Monday 10 March 2014

Man city yapigwa nje na wingan

abingwa watetezi wa kombe la FA, Wigan imejikatia tikiti ya nusu fainali ya kombe hilo baada ya kuilaza Manchester City kwa magoli mawili kwa moja katika uwanja wa Etihad.
Wachezaji wa Wigan wakisherehekea ushindi wao dhidi ya Man City

Wigan sasa itachuana na Arsenal katika mechi hiyo itakayochezwa katika uwanja wa Wembley.

Kwa mwaka wa pili mfululizo Wigan imeishinda Manchester City katika kinyanganyiro hicho, mwaka uliopita iliishinda City katika fainali na kutwa kombe hilo.

City, ambayo ilishinda kombe la ligi wikendi iliyopita, ileta kombe hilo uwanjani kabla ya mechi hiyo kuanza, lakini matumaini yao ya kushinda vikombe vitatu msimu huu sasa imetumbukia nyongo.
Kilio cha huzuni kwa Man City

Jordi Gomez, aliifungia Wigan bao la kwanza kupitia mkwaju wa penalti, baada ya linda lango wa City kumfanyia madhambi mchezaji wa Wigan.

Dakika chache baada ya kipindi cha pili kuanza James Perch naye akaongeza la pili.

Manchester City ilipata bao lake la kuvutia machozi kupitia kwa nyota wake Samir Nasri.

Licha ya kufanya mashambulizi kadhaa katika lango la wageni wao, juhudi za City zilizimwa na walinda lango wa Wigan.

Katika matokeo ya mechi zingine zilizochezwa hiyo jana, Sheffeild United iliinyuka Charton magoli mawili bila jibu, Sunderland nayo ikanyeshewa magoli matatu bila jibu na Hull City.

Katika hatua ya nusu fainali, Wigan kutoana jasho na Arsenal huku Sheffeild United ikipepetana na Hull City.

No comments: