru zaidi kwa kuwa wana ruhusa ya mitindo 18 ya nywele iliyoamriwa na Serikali ya nchi hiyo.

Kituo cha televisheni ya Serikali ya Korea Kaskazini ambacho kimekuwa kikirusha matangazo yake nchini humo pekee, kimekuwa kikitumika kutoa maelekezo na kueneza kampeni za kutekeleza unyoaji wa nywele katika mtindo huo wanaouita wa Kisoshalisti.

Siyo agizo geni

Mwaka 2005, televisheni ya serikali ilianzisha kampeni maalumu iliyokuwa imelenga kudhibiti aina na namna ya unyoaji kwa wanaume.

Vyombo vya habari vya serikali vilikwenda mbali zaidi kwa kutaka udhibiti zaidi sio tu katika namna ya unyoaji wa nywele, bali pia katika aina na namna ya uvaaji wa nguo.

Aina hiyo ya unyoaji wa Kim Jong –un ilikuwa maarufu katika miaka ya tisini. Baadhi ya watu maarufu hasa wasanii waliitumia kama sehemu ya utambulisho.

Hata hivyo, kwa mujibu wa taarifa, watu wengi nchini Korea Kaskazini hawakuipenda aina hiyo.

Friday, 28 March 2014

Rihana amchapa mtu kibao baada ya kumshika makalio

Hii ni Fundisho kwa Wanaume woote wanaopenda kuwasumbua wanawake waliona mvuto na Majumbile ya kuvutia, Mtoto wa Ki Barbdadian Mrembo Rihana ameweza kuwawakilisha wanawake wasiopenda udhalilishaji wa namna hii kwa Kumtandika Makofi Mwanaume aliyejitokeza kumshika Makalio Kwa nyuma.

Babu Etoo aipa adhabu Man U

Samuel Eto'o akishangilia baada ya kufunga goli.
LONDON, ENGLAND

MANCHESTER United basi tena. Ndicho unachoweza kusema baada ya mabingwa hao wa Ligi Kuu England kugeuzwa vibonde kwenye ligi hiyo kufuatia kichapo cha mabao 3-1 kutoka kwa Chelsea jana Jumapili kwenye Uwanja wa Stamford Bridge.

Samwel Eto’o alifunga ‘Hat-Trick’ kuifanya Chelsea kuzidi kuweka hai matumaini yao ya kushindania ubingwa wa ligi hiyo msimu huu baada ya kufikisha pointi 49, pointi mbili nyuma ya vinara Arsenal.

Eto’o alifunga katika 17, 45 na 49. Manchester United iliyomaliza ikiwa pungufu kufuatia kadi nyekundu ya Nemanja Vidic ilipata bao lake kupitia kwa Javier Hernandez kwenye dakika 78.

Mchezo mwingine wa ligi hiyo, Tottenham Hotspur waliichapa Swansea City mabao 3-1, shukrani kwa mabao mawili ya straika Emmanuel Adebayor na moja la kujifunga la Chico. Bao la Swansea lilifungwa na Wilfried Bony.

‘Rais akistaafu afutiwe kinga’

Rais wa nchi awe tu na kinga anapokuwa madarakani, akiondoka awajibike kwa matendo yake.

Wakati Bunge la Katiba likiwa bado halijaanza kujadili Rasimu ya Katiba, taasisi moja ya viongozi wa dini imetoa maoni mapya ikitaka Rais wa nchi awe tu na kinga anapokuwa madarakani, akiondoka awajibike kwa matendo yake.

Mapendekezo hayo yalitolewa Dar es Salaam jana na Baraza la Wadhamini la Taasisi ya Viongozi wa Dini Tanzania (IRCPT), lilipokutana kwa ajili ya kutafakari kwa pamoja juu ya mchakato wa Katiba Mpya.

Mkutano wa Baraza hilo linalojumuisha Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Titus Mdoe, Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaj Musa Salum na Padri John Solomon, uliongozwa na kaulimbiu ya ‘Katiba Moja Kwa Watanzania Wote, Pamoja Tutafika’.

Mwenyekiti wa IRCPT, Jaji Mstaafu Raymond Mwaikasu alisema tafakari inahitajika kuhusu kinga ya Rais na kwamba wao wanapendekeza awe nayo anapokuwa madarakani, lakini kinga hiyo iondolewe anapoachia madaraka, ili awajibishwe pale alipokosea.

Jaji Mwaikasu alisema pamoja na kwamba waliwasilisha maoni kwa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, hatua ya sasa inawalenga watu wenye lengo la kuingia Ikulu wakiwa na mawazo ya kujinufaisha wao, ndugu, jamaa na marafiki zao badala ya kuwatumikia wananchi.

“Hili linapaswa kutazamwa kwenye Katiba yetu mpya na sisi hatutakuwa wa kwanza kufanya hivyo, ila itasaidia kuwafanya viongozi kufuata maadili na iwapo itatokea Rais kuvunja Katiba, apelekwe mahakamani na akikutwa na hatia, awajibike hata kwa kujiuzulu,” alisema Jaji Mwaikasu. Naye Sheikh Salum alisema mali zote ni miliki ya Mungu, hivyo zinapaswa kugawanywa kwa usawa na ikitokea mtu akajimilikisha ni jambo lisilokubalika, hivyo ziwepo sheria za kuwabana viongozi wa aina hiyo.

Askofu Mdoe alisema Rasimu ya Katiba ni nzuri ingawa hakuna kitu kinachokamilika kwa asilimia 100, hivyo mazuri yaboreshwe, upungufu usahihishwe na yaliyokosekana yapatiwe fursa.

Alisema malumbano yanayoendelea kwenye Bunge la Katiba hayana tija kwani yana mwelekeo wa masilahi ya kisiasa badala ya masilahi ya umma.

“Wamebadilisha hali waliyotakiwa kuwa nayo, wanarudi katika makundi hasa ya kisiasa na mijadala kuwa ya kichama zaidi, wakifika bungeni wawe wazalendo wajadili na kuacha ushabiki,” alisema Askofu Mdoe.

Muundo wa Muungano

Kuhusu mjadala wa serikali mbili au tatu, Jaji Mwaikasu alisema hauna tija isipokuwa jambo muhimu ni kujenga msingi imara wa kuheshimiwa kwa Katiba itakayopitishwa. “Tunaambiwa Katiba imevunjwa, tunafanya nini? muhimu ni kuangalia viongozi wanaohusika wanadhibitiwa vipi, vinginevyo itakuwa ni bure,” alisema.

Alibainisha kuwa tatizo Bunge la Jamhuri ya Muungano limelala na walioteuliwa kutetea wanatetea mikate yao, hivyo akapendekeza kuwapo haja ya wananchi nao kupewa meno ya kuhakikisha Katiba inalindwa, ili pale itakapothibitika Rais amevunja Katiba wachukue hatua
Naye Katibu wa Kamati ya Amani ya Viongozi wa Dini Mkoa wa Dar es Salaam, Padri Solomon alisema alisema alitarajia Rais Jakaya Kikwete angeenda kufungua Bunge bila ya kutoa mawazo yake wala ya chama chake.

Padri Solomon alisema; “Badala ya kusimama kufungua tu, bahati mbaya alitoa hisia zake, sijui za chama, zimeleta mkanganyiko.”

Utoaji mimba

Wakati huohuo, Jaji Mwaikasu alieleza kuwa Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa bungeni wiki iliyopita, haielezi haki za watoto na mtoto maana yake nini.

Alisema sheria ya 2009 inaongelea kulinda uhai wa mtoto lakini inatambua mtoto kuwa ni wa wiki 28 hadi chini ya miaka 18, hivyo kutokana na hilo masuala ya utoaji mimba hayazuiliwi.

Alisema kwa viongozi wa dini, mtoto huanzia pale mimba yake inapotungwa na kwamba anapaswa kupewa ulinzi wa kisheria, hivyo kushauri suala hilo liwekwe wazi kwenye Katiba.

Siku 3 kuomboleza waliozama Ziwa Albert

Wakimbizi wa DRC walikuwa wanatoka kambini Uganda kuelekea nyumbani DRC

Maafisa wa utawala katika Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo wametangaza siku tatu kuomboleza wakimbizi waliofariki katika ajali ya boti katika ziwa Albert siku ya Jumamosi.

Boti hiyo, ilikuwa inawasafirisha wakimbizi wa DRC kutoka nchini Uganda wakirejea nchini mwao.

Inaarifiwa boti hiyo ilikuwa imebeba abiria zaidi ya inavyoweza kumudu na maafisa wanasema kuwa zaidi ya watu miambili hamsini waliOkuwa wameabiri boti hiyo walizama.

Serikali ya Uganda ilisema kuwa iliweza kupata maiti 107 ikiwemo watoto 57 baada ya bnoti hiyo kuzama. Wote walikuwa wanatarajiwa kufika salama nyumbani DRC.

Walikuwa wanaishi katika kambi za wakimbizi nchini Uganda na inaarifiwa watu 300 walikuwa wameabiri boti hiyo illipozama.

Barca na Uhispania kumkosa Valdez

Mlinda mlango wa Barcelona na timu ya taifa ya uhispania, Victor Valdes hatashiriki fainali za Kombe la dunia baada ya kupata jeraha kwenye mshipa wa mguu.

Victor mwenye umri wa miaka 32 aliondolewa uwanjani kwa machela wakati wa mechi kati ya Barcelona na Celta Vigo, ambapo Barcelona iliinyuka timu hiyo magoli 3-0 siku ya jumatano.
Kipa wa Barcelona Victor Valdez ajeruhiwa

Klabu ya Barcelona imethibitisha kuwa mchezaji huyo amepata jeraha na kuwa atahitaji kufanyiwa upasuaji.

Inaelezwa kuwa kutokana na hali hii huenda Valdes ukawa ndio mchezo wake wa mwisho akiwa na Barcelona na ataondoka kwenye klabu hiyo mkataba wake utakapomalizika kipindi cha majira ya joto.

Kocha wa Barcelona, Gerardo Martino amesema hakuna mpango wa kumtafuta mlinda mlango mwingine na kuwa atamaliza msimu huu na kikosi alichonacho.

Victor alipata jeraha dakika ya 22 katika dimba hilo lililokuwa Nou Camp, muda mfupi baada ya kupangua mpira wa adhabu wa Celta Vigo.

Valdes, ambaye ambaye ameichezea Barcelona kwa miaka 12, alikuwa akitegemewa kupambana na Iker Casillas kupata nafasi ya kuidakia timu ya taifa ya Uhispania katika michuano ya kombe la dunia

nchini Brazil mwaka huu lakini fursa hiyo imeonekana kuwa finyu kwake.

Valdes amepata jeraha ikiwa ni mara ya pili katika msimu huu mara ya kwanza alipata jeraha kwenye kifundo cha mguu wakati Uhispania ilipocheza mechi ya kirafiki na Afrika kusini mwezi Novemba

mwaka jana na kufungwa 1-0.

Jeraha hilo lilimfanya Valdes kukosa mechi nane ya Barcelona.

Watu Nne waambukizwa Ebola Conakry

Watu wanne wamethibitishwa kuugua ugonjwa hatari wa Ebola katika mji mkuu wa Guinea,Conakry.
Ni mara ya kwanza kwa Ebola kuzuka Conakry
Wataalamu wa afya wamesema kuwa wamewatenga wanne hao katika wadi ya hospitali moja mjini humo. Hii ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Ebola kuzuka mjini humo.

Tangu kuzuka kwa homa hiyo hatari mwezi uliopita, zaidi ya watu sitini wamefariki nchini humo.

Ripoti hizo zinajiri siku moja tu baada ya wataalamu wa afya nchini Guinea kusema kuwa homa hiyo hatari ilikuwa imedhibitiwa katika mkoa wa kusini.

Hata hivyo, kuenea kwa Ebola mjini Conakry kunadhirisha changamoto katika vita dhidi ya ugonjwa huo kutokana watu kusafiri kutoka eneo moja hadi lingine .

Nchi jirani zimeimarisha huduma zao za afya hasa katika maeneo ya mipakani.

Kura ya maoni kuhusu Crimea inautata

Baraza la umoja wa mataifa limetangaza matokeo ya azimio ambalo limeharamisha hatua ya Urusi kuandaa kura ya maoni kuhusu eneo la Crimea na kuunga mkono uhuru wa Ukraine.
Umoja wa mataifa unaunga mkono uhuru wa Ukraine

Nchi 100 zimepiga kura kuunga mkono Azimio hilo huku nchi 11 zikipinga.

Azimio hilo lililowasilishwa mbele ya baraza la Umoja wa Mataifa na Ukraine linanuia kuisisitizia Urusi kwamba inakabiliwa na tishio la kuendelea kutengwa zaidi kidiplomasia na jamii ya kimataifa.

Limehimiza haki ya taifa la Ukraine na kuitaja kura ya maoni iliyofanyika Crimea hivi karibuni kama isiyohalali.

Akizungumza baada ya azimio hilo kupitishwa,balozi wa Muungano wa Ulaya katika umoja wa mataifa , Thomas Mayr-Harting, amesema sio haki kutumia nguvu kubadili mipaka ya nchi.

Naye waziri wa mambo ya nje wa Ukraine , Andriy Deshchytsia, ameelezelea kudhirishwa na azimio hilo la Umoja wa Mataifa.

Akizungumza kabla ya azimio hilo kupitishwa balozi wa Urusi katika Umoja wa mataifa Vitaly Churkin aliomba baraza la Umoja wa mataifa kuheshimu matokeo ya kura ya maoni iliyofanyika Crimea ambapo raia wengi walipendelea kujiunga na Urusi.

Ukraine inatarajia kuwa kupitishwa kwa azimio hilo kutaipa shinikizo zaidi Urusi na kuionya dhidi ya kuendelea kuvamia maeneo yake.

Wednesday, 26 March 2014

Wajioba Ampa majibu Jk

ILIYOKUWA Tume ya Mabadiliko ya Katiba, chini ya Jaji Joseph Warioba, imetoa ufafanuzi katika baadhi ya maeneo ya Rasimu ya Katiba yaliyokosolewa na Rais Jakaya Kikwete katika hotuba yake ya uzinduzi wa Bunge Maalumu la Katiba wiki iliyopita.

Taarifa ya Tume hiyo kwa umma wa Watanzania, iliyosambazwa jana kwenye vyombo vya habari, ilisema hatua hiyo ya kutoa ufafanuzi katika baadhi ya maeneo imetokana na kile kinachoelezwa na Tume hiyo kuwa shauku kubwa ya wananchi kutaka ufafanuzi wa mambo mbalimbali kuhusu Rasimu ya Katiba baada ya hotuba ya Rais Kikwete.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, ufafanuzi huo umetokana na kikao cha tathmini kilichofanywa na wajumbe wa iliyokuwa Tume hiyo ya Warioba, kilichofanyika Jumatatu wiki hii ya Machi 24, mwaka huu jijini Dar es Salaam, baada Tume kuhitimisha kazi yake hiyo.

Maeneo ambayo Tume hiyo imeyafanyia ufafanuzi ni pamoja na Usanifu wa Katiba; Malengo muhimu na mwelekeo wa shughuli za Serikali na sera za kitaifa (Dira); Nchi mbili, Serikali mbili; Mamlaka ya Rais; Orodha ya mambo ya Muungano; Katiba na Mamlaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; Mamlaka ya Mahakama ya Rufani na takwimu kuhusu maoni ya wananchi juu ya muundo wa Muungano.Ufafanuzi kamili ni kama ifuatavyo:-

UTANGULIZI

Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika kutekeleza majukumu iliyopewa imetoa taarifa ya Tume yenye viambatisho vingi na vyenye maelezo ya kina kuhusu mchakato wa kuratibu, kukusanya, kuchambua maoni ya wananchi na kuandaa ripoti.

Baada ya kukamilisha kazi hiyo, Tume iliwasilisha Rasimu ya Katiba katika Bunge Maalumu la Katiba Machi 18, mwaka huu. Pamoja na Rasimu hiyo, Tume iliwasilisha Randama ya Rasimu ya Katiba na Bango kitita la Randama ya Rasimu ya Katiba ambayo ilitoa maelezo ya kila Ibara ya Rasimu ikitoa maudhui, madhumuni na lengo pamoja na sababu za mapendekezo ya kila Ibara.

Tangu kuwasilishwa kwa Rasimu na vyaraka zilizoambatana nayo katika Bunge Maalumu la Katiba, kumejitokeza tafsiri tofauti kuhusu baadhi ya mapendekezo yaliyomo kwenye Rasimu ya Katiba na baadhi ya taarifa zilizoambatana na Ripoti ya Tume. Katika maeneo ambayo kumekuwepo na tafsiri tofauti tofauti, ufafanuzi wa kina umetolewa kwenye Randama na bango kitita ya Randama ya Rasimu ya Katiba.

Kutokana na hali hiyo, Tume ya Mabadiliko ya Katiba, katika kikao chake cha tathmini ya kuhitimisha kazi kilichofanyika Machi 24, mwaka huu, jijini Dar es Salaam, imeamua kutoa maelezo ya ziada ya ufafanuzi kama ifutavyo:-

NCHI MBILI SERIKALI MBILI

Tangu Mwaka 1984 hatua ambazo zimechukuliwa na serikali zote mbili za Muungano na Zanzibar zimeifanya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka kuwa Nchi Moja yenye Serikali mbili na kuwa Nchi mbili zenye Serikali mbili. Kwa maana nyingine Masharti yaliyomo katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano yanaelekeza kwamba Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Nchi moja yenye Serikali mbili- Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Kufuatia Mabadiliko ya 10 ya Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984, Zanzibar imetamka ni Nchi tofauti na ilivyokuwa imetamka kwamba ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano kabla ya Mabadiliko hayo.

Wakati Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwa ni Nchi moja, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilikuwa na Mamlaka ya Kutunga Sheria juu ya Mambo ya Muungano kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yote, sasa uwezo huo umewekewa mipaka na Katiba ya Zanzibar Katika Ibara ya 132 ambayo inaelekeza kwamba Sheria iliyopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kabla ya kuanza kutumika Zanzibar ipelekwe kwenye Baraza la Wawakilishi na kupata ridhaa ya kutumika Zanzibar .Zipo Sheria zilizotungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zilipokosa ridhaa ya Baraza la Wawakilishi zilirejeshwa katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kufanyiwa marekebisho ili kukidhi maelekezo ya Baraza la Wawakilishi, kwa mfano, Sheria ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (Commission for Human Rights and Good Governance Act) na Sheria ya Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu (Deep Sea Fishing Authority Act)

MAMLAKA YA RAIS

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 imempa Rais wa Jamhuri ya Muungano mamlaka ya kuigawa Jamhuri ya Muungano katika maeneo ya kiutawala katika Mikoa na Wilaya. Hata hivyo, Marekebisho ya 10 ya Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984 yanampa Rais wa Zanzibar Mamlaka kama hayo ya kuigawa Zanzibar bila kufanya marekebisho stahiki ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Mwaka 1977. Kwa mantiki hiyo mamlaka ya Rais wa Jamhuri ya Muungano yamepungua na kubaki kwa Tanzania Bara tu.

MAMLAKA YA MAHAKAMA YA RUFANI

Katiba ya Muungano ya 1977 imetoa mamlaka ya kusikiliza rufaa nchi nzima. Lakini Zanzibar imezuia Mahakama hiyo kusikiliza rufaa kutoka Mahakama za Kadhi, kutafsiri Katiba ya Zanzibar na rufaa kuhusu mashauri ya haki za binadamu.

Kwa kifupi:

Waasisi walituachia mambo 21 (ukiacha usajili wa vyama) kwenye orodha ya Muungano. Katika kipindi cha miaka ishirini iliyopita yamepunguzwa. Mambo yote yaliwekwa kwa utaratibu uliowekwa na Katiba lakini yameondolewa kinyume na Katiba. Sehemu zote mbili ziliamua kuachia baadhi ya mambo yake kuwa chini ya Serikali ya Muungano, sasa sehemu moja inaondoa mambo yake. Kwa hiyo serikali ya Muungano itakuwa inashughulikia zaidi mambo ya upande mmoja.
Waasisi walituachia Bunge lenye madaraka nchi nzima. Sasa ni lazima lipate idhini ya Baraza la Wawakilishi.
Waasisi waliacha Rais akiwa na madaraka kamili. Madaraka hayo yamepunguzwa bila kufuata utaratibu wa Katiba.
Waasisi walituachia Mahakama ya rufani yenye madaraka kamili. Madaraka haya yamepunguzwa.
Waasisi waliunganisha nchi mbili ikawa moja. Sasa tunazo nchi mbili.

Hii ndiyo inafanya wananchi wa Tanzania Bara waamini Zanzibar ni huru katika mambo yao. Wanaona ina mamlaka kamili kushughulikia mambo yake na imechukua rasilimali zake. Serikali ya Muungano imebaki na mamlaka na rasilimali za Tanzania Bara. Wabunge wa Zanzibar wanashiriki kuamua mambo ya Tanzania Bara lakini wabunge wa Tanzania Bara hawana nafasi ya kushiriki katika kuamua mambo ya Zanzibar.

Tume iliona ni vigumu kwa Zanzibar kurudi kwa hiyari kwenye hali ya awali, yaani kurudisha mambo yote yaliyotolewa kwenye orodha ya Muungano, kurudisha madaraka ya Rais na kufuta kipingere cha nchi mbili kwenye Katiba yake. Tume iliona kwamba pamoja na mambo haya kufanywa kinyume na Katiba ya Muungano hali ibaki hivyo hivyo. Lakini kwa kufanya hivyo basi malalamiko ya Tanzania Bara nayo yasipuuzwe. Hivyo Tume nayo ikapendekeza Serikali ya Tanganyika iundwe.

HITIMISHO

Tume inapenda kuwashukuru wananchi wote kwa shauku kubwa ya kutaka ufafanuzi wa mambo mbalimbali kuhusu Rasimu ya Katiba. Tunawaomba wananchi wasome Randama ya Rasimu ya Katiba ambayo kwa sasa inapatikana katika tovuti yetu
- See more at: http://www.raiamwema.co.tz/warioba-amjibu-kikwete#sthash.9jda7jsX.dpuf

Friday, 21 March 2014

UCB yatoa mkopo wa bilion 9.2

BENKI ya Uchumi (UCB) inayomilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini, imefanikiwa kutoa mikopo ya zaidi ya shilingi bilioni 9.2 kwa kipindi cha miaka nane, lengo likiwa ni kuwawezesha wateja wake kuendesha miradi mbalimbali ya maendeleo na kujikwamua kiuchumi.
Hayo yalibainishwa jana na Meneja mkuu wa Benki hiyo Bi. Angela Moshi, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mafanikio mbalimbali waliyoyapata toka kuanzishwa kwa benki hiyo mwaka 2005.
Bi.Moshi alisema benki hiyo imeendelea kukua kwa kasi na hadi kufikia Desemba 31 mwaka jana, rasilimali zake zilifikia bilioni 17, Amana sh. bilioni 13, Hisa sh. bilioni 2.5 na mikopo iliyotolewa ikifikia sh.bilioni 9.2.
"Benki yetu ya uchumi imeendelea kukua kwa kasi na tangu kuanzishwa kwake mwaka 2005 hadi Desemba 2013 tumeshafanikiwa kutoa mikopo ya sh.bilioni 9.2 na katika kipindi cha mwaka jana 2013, benki hii ilipata faida ya sh. milioni 603 baada ya kulipa kodi ya serikali ya sh.milioni 150," alisema Bi.Moshi.
Meneja huyo akizungumzia huduma zinazotolewa na benki hiyo alisema kwa sasa zimefikia huduma 13, na moja ya huduma hizo ni utoaji huduma kupitia simu ya mkononi (UCB Mobile).
Alisema UCB Mobile inaenda sambamba na nia na shabaha ya kuanzishwa kwa benki hiyo ambayo ni kuwafikia wananchi wengi hususan wale wa kipato cha chini na waishio maeneo ya vijijini ikiwa ni pamoja na kuwapatia huduma za kifedha kwa gharama nafuu.
Alisema huduma ya UCB Mobile inafaida nyingi kwa wateja ikiwa ni pamoja na kupunguza msongamano ndani ya benki,kuwezesha wateja kuweka, kurejesha mikopo na kutoa fedha kwa haraka zaidi bila usumbufu.
"Huduma hii ya UCB Mobile ni ya uhakika na inafaida nyingi, kwani mteja wetu anaweza kupata huduma za kibenki akiwa mahali popote, anaweza kulipia huduma mbalimbali ikiwemo ada za shule, ada ya mtihani na huduma nyingine nyingi," alisema.
Meneja huyo alitumia nafasi hiyo kuwataka wateja wa benki hiyo kujiunga na UCB Mobile na kwa wananchi ambao hawana akaunti kujitokeza kufungua akaunti katika benki hiyo, ili kuweza kunufaika na huduma mbalimbali zitolewazo na benki hiyo.
Akizungumza mwenyekiti wa Bodi ya UCB Wilson Ndesanjo, alisema tangu kuanzishwa kwa benki hiyo imeweza kuwapa wanahisa wake gawio lililotokana na faida mara nne, hivyo kutoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro na mikoa mingine,kununua hisa za benki hiyo kama njia ya uwekezaji wa uhakika

Mtikila asema wajumbe wanatishwa

Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, Mchungaji Christopher Mtikila amedai kwamba kuna vitisho vinavyotolewa vya kuwashughulikia wajumbe wanaopinga Muungano.

Amedai kwamba kumekuwa na uvunjaji wa kanuni na Katiba ya nchi waziwazi unaofanywa na kikundi kidogo cha watu ambao wanatishia wasiowaunga mkono.

Alitoa kauli hiyo jana mchana alipokuwa akiuliza swali katika semina ya Bunge hilo iliyokuwa ikiendeshwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Katiba Kenya, Amos Wako.

Wako ambaye ni Seneta wa Busia Mashariki na aliyewahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Kenya, alialikwa katika Bunge la Katiba kutoa uzoefu wa namna nchi hiyo ilivyopita katika mchakato huo.

“Mimi nililonalo halihusu mazungumzo tuliyopata kutoka kwa wenzetu wa Kenya, ni kuhusu Kanuni ya 4, uhuru wa maoni na kujieleza. Waheshimiwa wabunge, ndani ya Bunge hili ni juzi kulikuwa na watoa mada na wachangiaji wazuri. Nimetafakari kwa uzalendo wangu na ukomavu wangu wa kisiasa nikaona tusipojadiliana, tutaharibu matarajio ya wananchi na sitaogopa suala la kuwa tutashughulikiwa kama wenzetu.”

Mchungaji Mtikila alisema kumekuwa na vitisho kwa baadhi ya wajumbe ambavyo vinalenga kuwafunga midomo wajumbe ambao wanawakilisha kundi la Watanzania milioni 45.

Mtikila alisema kumekuwa na vitisho kwa baadhi ya wajumbe wanaopinga Muungano akisema msimamo huo unatoka katika kikundi alichokiita ni cha CCM.

Akifafanua, alisema hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Profesa Mark Mwandosya aliyoitoa juzi ilikuwa nzuri, pia ilijaa vitisho.

Katika mchango wake, Profesa Mwandosya aliwataka wajumbe wa Bunge hilo kuwa makini na watulivu wakati wa kusikiliza hotuba ya Rais leo na kuacha zomeazomea.

Mtikila alidai kwamba Profesa Mwandosya alisema Rais wa nchi ni Amiri Jeshi Mkuu ambaye ana uwezo wa kuamuru chochote kauli ambayo hata hivyo, ilitolewa na mjumbe mwingine, Dk. Zainab Gama ambaye alimtaka Mwenyekiti wa Bunge, Samuel Sitta kutumia kanuni kuwadhibiti wajumbe wanaokwenda kinyume na kanuni walizojiwekea.

Mtikila alidai kuwa misimamo imewahi kuwadhuru waliosimamia ukweli ambao walishughulikiwa akiwataja Dk. Stephen Ulimboka, Horace Kolimba na Dk. Sengondo Mvungi.

“Hata mimi nilishangilia kwa baadhi ya maeneo kuhusu suala la ujio wa Rais, lakini Mwandosya alitoa mifano ya nchi kadhaa huku akisahau kuwa tumeona kina Tony Blair (aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza), wakipigwa mayai viza, akataka tukumbuke kuwa anayekuja ni amiri jeshi mkuu... hii ni kujenga hofu kwa wabunge,” alisema Mtikila.
Mjumbe huyo alisema aliyeajiriwa na akafanya vizuri anapaswa kushangiliwa lakini aliyekosea ni vyema akakosolewa kwa kuzingatia uhuru wa mtu kwa mujibu wa Kanuni 4 ya Bunge hilo na Ibara ya 100 ya Katiba Kifungu cha 27 (2) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba.

Alijipambanua kuwa amekwenda Dodoma akiwa na msimamo mmoja ambao kila mtu anaufahamu kuwa anapinga Muungano kwa sababu anaitaka Tanganyika.

Akijibu hoja hizo, Sitta alisema katika nchi ya kidemokrasia kama Tanzania ambayo inaongozwa kwa sheria, watu wanashughulikiwa kwa sheria.

Alisema ndani ya Bunge kinachowashughulikia watu ni kanuni, akasema hatarajii kuona watu wakiingia na mayai viza ndani ya Bunge kwa ajili ya kumpiga mtu yeyote.

Alisema kilichoelezwa na Profesa Mwandosya kilikuwa ni umuhimu wa kuwapo staha bungeni na siyo vitisho kwa wajumbe na kwamba kama kuna watu ambao wanaweza kuwa na hasira, kuna njia nyingi za kuzionyesha lakini siyo ndani ya Bunge. Alimtaka Mchungaji Mtikila asiogope na awe na amani.

CHELSEA yaiadhibu Galatasaray 2 0

CHELSEA ndiyo timu pekee ya Uingereza iliyojihakikishia nafasi ya kushiriki mechi za robo fainali za Ligi ya Mabingwa barani Ulaya baada ya kuinyamazisha Galatarasay ya Uturuki kwa mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Stamford Bridge.
Kwa mujibu wa BBC, matokeo hayo yanaipa Chelsea ushindi wa jumla ya mabao 3-1.
Hatua ya kocha Jose Mourinho kumpumzisha mshambulizi wake, Fernando Torres, na badala yake kumchezesha nyota wa Cameroon, Samuel Eto'o, ilizaa matunda punde baada ya kipenga cha kwanza.
Etoo ambaye majuzi alikejeliwa kutokana na umri wake mkubwa alimnyamazisha Mourinho kwa kufunga bao la kwanza kunako dakika ya nne na kufufua matumaini ya mashabiki wa Chelsea na hasa Uingereza.
Wawakilishi wengine wa Uingereza Manchester city na Arsenal tayari wameondolewa kwenye mashindano hayo, hivyo matumaini ya Waingereza yamebaki kwa Chelsea.
Vijana wa Stanford Bridge hawakuzembea, kwani waliendeleza gongagonga hadi dakika tatu kabla ya kipenga cha mwisho kipindi cha kwanza wakati mkwaju wa John Terry ulipotemwa na kipa wa Galatasaray, Fernando Musiera na kisha Garry Cahili akacheka na wavu na Kuihakikishia Chelsea fursa ya kusonga mbele.
Katika mechi ya awali iliyochezwa nchini Uturuki, timu hizo zilimaliza mchezo kwa matokea 1-1.
Mshambulizi wa Galatasaray, Didier Drogba, alishindwa kung'ara Stamford Bridge na badala yake kushuhudia timu yake ya zamani ikifuzu robo fainali Ligi ya Mabingwa.
Chelsea wanaungana na vinara wa ligi kuu Hispania, Real Madrid, ambao wamefuzu robo fainali baada ya jana kuichapa Shalke 04 ya Ujerumani kwa mabao 3-1.
Real wamepata ushindi wa jumla ya mabao 9-2 baada ya mchezo huo wa marudiano uliochezwa Uwanja wa Bernabeu.

Mtoto abakwa na kuuwawa kwa kuvunjwa shingo

MTOTO wa miaka 13, mkazi wa Kijiji cha Nyangoto Kata ya Matongo wilayani Tarime mkoani Mara (jina linahifadhiwa) amefariki baada ya kubakwa kisha kuvunjwa shingo na paja la mguu wake wa kulia.
Kamanda wa Mkoa wa Polisi Tarime/Rorya Justus Kamugisha, aliwaambia waandishi wa habari ofisini kwake jana kuwa tukio hilo lilitokea saa 6.30 mchana juzi.
Kamugisha aliongeza kuwa marehemu kwa mara ya mwisho alionekana akiongozana na mwanaume mmoja (jina tunalo) ambaye anadaiwa kutoroka baada ya kutenda tukio hilo. Alisema chanzo cha tukio hilo ni tamaa ya ngono.
"Mtoto huyo aligundulika akiwa tayari amekufa baada ya kubakwa na alikutwa amevunjwa shingo na paja la upande wa kulia,"alisema.
Juhudi za Jeshi la Polisi za kumtafuta mtuhumiwa ambaye alitoroka baada ya kutenda tukio hilo zinaendelea ili afikishwe kwenye vyombo vya sheria.
Kwa upande wa Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya Nyangoto, Dkt. Kaijage Kagumilwa, alisema kuwa walipokea mwili wa marehemu saa saba mchana siku ya tukio.
Mwili wa mtoto huyo ulikutwa na majeraha mwilini. Dkt Kagumilwa alifafanua kuwa mtuhumiwa wa tukio hilo ana matatizo ya akili na kwamba ni ndugu wa karibu na marehemu.

Monday, 17 March 2014

Chadema yafa kiume kalenga

Polisi akilinda Kituo cha Kupigia Kura cha Shule ya Chekechea ya Mchwivila katika Jimbo la Kalenga, Iringa jana

Mgombea wa CCM, Godfrey Mgimwa anaonekana kufanya vizuri katika uchaguzi mdogo wa ubunge uliofanyika jana katika Jimbo la Kalenga, mkoani Iringa.

Mgimwa aliwaacha mbali mshindani wake wa karibu, Grace Tendega wa Chadema na Richard Minja wa Chausta.

Kutokana na hali hiyo, wafuasi wa CCM katika sehemu mbalimbali za jimbo hilo na Mjini Iringa walikuwa wakishangilia kile walichokiita ushindi wa kishindo.

Watu 71, 765 walitarajiwa kupiga kura katika vituo 216, lakini waandishi wa Mwananchi walisema kulikuwa na idadi ndogo ya watu waliojitokeza katika baadhi ya vituo, huku wengi wakilalamika kushindwa kupiga kura kutokana na kupoteza vitambulisho.

Vituo vya kupigia kura vilifungwa saa 10:00 na kazi ya kuhesabu kura ilianza mara moja na matokeo yalianza kubandikwa kwenye vituo husika kuanzia saa 11:00 jioni huku CCM kikionekana kufanya vizuri kuliko vyama vingine.

Msimamizi wa Uchaguzi, Jimbo la Kalenga, Purdenciana Kisaka alisema uchaguzi ulifanyika kwa ufanisi... “Mimi na timu yangu hivi sasa tunajiandaa kupokea masanduku ya kura, ili tujumlishe na kuona kile kilichomo. Tutatangaza matokeo mapema kadiri inavyowezekana,” alisema Kisaka.

Matokeo ambayo yalikuwa yamebandikwa vituoni na kunukuliwa na waandishi wetu ni kama ifuatavyo:

Kata ya Ifunda:

Kituo cha Zahanati ya Kibena na. 1; CCM 93, Chadema 36, Chausta 2, Zahanati na.2: CCM 91, Chadema 28, Chausta 0, Shule ya Msingi Kibena CCM 91, Chadema 23, Chausta 0, Ofisi ya Kijiji Ifunda A; CCM 84, Chadema 73, Chausta 1, Kituo B; CCM 75, Chadema 76, Chausta 0.

Kituo cha Kivalali Nyumba ya Mifugo na. 2; CCM 109, Chadema 14, Chausta 1, Kivalali na. 1: CCM 99, Chadema 19, Chausta 1, Kilimahewa B Ofisi ya Kitongoji; CCM 57, Chadema 32, Chausta 1.

Kata ya Maboga:

Kijiji cha Makongati Kituo cha Josho, CCM 120, Chadema 13, Chausta 1, Shule ya Msingi Makongati; CCM 160, Chadema 9, Chausta 2,Kijiji cha Kiponzelo, Kituo cha Msombe; CCM 98, Chadema 13, Chausta 0, Shule ya Msingi Kiponzelo; CCM 45, Chadema 5, Chausta 1.
Ofisi ya Kijiji; CCM 231, Chadema 18, Chausta 1, Ofisi Baraza; CCM 207, Chadema 8, Chausta 1, Kijiji cha Magunga, Shule ya Msingi; CCM 180, Chadema 02, Chausta 0, Jengo la Josho Magunga; CCM 184, Chadema 4, Chausta 1

Kata ya Mgama:

Shule ya Msingi Katenge na 1; CCM 90, Chadema 23, Chausta 0, Katenge na 2; CCM 92, Chadema 28, Chausta 1, Shule ya Msingi Mgama; CCM 122, Chadema 40, Chausta 1, Zahanati ya Ihemi; CCM 117, Chadema 67, Chausta 1, Ofisi ya Kijiji Ihemi; CCM 117, Chadema 53, Chausta 0, Mgama Zahanati; CCM 110, Chadema 38, Chausta 0.

Ofisini Mgama; CCM 109, Chadema 44, Chausta 0, Kituo cha Mawasiliano; CCM 97, Chadema 27, Chausta 0.

Kata ya Kiwele

Shule ya Msingi Itagutwa; CCM 105, Chadema 39, Chausta 2, Itagutwa Ofisini; CCM 88, Chadema 43, Chausta 1, Itangutwa Kipengele; CCM 90, Chadema 60, Chausta 2, Malamba B; CCM 148, Chadema 21, Chausta 1, Godauni; CCM 79, Chadema 65, Chausta 1, Ofisi ya Kijiji Kiwele; CCM 99, Chadema 39, Chausta 3.

Shule ya Msingi Kiwele; CCM 61, Chadema 30, Chausta 0, Matembo; CCM 47, Chadema 7, Chausta 0, Mfyome Godauni; CCM 143, Chadema 29, Chausta 0.

Shule ya Msingi Mgera; Chadema 108, CCM 42, Chausta 0, Kidete; CCM 43, Chadema 38, Chausta 1, Mapinduzi; CCM 96, Chadema 65, Chausta, Kidete Ofisi ya zamani; CCM 142, Chadema 58 na Chausta 1.

Kata ya Lumuli

Kituo cha Shule ya Msingi Muwimbi; CCM 164, Chadema 22, Chausta 1, Ofisi ya zamani Muwimbi; CCM 116, Chadema 10, Chausta 0, Shule ya Msingi Muwimbi ‘B’; CCM 87, Chadema 11, Chausta 0, Shule ya Msingi Kitapulimwa; CCM 52, Chadema 58, Chausta 0.

Kata ya Nzihi

Kijiji cha Magubike Kituo Ibogo A; CCM 88, Chadema 19, Chausta 1, Ibogo B; CCM 107, Chadema 15, Chausta 1, Kijiji cha Kidamali A; CCM 91, Chadema 76, Chausta 0, Kidamali B; CCM 94, Chadema 52, Chausta 0, Kijiji cha Nyamihuu, Ofisi ya Kijiji A; CCM 80, Chadema 38, Chausta 0, Kituo B; CCM 58
Nyamihuu Shuleni; CCM 44, Chadema 33, Chausta 0, Nzihi Katani A; CCM 112, Chadema 34, Chausta 1, Kituo B; CCM 116, Chadema 32, Chausta 2,

Kata ya Wasa

Kijiji cha Usengelindete, Zahanati; CCM 260, Chadema 46, Chausta 1, Shule ya Msingi Usengelindete; CCM 116, Chadema 7, Chausta, Kijiji cha Mahanzi, Ofisi ya Kijiji; CCM 130, Chadema 46, Chausta 2, Mahanzi, Ofisi ya Kijiji; CCM 130 Chadema 46, Chausta 2.

Ofisi ya Kijiji cha Mahanzi; CCM 130, Chadema 46, Chausta 2, Ofisi ya Kijiji cha Wasa 1; CCM 149, Chadema 15, Chausta 0, Ofisi ya Wasa 2; CCM 82, Chadema 16, Chausta 0.

Kata ya Luhota

Ofisi ya Kata Luhota; CCM 114, Chadema 48, Chausta 1, Matema Moja; CCM 111, Chadema 34, Chausta 2, Shule ya Msingi Kilambo; CCM 96, Chadema 49, Chausta 2.

Kata ya Kalenga

Chekechea Masukanzi na.2; Chadema 11, CCM 40, Chausta 1, Tosamaganga 1; CCM 3, Chadema 2, Chausta 0, Ofisi Tarafa ya Kalenga; CCM 106, Chadema 26, Chausta 0, Ofisi ya Kijiji cha Kalenga no 1; CCM 134, Chadema 34, Chausta 1, Ofisi ya Kijiji na.2; CCM 168, Chadema 34, Chausta 0.

Kata ya Ulanda

Ofisi ya Kijiji Ibangamoyo CCM 119, Chadema 43, Chausta 1, Mangalali; CCM 196, Chadema 37, Chausta 1, Kituo cha Mwika; CCM 60, Chadema 13 na Chausta 0.

Kata ya Lyamgungwe

Shule ya Msingi Lyamgungwe; CCM 142, Chadema 12 na Chausta 1.
Kata ya Mseke

Kijiji cha Kilindi; CCM 69, Chadema 23, Chausta 23.

Mbali ya kata hizo, habari zilizopatikana wakati tukienda mitambo zilisema CCM ilikuwa ikiongoza katika kata nyingine nyingi.

Awali

Uchaguzi huo uliambatana na matukio kadhaa likiwamo la kukamatwa kwa Msimamizi wa Kituo cha Zahanati ‘B’ katika Kata ya Magulilwa, Benjamin Charles (60) akituhumiwa kumpa karatasi mbili za kupigia kura mpiga kura, Michael John wa Kitongoji C.

Kisaka alisema baada ya msimamizi huyo kukamatwa, alituma msimamizi wa akiba kuendelea na kazi.

“Nimemtuma mwanasheria wetu akaangalie hilo tatizo, suala kama hili tunalifanyia kazi kama tatizo binafsi la msimamizi, kwa hiyo baada ya mwanasheria kurejea tutajua kilichotokea lakini taratibu za kisheria zitachukua mkondo wake,” alisema Kisaka.

Imeandikwa na Geofrey Nyang’oro, Beldina Majinge, Rose Mnyeti, Shaman Lupimo, Hawa Kalinga, Hakimu Mwafongo, Zainab Maeda, Clement Sanga na Saidi Ng’amilo.

Friday, 14 March 2014

MB; DOG kuachia song Mpya hivi karibuni

MKALI wa muziki wa kizazi kipya nchini, Mbwana Mohammed maarufu kama Mb Dogg, yupo kwenye mipango ya kuachia wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la Baby mbona umenuna?
Mb Dogg pichani, wimbo wake mpya wa 'Baby Mbona Umenuna' utakuwa balaa na unatarajiwa kumuweka tena kileleni.


Wimbo huo umerekodiwa katika Studio za Maccopa, ambapo unatarajiwa kurudisha makali na heshima ya msanii huyo aliyewahi kuwika katika tasnia hiyo.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Kampuni ya Qs Mhonda J Entertainment, Joseph Mhonda, alisema kwamba wimbo huo ni moto wa kuotea mbali ambao kwa kiasi kikubwa utamuweka juu zaidi.


Alisema kwamba Mb Dogg ni msanii aliyejichimbia kwa muda mrefu akiwa na mahitaji ya kurudi kwenye nafasi zake za juu alipokuwa awali.


“Sisi kama Kampuni tunaofanya kazi na Mb Dogg tunaamini kabisa huu ni wakati wake wa kurudi tena kileleni ili aendeleze makali yake ya awali.

“Baby Mbona umenuna ni wimbo ambao kwa hakika utadhihirisha ubora wa mwimbaji huyu wa Latifa na nyinginezo zilizomuweka kileleni,” alisema.

Mb Dogg anatokea katika kampuni hiyo kwa sasa, akiwa sambamba na Nay wa Mitego anayetamba na wimbo wa Muziki Gani, aliyeimba na Diamond.

Coastal kuifuata Azam

TIMU ya Coastal Union, yenye maskani yake jijini Tanga, inajiandaa vizuri kukabiliana na joto katika mchezo wao dhidi ya Azam utakaopigwa Jumamosi ya Machi 15, katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

Mechi hiyo inachezwa huku kukiwa na marekebisho kadhaa, hasa kati ya Simba na Costal, waliopangwa kucheza Jumatano, kabla ya mechi hiyo kusogezwa mbele hadi Machi 23.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Msemaji wa Costal Union, Hafidh Kido, alisema kuwa wanajiandaa vyema ili kusaka ushindi dhidi ya Azam.

Alisema ingawa wamepata matokeo mabaya ya sare dhidi ya Ashanti United, ila bado hawajakata tamaa katika patashika ya Ligi ya Tanzania Bara.

“Coastal bado hatujakatishwa tamaa katika harakati za kuiweka juu zaidi timu yetu, hivyo kwa sasa tunajiandaa kuwakabiri Azam.

“Naamini utakuwa ni mchezo mgumu kupita kiasi, ukizingatia kuwa Azam wao wanasaka ubingwa, hivyo watataka mbeleko kutoka kwetu, jambo ambalo haliwezekani kirahisi,” alisema.

Simba inayonolewa na kocha wake Zdravko Logarusic, imeshindwa kuonyesha cheche za kuunyaka ubingwa wa Tanzania Bara, baada ya kuendelea kupata matokeo mabaya katika mechi zake.

Roboti kuongoza magari Dar

Magari yakipita pembeni mwa roboti anayeyaongoza katika moja ya barabara za jiji la Kinshasa, Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Tanzania inatarajia kuweka roboti hao ili kupunguza mzigo wa kuongoza kwa askari wa usalama barabarani ambao mmoja huudumia magari yapatayo 1,400 kwa siku

Matumizi ya roboti katika kuongoza magari imeelezwa kwamba inaweza kusaidia kukabiliana na tatizo la foleni za magari Jijini Dar es Salaam.

Mkakati huo umeelezwa kwamba utakuwa mbadala bora zaidi wa taa au askari wa usalama barabarani ambao wamekuwa wakiongoza magari kwenye makutano ya barabara.

Katika maeneo mengi, taa za kuongoza magari zimeshindwa kusaidia kupunguza msongamano huku askari hao wakitupiwa lawama na baadhi ya watumiaji wa barabara kwamba wamekuwa wakipendelea upande mmoja.

Roboti zimeonekana kuwa na sifa ya kipekee kwa uwezo wake wa kuongoza magari bila upendeleo hasa kwa kuhakikisha hakuna upande unaoelemewa na msongamano.

Kwa mujibu wa Mtandao wa Televisheni ya CCN ya Marekani, Jiji la Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) limefanikiwa kutumia roboti kuongoza magari na kupunguza foleni kwa kiwango kikubwa.

Roboti mbili zimefungwa katika jiji hilo na zinafanya kazi hiyo kwa saa 24, huku zikitumia kamera maalumu kurekodi kila tukio na kurahisisha kuwabaini wanaokiuka sheria za usalama barabarani.

Roboti hizo ambazo zimetengenezwa na Wakongo wenyewe, zina urefu wa futi nane na zinafanya kazi kwa saa 24 zikitumia nguvu za jua.

Zina uwezo wa kuinua na kushusha mikono wakati wa kuzuia au kuruhusu magari. Pia zina uwezo wa kuwaeleza waenda kwa miguu wakati mwafaka wa kuvuka barabara.

Mapema mwaka huu, Kenya ilifunga kamera maalumu (CCTV) kwa ajili ya kuongoza magari na kuratibu makosa ya barabarani katika jiji la Nairobi.

Hivi karibuni, Kamanda wa Usalama Barabarani Tanzania, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP), Mohammed Mpinga alikaririwa akielezea umuhimu wa kufunga kamera hizo kwa lengo la kuimarisha usalama.

Mataifa yenye magari mengi kama China ambayo ina magari milioni 120 yaliyosajiliwa imechukua hatua madhubuti kukabiliana na foleni katika miji yake.

Moja ya mikakati hiyo ni kuimarisha usafiri wa umma na kuweka tozo maalumu kwa wanaoingia na magari binafsi mijini.
Kwa Dar es Salaam, mikakati iliyopo sasa ni ujenzi wa barabara kwa ajili ya mabasi yaendayo kasi ambao umeshaanza kuanzia Kivukoni hadi Kimara, usafiri wa treni kuanzia Ubungo hadi Stesheni na Pugu Mwakanga mpaka Kurasini na ujenzi wa barabara za juu, Ubungo na Tazara ambao hata hivyo, haujaanza.

Wakati huohuo, Manispaa ya Temeke imeeleza mkakati wa kupunguza foleni.

Ofisa Uhusiano wa Manispaa ya Temeke, Joyce Msumba alisema jana kwamba katika mkakati huo, itapanua Barabara za Temeke Sokota-Mtoni kwa Aziz Ali; Kizuiani-Kibada na Mbagala Kilungule-Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.

Alisema upanuzi wa barabara hizo utakaoanza mwakani, uko katika Mradi wa Maendeleo ya Jiji la Dar es Salaam unaofadhiliwa na Benki ya Dunia. “Barabara hizo zitakuwa za njia nne ambazo zitakuwa na vituo vikubwa vya daladala na zikikamilika, zitapunguza msongamano wa magari kwa kiasi kikubwa,” alisema.

Msumba alisema baadhi ya nyumba zitabomolewa kupisha ujenzi huo na wakazi wake watalipwa fidia.

Alisema wakati wa upanuzi wa Barabara ya Temeke Sokota- Mtoni kwa Aziz Ali, Kituo cha daladala cha Temeke Mwisho kitavunjwa.

Kituo hicho kilijengwa na manispaa hiyo kwa gharama ya Sh126 milioni na tangu kilipokamilika mwaka 2012, hakijawahi kutumika. Daladala zilizotakiwa kukitumia zinaishia Tandika ambako hakuna kituo maalumu.

DRC

Roboti mbili zimefungwa katika jiji la Kinshasa, DRC na zinafanya kazi hiyo kwa saa 24, huku zikitumia kamera maalumu kurekodi kila tukio na kurahisisha kuwabaini wanaokiuka sheria za usalama barabarani

Monday, 10 March 2014