Friday 31 January 2014

Polisi wapambana na wananchi Karatu


Mamia ya wananchi wenye hasira katika Kijiji cha Bashay kilichoko wilayani hapa wamepambana na polisi kwa kuwarushia mawe kwa kile walichodai kuishinikiza Serikali kuweka matuta katika Barabara ya Karatu hadi Ngorongoro.

Tukio hilo lililotokea saa 4 asubuhi baada ya watoto wawili Priska John(5) na Happiness Filbert (5) walipogongwa na gari wakati wakivuka barabara ambapo mmoja alifariki dunia papo hapo huku Priska akikimbizwa hospitali.


Wananchi hao walifikia uamuzi huo wa kufunga barabara na kuzuia magari yakiwamo ya watalii kwa nia ya washinikiza mkuu wa wilaya kwenda kuwasikiliza na ndipo polisi walipojaribu kuondoa mawe hayo bila mafanikio.

“Tumechoka kuwaona polisi wakiokota maiti za watoto wetu barabarani kama wanaokota mizoga ya mbwa na leo(jana) tunawapiga mawe mpaka wakitumwa tena kuja kuchukua maiti ya aliyegongwa na gari wakatae,”alisikika mama mmoja akipaza sauti kwa uchungu.

Vurugu kati ya wananchi na polisi zilianza huku wananchi wakiporomosha mawe pasipo kujali wanarushia polisi au magari yaliyokuwa yakipita huku polisi walipambana kwa kurusha mabomu ya machozi kwa takribani saa mbili.

Hata hivyo katika vurugu hizo hakuna aliyeripotiwa kuumia huku wananchi wakiitupia lawama Serikali kwa kushindwa kuweka matuta katika barabara hiyo ambapo mara kwa mara ajali zimekuwa zikiripotiwa kutokea katika Barabara ya Karatu hadi Ngorongoro.

Akizungumzia tukio hilo Mtendaji wa Kijiji cha Bashay, Joseph Surumbu alikiri kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema, ajali katika eneo hilo zimekuwa zikitokea mara kwa mara huku akiitupia lawama Seriklai kwa kushindwa kuweka matuta katika eneo hilo.

Hili ni tukio la pili kutokea kwa kipindi cha miezi mitatu kwa wananchi kupambana na polisi baada ya watoto kugongwa wakishinikiza barababa hiyo kuwekwa matuta.

Daktari kiongozi wa Hospitali Teule ya Wilaya, Daniel Simpa alithibitisha kuupokea mwili wa mtoto Happiness Filbert huku mwenzie akiwa amejeruhiwa na anaendelea na matibabu.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Julio achana na SImba njoo Mwadui Fc

Kocha wa zamani wa Simba, Jamhuri Kihwelo Julio ambaye yupo kwenye mipango ya kufundisha timu ya Mwadui FC.

KOCHA msaidizi wa zamani wa Simba, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, ameitwa katika kuinoa timu ya Mwadui FC inayoshiriki ligi daraja la kwanza, huku akisubiriwa kwa hamu kuona timu hiyo inapata tiketi ya kucheza Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
Habari zilizotufikia katika chumba chetu cha habari zinasema kuwa tayari Julio ameshawasili katika timu hiyo kwa ajili ya kuanza taratibu za kuinoa timu hiyo.

Julio alikuwa kocha msaidizi wa Simba, hata hivyo alienguliwa akiwa sambamba na kocha wake mkuu, King Abdallah Kibadeni, jambo linalomuumiza kichwa hadi leo.

Akizungumza kwa njia ya simu, Julio alisema kuwa ni mapema mno kuelezea maisha yake ya soka, ikiwa ni miezi michache tangu alipoenguliwa Simba kwa mizengwe.

“Naomba wadau wasiwe na haraka na mimi katika maisha yangu ya soka ndani na nje ya nchi, maana kama hizo habari za mimi kuinoa Mwadui zitakuwapo, basi kila mmoja atajua.

“Ni kweli nipo mkoani Shinyanga kwa mambo yangu binafsi, ila si kuinoa timu hiyo ya Mwadui kwakuwa ni mapema mno kutolea ufafanuzi jambo kama hilo, ukizingatia kuwa bado nina uchungu wa kusimamishwa timu ya Simba kwa mizengwe,” alisema Julio.

Kwa mujibu wa mtoa habari wetu, Julio Mameanza kuridhishwa na kiwango cha wachezaji wake mbali ya kutoa suluhu ya pili katika mechi za ligi kuu Tanzania Bara.

35 wauawa CAR mapigano yakichacha

Rais mpya wa muda nchini CAR, Catherine Samba Panza

Kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu imesema kuwa watu 35 wameuawa katika mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Bangui katika kipindi cha siku tatu zilizopita

Msemaji wa kamati hiyo ya Red Cross mjini Bnagui ,Nadia Dibsy,amesema kuwa mji huo sasa unakumbwa na vita vibaya.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Associated Press, miili ilionekana ikiwa imekatakatwa kwa mapanga na kutapakaa kote.

Vita inasemekana vimekithiri huku wanajeshi 1,600 wa Ufaransa na wengine 5,000 wa Muungano wa Afrika wakiwa nchini humo kujaribu kutuliza hali.

Mgogoro wa kisiasa ulianza mwezi Machi mwaka jana kutokana na mapinduzi ya kijeshi yaliyotokea wakati huo ambapo waasi waisilamu walimsaidia aliyekua Rais Djotodia kuingia mamlakani kwa nguvu.

Tangu hapo vita vimekuwa vikichacha kati ya waasi waisilamu na wakristo.

Na sasa kwa kuwa waisilamu wameondoka mamlakani, wakristo nao wameanza kulipiza kisasi.

Tanzania yajibu madai ya News of Rwanda.

Rais Jakaya Kikwete akitoa hotuba baada ya kuapishwa kwa muhula wa pili.

Ubalozi wa Tanzania nchini Rwanda umeeleza kusikitishwa na taarifa za blog ya Rwanda “News of Rwanda” ambayo inaunga mkono serikali ya nchi hiyo iliyotolewa mwishoni mwa juma zikimtuhumu rais wa Tanzania Jakaya Kikwete kwa kuunga mkono na kufanya mikutano na wanachama wa makundi ya waasi yanayopingana na serikali ya Rwanda.

Akizungumza na Sauti ya Amerika mkurugenzi wa mawasiliano ya Ikulu ya Tanzania Salva Rweyemamu amesema wao wameshangazwa kwa sababu mwaka jana kulikuwa na matatizo na marais wa nchi hizo wameshazungumza vizuri wakakubaliana na kuonyesha kwamba sasa mambo yameisha na kwamba wanaendeleza urafiki wao, udugu wao na ujirani mwema wa miaka mingi kati yao na kuongeza kwamba hilo ni jambo la kusikitisha sana kwa upande wa Tanzania .

Ametoa wito kwa vyombo vya habari nchini humo visaidie kujenga uhusiano mwema na visiwe mwanzo wa choko choko ya kugombanisha watu akiuliza kuwa “Tanzania wakigombana na Rwanda magazeti yatauzwa?” au mkiwa kwenye hali ya vurugu kama ilivyo nchi zingine ambapo watu wanapigana kila siku kuna watu wananunua magazeti pale?

Hofu baada ya mashambulizi Nigeria

Jeshi la Nigeria limekuwa likipambana na Boko Haram wanaowashambulia watu kiholela

Maafisa wa utawala nchini Nigeria wanasema kuwa zaidi ya watu elfu mbili wametoroka makwao baada ya watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa kiisilamu kushambulia kijji kimoja Kaskazini mwa nchi.

Watu hamsini na wawili waliuawa katika kijiji cha Kawuri kilicho katika jimbo la Borno siku ya Jumapili.

Shambulizi hilo limesemekana kusababishwa na kundi la wanamgambo la Boko Haram.

Zaidi ya watu 30 pia waliuawa siku hiyo hiyo wakatio ambapo kanisa liliposhambuliwa katika jimbo jirani la Adamawa

AU kujadili Sudan Kusini na CAR mjini Addis Ababa,Ethiopia

waziri mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn (L) na mwenyekiti wa AU Nkosazana Dlamini-Zuma mjini Addis Ababa

Wanachama 54 wa Umoja wa Afrika wanaanza kikao muhimu nchini Ethiopia alhamisi huku wakuu wa nchi wakikabiliwa na shinikizo la kusaidia kumaliza mapigano na ongezeko la mizozo ya kibinadamu katika nchi za Sudan Kusini na Jamhuri ya Afrika ya kati-CAR.

Kabla ya ufunguzi rasmi baraza la amani na usalama la AU jumatano usiku lilikutana mjini Addis Ababa kupokea ripoti kutoka nchi zote pamoja na ripoti tofauti kuhusu mzozo wa kisiasa wa nchini Misri. Bado haiko bayana hata hivyo nchi wanachama wanaweza kufanya nini kusuluhisha mizozo.

Wiki iliyopita, pande zinazopigana huko Sudan Kusini zilitia saini sitisho tete la mapigano lakini mashahidi wanasema mapambano kati ya majeshi ya serikali na waasi yanaendelea. Maelfu ya watu wameuawa na takriban raia 800,000 wamelazimika kuondoka kwenye makazi yao tangu mapigano yazuke mwezi uliopita. wachambuzi pia wanaonya kwamba serikali ya Juba huenda ikawa haina uwezo wa kuzima ghasia.
Waasi wa kundi la Seleka huko CARWaasi wa kundi la Seleka huko CAR
AU pia itakuwa mwenyeji wa mkutano wa wafadhili siku ya jumamosi kuchangisha fedha kwa ajili ya misaada ya kibinadamu na operesheni za ulinzi wa amani huko Jamhuri ya Afrika ya kati-CAR.

Ghasia huko Sudan Kusini zilianza kati kati ya Disemba baada ya Rais Salva Kiir kumshutumu Makamu Rais wa zazmani Riek Machar kwa jaribio la mapinduzi dai ambalo Machar amelikanusha. Umoja wa Mataifa unasema raia 100,000 wamekimbilia nchi jirani.

Jamhuri ya Afrika ya kati imetumbukia katika ghasia mwishoni mwa mwaka jana baada ya waasi kumuangusha Rais Francois Bozize.

Zaidi ya watu 1,000 wanakhofiwa wameuawa tangu ghasia ziongezeke mjini Bangui mapema mwezi Disemba. Wafanyakazi wa misaada wa Umoja wa Mataifa wanakadiria kuwa zaidi ya watu 900,000 wamelazimika kuondoka makwao.

IGAD:Waangalizi kwenda S. Kusini

Wanajeshi wa Sudan Kusini

Shirika la kikanda la IGAD la mataifa yaliyo katika upembe mwa Afrika, limeamua kuwa waangalizi wanapaswa kwenda nchini Sudan Kusini kuhakikisha kuwa mkataba wa kusitisha mapiganop unatekelezwa.

Uamuzi ulifikiwa katika mkutano wa Muungano wa Afrika unaondelea mjini Addisa Ababa Ethiopia.

Makabiliano makali yameendelea kuripotiwa nchini humo, licha ya mkataba wa amani kutiwa saini wiki jana kati ya waasi na serikali.

IGAD pia imetoa wito wa kuondolewa kwa wanajeshi wote wa kigeni nchini humo.

Hata hivyo, waziri wa mambo ya nje wa Uganda, Sam Kutesa, amesema kuwa Uganda haina mipango ya kuondoa wanajeshi wake ambao wamekuwa wakisaidia majeshi ya Sudan Kusini kupambana na waasi nchini humo.

DK slaa ndege ya kikwete tutaiuza

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Willbrod Slaa, amesema chama chake kikiingia madarakani mwaka 2015 kipaumbele cha kwanza kitakuwa ni kuuza ndege ya rais ambayo inatumiwa na Rais Jakaya Kikwete, ili kutatua changamoto zinazowakabili wananchi.
Katibu huyo alisema hayo juzi wakati akihutubia wananchi wa Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa mikutano ya M4C Operesheni Pamoja Daima.
"Kipaumbele kingine ambacho kipo katika ilani ya chama chetu ni kuhakikisha tunauza ndege ya Rais ya sasa iliyopo na kununua ndege itakayokuwa na uwezo wa kutua kila sehemu," alisisitiza Dkt. Slaa.
Alisema hatua hiyo inalenga kutatua changamoto zinazowakabili katika maeneo mbalimbali.
Katika hatua nyingine, Dkt. Slaa alisema mishahara ya askari wenye vyeo vidogo ni midogo, hivyo haiwezi kukidhi mahitaji yao.
Alisisitiza kuwa mishahara ya askari hao imekuwa midogo sana kulingana na kazi wanazozifanya, huku posho zao za kila wiki zikiwa hazikidhi mahitaji yao kutokana na kuwa ndogo hali inayosababisha askari hao kushiriki vitendo vya rushwa.
Alisema jeshi la polisi limekuwa likijihusisha na vitendo vya rushwa kwa kuwakamata wauza gongo, pamoja na watu wenye dawa za kulevya kutokana na mishahara yao kuwa ya chini.
Alimtaka Mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP, Ernesti Mangu, kuhakikisha askari hao wanaachana na vitendo vya rushwa kwa kuwaongezea mishahara, pamoja na kuacha tabia ya kutumia kauli za kijeshi.
Aidha, Dkt. Slaa alibainisha kuwa Tanzania inakabiliwa na janga la kuwa na vijana wengi wa mitaani hali inayohatarisha maisha ya wananchi wengine kutokana na vijana hao kutokuwa na kazi yoyote, huku akilaumu Serikali kwa kushindwa kutatua kero hiyo.

Malecela amchambua Lowasa

MAKAMU Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Taifa, John Samwel Malecela, ameitaka Sekretarieti ya chama hicho kuchukua hatua za haraka dhidi ya wanachama wanaoharibu misingi ya chama hicho kwa kutumia fedha zao hadharani kwa lengo la kutafuta umaarufu na ushawishi kwa vijana katika harakati za kugombea urais mwaka 2015.
Ushauri huo ulitolewa jana mjini hapa na Malecela wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mbio za urais ndani ya chama hicho wakati muda ukiwa bado.
Malecela alisema kuwa wanachama wa chama hicho wamekuwa njia panda, huku wakitamani kujua tamko au karipio la chama juu ya suala hilo la harakati za urais mwaka 2015 bila mafanikio.
Alisema ni lazima Sekretarieti ya chama ibadilike na kuchukua hatua mara moja ili kuleta imani kwa wanachama wake.
“Ninaomba niseme bila kuwa na karipio au tamko hawa wanaotumia fedha zao hadharani kwa lengo la kutafuta umaarufu na ushawishi kwa vijana ili kupata madaraka wanaharibu misingi yetu bora ya uongozi iliyowekwa na waasisi wetu ndani ya chama,” alisema Malecela.
Aliongeza kuwa kipindi cha nyuma viongozi wa chama hicho hawakuongozwa na fedha kutafuta madaraka, bali nidhamu, busara na uchungu wa rasilimali za taifa.
"Hivyo, ndivyo vilivyowezesha kuongoza taifa ikiwa ni pamoja na kufuata misingi na maadili ya uongozi ndani ya chama na serikali," alisema na kuongeza kuwa;
"Viongozi wa zamani wamekuwa wakiumia sana kuona chama kinataka kutekwa na wenye fedha kwa uchu wa madaraka hali inayowafanya kujiuliza wanakopata fedha hizo pamoja na masilahi ya madaraka wanayotaka kununua ni ya nani, wakati Watanzania wakiendelea kuwa masikini."
Malecela alisisitiza kuwa; “Tunaumia sana kuona chama sasa kinataka kutekwa na wenye fedha kwa uchu wa madaraka hadi tunashangaa na kujiuliza hizi fedha wanazipata wapi.
Madaraka wanayotaka kwa kununua ni kwa masilahi ya nani huku Watanzania wakiendelea kuwa maskini?”
Malecela alipongeza juhudi za Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Paul Makonda, na kusema kuwa anamuunga mkono kwa kitendo chake cha kumkemea Mbunge wa Monduli,Edward Lowassa, kwa kukiuka misingi ya katiba ya chama na kuvuruga chama kwa lengo la kutaka urais mwaka 2015.
“Nadiriki kusema nampongeza na kumuunga mkono kijana huyu (Makonda) kwa kauli zake nzito na za kijasiri kwa masilahi ya CCM kwa kuweza kumkemea, Lowassa, bila kujali cheo na umaarufu wake kwa jinsi anavyokivuruga chama chetu kwa lengo la kutaka urais mwaka 2015, huku Sekretarieti ya chama ikiwa imekaa kimya wakati inajua muda wa kuanza mbio hizo bado na kufanya hivi kwa sasa ni kukiuka misingi ya katiba ya chama,” alisema Malecela.
Alibainisha kuwa anasikitishwa kuona juhudi za uongozi wa sasa wa chama ngazi ya juu ikiwa ni pamoja na Sekretarieti inayoongozwa na Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana na Katibu wake Nape Nnauye za kutetea chama hicho zikibezwa na baadhi ya watu wenye lengo la kutaka kuharibu chama.
Wakati huo huo, Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, ameishukia UVCCM kwa kuwahusisha viongozi wa dini na mbio za urais wa mwaka 2015.
Akizungumza na Waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Shekhe Salum, alisema kuwa kauli iliyotolewa na Makonda imewagusa hivyo ni lazima aijibu.
Alisema ikizingatiwa kuwa yeye ni Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, hawatujui Makonda amewahusishaje viongozi wa dini na mambo ya kampeni za urais mwaka 2015 hazijaanza na hakuna hata mtu mmoja aliyetangaza kugombea nafasi hiyo.
"Wasiwasi wa kumuogopa Lowassa unatoka wapi? Kama yeye anawajua wanaogombea urais kuwaambia Watanzania kuwa huyo hafai mbona hatuambii anayefaa ni nani?" alihoji.
Alihoji ni wapi Makonda amepata kazi ya kuwachagulia Watanzania Rais anayefaa amepewa na nani? aliendelea kusema; "Kosa la viongozi wa dini ni nini, maana kama kualikwa kwenye makanisa au misikiti kufanya harambee mbalimbali wanasiasa wote wanaotajwa kuwa wanaweza kugombea urais wanaalikwa, kwa nini viongozi wa dini walaumiwe kwa ajili ya Lowassa?."
Alisemaa namkumbusha Makonda kuwa, Lowassa amekuwa kiongozi katika awamu zote za utawala wa nchi hii, hivyo anaposema hafai ina maana yeye anamjua zaidi kuliko marais wote.
Katika hatua nyingine, Shekhe Salum alisema kuwa kushambuliwa kwa Mawaziri na kuwaita Mizigo ni ukosefu wa maadili na huko ni kumtukana aliyewateua.
Alisema wanaamini kuwa Rais hakukurupuka kufanya uteuzi huo, lakini hao wanaowakashfu mawaziri ambao pia ni wabunge kuwa mizigo wao wanao uwezo wa kumfikia yule aliyewateua na wanajua kuwa anaweza akabadilisha uteuzi huo, hivyo wangemshauri mwenyekiti wao wa taifa (Rais Jakaya Kikwete) ili awawajibishe badala ya kuwakashfu kupitia vyombo vya habari.
Juzi Makonda, alimshukia Lowassa akimtuhumu kutumia watu kukigawa chama na watu kwa ajili ya tamaa ya urais mwaka 2015. Hata hivyo, kauli hiyo ya makonda imepokewa kwa hisia tofauti na kuzidisha malumbano ya kisiasa ndani ya chama hicho.

Chadema kususia Bunge la Katiba

Mjumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la chama cha CUF, Ismail Jussa Ladhu akihutubia kwenye mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Uwakilishi Jimbo la Kiembesamaki alipokuwa akimnadi mgombea wa chama hicho Abdulmalk Haji Jecha, uliofanyika kwenye Uwanja wa Kiembesamaki, mjini Magharibi, kisiwani Unguja.

Morogoro/Zanzibar. Wakati Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akisema wabunge wa chama chake watasusia vikao vya Bunge Maalumu la Katiba ikiwa hoja ya kuundwa kwa Serikali tatu itapingwa na wabunge wa CCM, Mwakilishi wa Mji Mkongwe (CUF), Ismail Jussa Ladhu ametaka kuvunjwa kwa Muungano.

Akihutubia kwenye Uwanja wa Tubuyu nje kidogo ya Mji wa Morogoro juzi, Mbowe alisema wabunge wa chama chake wataandamana nchi nzima kufikisha ujumbe kwa wananchi kwamba maoni yao yamepingwa na wabunge wa CCM walio wengi.

“Tutawaeleza wananchi kwamba maoni ya CCM ndiyo yameonekana ya maana kuliko ya wananchi ambao ni wengi zaidi,” alisema Mbowe kwenye mkutano huo ambao ni sehemu ya Operesheni ya Vuguvugu la Mabadiliko - M4C Pamoja Daima.

Alisema Tume ya Mabadiliko ya Katiba ilikusanya maoni na kubaini kuwa asilimia 62 ya Watanzania wanataka Serikali tatu za Tanganyika, Zanzibar na ya Muungano.

“Serikali ya CCM haitaki kusikia maneno Serikali tatu wanasema sera yao ni ya Serikali mbili, wanafanya kila hila ili kuikataa hoja hiyo. Natangaza kwamba wakifanya hivyo tutasusia na kwenda kuwashtaki kwa wananchi,” alisema Mbowe.

Aliongeza kwamba wataandamana kuanzia Kagera hadi Mtwara kuwaeleza wananchi kwamba hoja yao imepingwa na CCM.

Mbowe alisema baadhi ya viongozi wa CCM wamekuwa wakitoa kashfa dhidi ya Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba kwamba amechukua maoni ya Chadema.

“Wanakosea hayo si maoni ya Chadema, bali ni maoni ya wananchi, Warioba amezingatia maoni ya wananchi,” alisema.

Mwenyekiti huyo alisema Katiba inayotafutwa si ya chama, bali ni ya Watanzania na kwamba inashangaza CCM kuipinga hoja Serikali tatu.

“Tunafahamu wanaogopa kuikubali hoja ya Serikali tatu kwa sababu wanafahamu huo ndiyo utakuwa mwisho wao wa kuwa madarakani,” alisema Mbowe huku akishangiliwa na wafuasi wa chama hicho.

Alisema CCM wanaelewa kwamba kukiwa na Serikali tatu, Chadema kitashinda Tanganyika na CUF Zanzibar katika uchaguzi wowote utakaoitishwa.

“Kwa hiyo hivi sasa wana wasiwasi kweli, wanatafuta kila njia ya kuichakachua hoja ya Serikali tatu lakini wafahamu kuwa Chadema wanaifuatilia hoja hiyo kwa ukaribu,” alisema
Aliwataka wananchi kufuatilia Bunge Maalumu la Katiba litakapoanza mwezi ujao ili kuangalia wabunge wao wanavyowawalisha katika suala hilo muhimu.

Hata hivyo, Mbowe alisema chama hicho kikishinda katika uchaguzi wa mwaka 2015 hakitahangaika kulipa kisasi kwa kuwachukulia hatua za kisheria viongozi, bali kitajikita kutafuta maendeleo.

“Wasituogope tutasamehe kama alivyosamehe aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini, Nelson Mandela. Hatutalipa kisasi tukiingia Ikulu, kwa sababu hakuna binadamu asiye na makosa. Tutaelekeza nguvu zetu kuwaletea maendeleo Watanzania,” alisema Mbowe.

Jussa na Muungano

Akihutubia mkutano wa kampeni katika Jimbo la Kiembesamaki jana, Jussa alisema hakutakuwa na maendeleo yatakayofikiwa Zanzibar ikiwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar hautang’oka.

Jussa ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza Kuu la Taifa la CUF, alisema Zanzibar yenye watu milioni 1.5 haiwezi kuwa na tatizo la watu kukosa ajira lakini sera na mipango ya kiuchumi imekuwa ikikwama katika utekelezaji wake kutokana na kukosa mamlaka kamili.

Alisema Zanzibar haiwezi kukopa katika taasisi za kimataifa bila ya kuwekewa dhamana na Waziri wa Fedha wa Muungano wakati Zanzibar ni nchi na kuwataka wananchi kutumia kura zao katika Uchaguzi Mkuu wa 2015 kuleta mabadiliko ya kiutawala.

“Hakuna sababu ya vijana Zanzibar kukosa ajira, kuna watu wasiozidi milioni 1.5, Muungano umefika wakati ung’oke, ndiyo kikwazo cha maendeleo ya Zanzibar na watu wake kiuchumi na kisiasa,” alisema Jussa.

Alisema mradi wowote unaobuniwa Zanzibar hauwezi kupata mfadhili bila kuwekewa dhamana na Serikali ya Muungano na kukwama kwa juhudi zote za kujiunga na jumuiya za kimataifa akitolea mfano Jumuiya ya Kimataifa ya Kiislamu (OIC).

Alisema Rais wa Zanzibar amepoteza mambo muhimu chini ya mfumo wa Muungano ikiwa ni pamoja na kutopigiwa mizinga 21 akiwa nje ya nchi, kupeperusha bendera ya Zanzibar, kutokagua gwaride na kupigiwa wimbo wa Taifa la Zanzibar.

“Haya ya sasa si mamlaka kamili, wapi Dk Shein alikokwenda akapigiwa mizinga 21 au alipeperushwa wapi bendera ya Zanzibar wakati wa safari zake za nje?” alihoji Jussa.

Mbunge, Mkurugenzi nusura wazichape

Mbunge wa Viti Maalumu wa Chadema wa Mkoa wa Manyara, Paulina Gekul jana alilazimika kuokolewa na polisi wilayani hapa, kutokana na kushambuliwa na Mkurugenzi wa Halmashari ya Mji wa Babati, Omari Mkombole na Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Mohamedi Fara, wakigombea kabrasha lenye majina ya wanaopaswa kupewa ardhi.

Katika tukio hilo, Gekul ameeleza kuchaniwa nguo zake, kudhalilishwa na kuporwa fedha zaidi ya Sh5 milioni zilizokuwa kwenye mkoba wake.

Tukio hilo la kushambuliwa kwa mbunge huyo lilitokea juzi saa 12 jioni katika ukumbi wa halmashauri ya mji wa Babati, mara baada ya kikao kilichokuwa kikifanyika chini ya mkurungenzi huyo kumalizika.

Akizungumza mara baada ya kutoka polisi jana kutoa maelezo juu ya vurugu hizo, Gekul alisema kikao hicho kilichosababisha vurugu hizo, kilikuwa kinajadili mustakabali wa ugawaji wa shamba la Sisal Plantation lenye ekari 4200.

Alisema shamba hilo wakulima walilipia mwaka 2000 na Baraza la Madiwani lilikwishatoa uamuzi wa kugawanywa, lakini juzi katika orodha iliyotolewa, alibaini majina mengi yameghushiwa na walengwa wengi hawapo na baada ya viongozi wa halmashauri kubaini amegundua njama hizo, ndipo waliagiza kurejeshwa makabrasha yote.

“Mimi nilikataa kwa sababu orodha hii ina makosa na mimi nawafahamu baadhi ya wakulima wanaopaswa kupewa eneo hili “alisema Gekul.

Alisema Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Mohammedi Fara

baada ya yeye kukataa kurejesha, aliahirisha kikao na walipotaka kutoka nje ghafla alitokea Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Omari Mkombole ambaye alidai alikwenda Polisi kufuatilia suala la wakulima hao na tayari wanataka kuendesha msako wa waliovamia eneo hilo bila idhini ya halmashauri.

“Lakini cha ajabu baada ya kusema hivyo, mkurugenzi huyu akanifuata na kunikaba kwa nguvu, kisha kunichania nguo zangu na kunipokonya karatasi akidhani zina majina ya wakulima hao,

Alisema baada ya mlango kufungwa alianza kupokonywa kwa nguvu pochi yake na wakachambua ndani na kuondoka na nyaraka zote, huku ufunguo wa gari ukitupwa.

Mkurugenzi wa Halmashauri Omari Mkombole, alipopigiwa simu ya mkononi ili kuzungumzia tukio hilo, hakupokea na simu yake iliita bila kupokewa, huku Mwenyekiti wa Halmashauri akikiri kutokea kwa vurugu hizo.

Thursday 30 January 2014

Balotel alimwa fain

MSHAMBULIAJI wa AC Milan, Mario Balotelli, amepigwa faini ya pauni 8,200 kwa kuwaoneshea ishara mashabiki wa Cagliari baada ya kufunga katika ushindi wao wa mabao 2-1 Jumapili.
Balotelli (23) alipewa kadi ya njano kwa kuonesha kitendo kisicho cha uanamichezo baada ya kusawazisha dakika ya 87.
Kwa mujibu wa BBC, hiyo ilikuwa kadi yake ya njano ya nane ya msimu, ambayo inamaanisha hatacheza mchezo wa Jumamosi dhidi ya Torino.
Balotelli alitolewa nje ya uwanja mapema msimu huu kwa kuwatukana waamuzi mwisho wa mchezo dhidi ya Napoli.
"Balotelli atajifunza," kocha wa Italia, Cesare Prandelli, alisema mapema juzi.
"Atahitaji upendo mwingi, ni mtu anayeifanyia mengi Milan na muhimu kwa timu hiyo," alisema Prandelli.

Matamshi kuhusu ubakaji yakera India

wanawake wanao vaa nguo fupi

Matamshi ya mwanasiasa mmoja mwanamke nchini India kuhusu ubakaji yamelaaniwa na watu wengi kote nchini humo.

Asha Mirge, ambaye ni mwanachama wa kikundi cha viongozi wanawake serikalini katika jimbo la Maharastra, amesema kuwa wanawake pia wanachangia pakubwa kwa wao wenyewe kubakwa kutokana na mavazi pamoja na wanavyotembea na hata kuzungumza.

Amehoji kwa nini wanawake hutoka nje nyakati za usiku.

Matamshi haya yaliyozua gumzo katika vyombo vya habari kote nchini India, yamesababisha kero kubwa kutoka kwa makundi ya wanaharakati wa maswala ya wanawake na wanasiasa wengine.

Bi Mirge hata hivyo ameomba radhi kwa matamshi yake akisema yametiwa chumvi.

Inda imekuwa ikimbwa na visa vya mara kwa mara vya ubakaji kiasi cha serikali kubuni sharia kali dhidi ya wabakaji.

Ni wiki jana tu ambapo wazee wa kijiji waliamrisha kubakwa kwa mwanamke ambaye alikuwa na uhusianao wa kimapenzi na mwanamume ambaye sio wa kutoka jamii moja naye.

Operesheni Tokomeza yaburuta 516 kortini

OPERESHENI Tokomeza iliyoendeshwa na Serikali kusaka watu waliokuwa wakijihusisha na vitendo vya ujangili imeweza kufikisha mashauri 516 yaliyofunguliwa katika mahakama mbalimbali nchini.
Hayo yalisemwa Dar es Salaam jana na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Othuman Chande, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na maadhimisho ya Siku ya Sheria Duniani ambayo yatafanyika Februari 3, mwaka huu.
Alisema mashauri 516 yalifunguliwa katika mahakama mbalimbali kutokana na Operesheni Tokomeza ujangili iliyoanza Oktoba 4, mwaka jana hadi ilipositishwa Novemba Mosi, mwaka jana.
Alisema kuwa Mahakama ilipokea kesi 516 zilizohusika na Oparesheni Tokomeza ujangili ambapo mpaka sasa kesi 198 zimeshasikilizwa na kumalizika wakati wa operesheni.
Alisema kuwa katika kesi hizo mashauri yaliyofunguliwa chini ya sheria mbalimbali, sheria ya uhujumu uchumi sura ya 200 iliyorejeshwa mwaka 2002, sheria ya hifadhi ya wanyamapori sura ya 283, sheria ya mbuga za Taifa sura 282, sheria ya silaha na risasi sura 223, sheria ya misitu sura ya 323 na sheria ya makosa ya jinai sura ya 16 na sheria ya kifo sura ya 24.
Hata hivyo alisema Mahakama za Hakimu Mkazi sita na Mahakama za Wilaya 19, zilihusika na kesi hizo ambapo kesi zilizosikilizwa na kumalizika wakati wa operesheni ni 198 sawa na asilimia 38.37.
Alisema vitendo vya wananchi kujichukulia sheria mkononi na kuchoma Mahakama za mwanzo zimesababisha watu wengi kukosa haki yao ya msingi kutokana na majalada ya kesi kuungua.
Alisema kuwa kuanzia mwaka 2012 yamekuwapo matukio mbalimbali ya uchomaji moto majengo ya Mahakama za Mwanzo nchini na matukio hayo ni yale yaliyotokea Mahakama ya Mwanzo Mtwara Mjini, Mikindani, Lisekese na Mahakama ya Mwanzo Wanging'ombe katika mkoa wa Iringa.
"Januari 25, mwaka 2013 Mahakama ya Mwanzo Mtwara mjini ilichomwa moto na wananchi katika vurugu zilizotokea siku hiyo mjini Mtwara wakati wa mzozo wa rasilimali gesi na kusababisha jengo na majalada yote kuteketea kwa moto," alisema.
Alisema kutokana na matukio ya kuchomwa moto kwa mahakama za mwanzo kumesababisha wananchi wengi kukosa haki zao za msingi kutokana na kupotea kwa vielelezo muhimu pamoja na ushahidi.
Aliongeza kuharibiwa kwa majalada ya kesi kumesababisha kesi nyingi kusimama au kutoendelea kabisa katika baadhi ya mahakama na kuchangia wananchi kukosa haki.
Alisema kwa mwaka huu wa fedha 2013/2014 mahakama ya Tanzania imepanga kujenga majengo mapya 25 kwa ajili ya mahakama za mwanzo na kukarabati majengo mengine 10.
Hata hivyo, alisema kitendo cha wananchi kujichukulia sheria mkononi si kizuri kwani hawawezi kujenga mahakama eneo ambalo ilikuwepo lakini ikaunguzwa na wananchi wenye hasira. Pia alisema kuwa takwimu za mahitaji ya majengo ya mahakama za mwanzo nchini ni zaidi ya majengo 296 mapya na mengi mengine yanahitaji ukarabati.

Jaribio la kumuua waziri Libya latibuka

Kumekuwa na jaribio lililotibuka la kumuua kaimu waziri wa ndani nchini Libya Al-Sidik Abdel-Karim.

Shirika la kitaifa la habari LANA na lile la AFP yamethibitisha tukio. Inaarifiwa kwamba gari alimokuwa Abdel Karim lilipigwa risasi alipokuwa akielekea katika mkutano katika makao makuu ya bunge.

Abdel-Karim anatarajiwa kuhutubia waandishi habari hivi punde.

Abdel Karim aliteuliwa na waziri mkuu nchini Libya kuwa kaimu waziri wa ndani baada ya waziri Mohamed Sheikh kujiuzulu mnamo Agosti mwaka jana.

Seddik Abdelkarim, alikuwa katika gari lake aliposhambuliwa na watu wasiojulikana waliomfyatulia risasi. Inaarifiwa hakuna aliyeuawa kwenye shambulizi hilo.

Libya imekuwa ikikabiliwa na hali ngumu ya kisiasa tangu waasi kuipindua serikali na kumuua aliyekuwa Rais Muamer Kadhafi mwaka 2011.

Waziri huyo alikuwa njiani kuelekea bungeni wakati gari lake liliposhambuliwa.

Shambulizi lenyewe limetokea chini ya wiki tatu baada ya mauaji ya naibu waziri wa viwanda Hassan al-Droui, aliyeuawa mjini Sirte

Uingereza yapokea wakimbizi toka Syria

Maisha ni magumu kwa wakimbizi nchini Syria

Uingereza imesema kuwa itatoa hifadhi ya muda kwa mamia kadhaa ya wakimbizi wa Syria ambao wanakabiliwa na hali mbaya zaidi ya maisha.

Naibu waziri mkuu, Nick Clegg, amesema kuwa serikali ya muungano itatoa fursa ya kwanza kwa wanawake wanaokabiliwa na hatari ya kubakwa, wale waliobakwa tayari, wazee na watu wanaoishi na ulemavu.
Shirika la umoja wa mataifa kuhusu wakimbizi UNHCR, ambalo limetowa wito kwa mataifa ya magharibi kutoa hifadhi kwa wakimbizi alfu thelathini kutoka Syria, limechangamkia tangazo hilo la Uingereza.

Mwakilishi wa shirika hilo nchini Uingereza amesema ni jambo la kutia moyo na hatua muhimu ambayo itasaidia kutoa suluhu zinazohitajika kwa wakimbiizi ambao wameathirika na kukabiliwa na hali ngumu ya maisha.
Hadi kufikia sasa serikali ya Uingereza imekataa kuwapokea wakimbizi ikisisitiza badala yake, kwamba inatoa msaada wa karibu dola bilioni moja.

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu Amnesty International, limekosoa vikali viongozi wa ulaya ambao walitoa ahadi ya kuwapokea wakimbizi alfu kumi na nne pekee, wakati mataifa jirani na Syria yanahifadhi karibu wakimbizi milioni mbili.

Kenya matatani kukumbwa na njaa

Serikali ya Kenya imetoa tahadhari kuhusu tisho la nja kwa watu milioni 1.6 kutokana na uhaba wa chakula.

Wizara ya kilimo imesema kuwa chakula kilichohifadhiwa kwa sasa kinaweza kudumu tu hadi mwezi Mei.

Wafanyabiashara wa sekta binafsi wametakiwa kuingilia kati na kununua chakula zaidi kutoka nje ili kuokoa hali.

Hii leo serikali imetoa tahadhari kuhusu uhaba wa chakula lakini wiki jana halmashauri ya serikali ya kukabiliana na ukame ilitoa tahadhari kwa serikali kuhusu tisho la ukame.

Baadhi ya maeneo yaliyoathirika kutokana na ukame ni maeneo ya Mashariki ambako mvua haijanyesha kwa muda mrefu.

Mkuu wa halmashauri hiyo aliitaka serikali kuchukua hatua mwafaka ili kuzuia ukame na janga la njaa ambalo liliwahi kushuhudiwa nchini humo miaka kadhaa iliyopita.

Katika eneo la Turkana Kaskazini mwa Kenya ambako jamii za kuhamahama huishi, hali inasemekana kuwa mbaya zaidi.

Kuna ripoti za watu kukabiliwa na njaa pamoja na ukame. Mtoto mmoja aliripotiwa kufariki kutokana na njaa

Inaarifiwa watu kadhaaa wamelazwa hospitalini kutokana na utapia mlo huku familia moja ikilazimika hata kupika nyama ya Mbwa kutokana na ukosefu wa chakula.

Tambwe akata tamaa kuwa mfungaji bora

Mshambuliaji wa Simba, Amisi Tambwe amesema itamwia vigumu kuibuka kinara wa upachikaji mabao kama waamuzi wataendelea kuchezesha vibaya kwenye Ligi Kuu Bara.

Tambwe alisema hayo baada ya mwamuzi Andrew Shamba wa Pwani kukataa mabao yake mawili kwa madai alifanya makosa kabla ya kufunga.

Mshambuliaji huyo raia wa Burundi alifunga mabao hayo wakati wa mchezo wa Ligi Kuu kati ya Simba na Rhino Rangers uliopigwa mwishoni wiki kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Akizungumza na gazeti hili, Tambwe alisema mwamuzi Shamba hakuwa sahihi kukataa mabao yake kwa sababu hayakuwa na matatizo yoyote.

“Binafsi naamini mabao niliyofunga yalikuwa halali kabisa ingawa mwamuzi alikataa, sisemi kama aliwapendelea wapinzani, lakini inawezekana hana uwezo.

“Hofu niliyonayo ni kama waamuzi wa aina hii wataendelea kupewa nafasi ya kuchezesha itakuwa vigumu kwangu kutimiza malengo yangu ya kumaliza ligi nikiwa mfungaji bora,”alisema Tambwe.

Man city yashikilia usukani England

Mshambulizi Sergio Aguero wa Man City

Klabu ya Manchester City imechupa hadi kileleni mwa ligi kuu ya soka nchini England baana ya kuonesha soka safi dhidi ya klabu ya Tottenham katika uga wa White Hart Lane.

Kikosi cha kocha Manuel Pellegrini kilihitaji ushindi dhidi ya Spurs ili kuwapiku Arsenal kwenye jedwali la msimamo wa ligi hiyo, na matumaini hayo yalianza kuonekana mapema wakati Aguero alipovuna bao la kwanza, hii ikiwa ni mara ya nane mfululizo akiifungia City katika mechi nane mfululizo.

Yaya Toure aliiweka Man City kifua mbele kwa bao la pili, dakika ya tano kipindi cha pili kupitia mkwaju wa penalti uliozua utata ambapo mlinda ngome wa Spurs Danny Rose alitimuliwa uwanja kwa kulishwa kadi nyekundu japo alionekana kuugusa mpira kwanza kabla ya kuadhibiwa kwa kumchezea rafu Edin Dzeko.

Dzeko aliongeza bao la tatu na ingawa Etienne Capoue alifunga bao la kufuta machozi kwa Spurs, bado kulikuwa na fursa kubwa kwa Man City kuendelea kuinyeshea Spurs mvua ya magoli kupitia mchezaji wa akiba Stevan Jovetic aliyefunga bao lake la kwanza katika ligi kuu tangu uhamisho wake wa pauni £22m kutoka klabu ya Fiorentina ya Italia.

Aguero afunga mabao 50

Baada ya mechi hiyo Sergio Aguero sasa ameandikisha rekodi ya kufunga takriban mabao 50 ya ligi kuu baada ya mechi 81, na kuibuka kuwa mtu wa tano kufunga kiasi hicho cha mabao, baada ya Andy Cole, Alan Shearer, Ruud van Nistelrooy na Fernando Torres.

Kisha City ikaongeza maumivu zaidi kwa Spurs baada ya kile kipigo cha mabao 6-0 mwezi November mwaka uliopita, pale Vincent Kompany alipokamilisha kibarua kwa kufunga bao la tano na la ushindi.

Chelsea 0 - 0 West Ham

Kwenye matokeo ya mechi nyinginezo Chelsea ilipata pigo kwenye harakati zake za kutafuta uongozi kwenye jedwali baada ya kulazimika kutoka sare ya kutofungana na West Ham katika uwanja wa nyumbani Stamford Bridge.
Kwingineko Aston Villa iliishinda West Brom mabao 4 - 3 nayo Sunderland ikainyuka Stoke 1-0.

Hii ndiyo orodha ya saba bora tarehe 30-01-2014:

1 Man City 53
2 Arsenal 52
3 Chelsea 50
4 Liverpool 46
5 Tottenham 43
6 Everton 42
7 Man Utd 40

Wednesday 29 January 2014

Sudan kusin ndo kumeiva sasa

Wanajeshi wa serikali ya Sudan Kusini na waasi bado wanaendelea na mapigano licha ya makubaliano ya wiki iliyopita ya kuweka chini silaha, huku kila upande ukitafuta kuchukua udhibiti wa miji mikuu nchini humo

Umoja wa Mataifa umesema idadi ya raia wanaotafuta hifadhi katika kambi zake nchini humo inazidi kupanda. Naibu wa msemaji wa umoja wa Mataifa Fahran Haq amewaambia waandishi wa habari kuwa kikosi cha kulinda amani cha umoja wa Mataifa kilichoko Sudan Kusini, UNMISS, kimeripoti kuzorota kwa hali ya usalama katika baadhi ya maeneo ya jimbo la Unity ambako kuna viwanda muhimu vya mafuta na mapigano ya mara kwa mara yameripotiwa kati ya wanajeshi na waasi wanaomuunga mkono aliyekuwa makamu wa Rais Riek Machar. Haq amesema idadi ya watu waliopewa hifadhi katika kambi za Umoja wa Mataifa kote nchini humo imeongezeka na kufikia watu 79,000 kutoka idadi ya awali ya 76,000. Nusu ya idadi hiyo iko kazika kambi mbili za Umoja wa Mataifa mjini Juba.

Raia wengi wa Sudan Kusini wanaendelea kutoroka nchini humo kutokana na hofu kwamba makubaliano ya kusitisha vita huenda yasitekelezwe. Huyu hapa ni mmoja wa raia wanaoishi katika kambi ya wakimbizi nchini Uganda. "Bado kuna dalili za kuendelea mapigano, licha ya muafaka wa kusitisha mapigano. Serikali haitaki kuwapa waasi nafasi yoyote, nao waasi wanataka madaraka, na watajaribu wawezavyo kujipanga upya na kushambulia. Kwa hivyo kuna hofu mapigano yanaweza kuanza tena"
Konflikt im Südsudan Flüchtlinge 17.01.2014

Takribani watu 47,000 wamepewa hifadhi nchini Uganda na msemaji wa Shirika la Kuwashughulikia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa nchini Uganda Lucy Beck anasema hali ni mbaya katika kambi hizo."Kufikia jana walikuwa karibu 197, lakini wale wanaowasili ni wanyonge baada ya kusafiri kwa muda mrefu bila pesa za kutosha. duru nchini Sudan Kusini zinasema kuna watu wengi ambao hawajafanikiwa kufika Uganda, au wangali njiani".

Mkuu wa shirika la misaada ya kibinadaaamu wa Umoja wa Mataifa Valerie Amos ambaye hapo jana alizuru mji wa Malakal amesema uhalifu wa kivita umefanyika Sudan Kusini na kuongeza kuwa watu aliozungumza nao wamepoteza kabisa imani na wanataka kuhamishwa hadi maeneo mengine nchini humo au hata katika nchi nyingine. Mashirika ya kutoa misaada nchini humo yamesema kiasi ya watu 10,000 wameuawa katika mzozo huo ulioanza tarehe 15 mwezi uliopita.

Na wakati hali ikiendelea kuwa tete nchini humo, Waziri wa sheria wa Sudan Kusini Paulino Wanawilla Unago amesema kuwa kiongozi wa waasi Riek Machar na wenzake sita wanastahili kushtakiwa kwa makosa ya uhaini kuhusiana na jukumu lao katika umwagaji damu uliofanywa nchini humo. Waziri huyo amesema wanasiasa wengine saba waliokamatwa baada ya vurugu kuzuka, wataachiliwa huru, ikiwa ni mojawapo ya masharti ya waasi katika meza ya mazungumzo.

Miongoni mwa wale waliowekwa kizuizini ni Pagan Amum, ambaye alikuwa katibu mkuu wa chama tawala, aliyekuwa waziri wa usalama wa taifa Oyai Deng Ajak, balozi wa zamani nchini Marekani Ezekiel Lol Gatkuoth na aliyekuwa naibu waziri wa ulinzi Majak D'Agoot.

Dk slaa ampa vidoge J k kuhusu safari zake za mara kwa mara

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willbrod Slaa, ameitaka Serikali kutoa kauli juu ya madai ya ufujwaji wa fedha kwenye safari za nje hasa zinazohusu msafara wa Rais Jakaya Kikwete, akisema zingeweza kusaidia kuboresha maisha ya wananchi wake, hususan watumishi.

Dk. Slaa amesema tangu Rais Kikwete aingie madarakani mwaka 2010, amefanya safari za nje ya nchi zipatazo 358, huku kila safari ikigharimu takribani milioni 500, akisema fedha hizo zingeweza kusaidia katika kuboresha hali ya watumishi nchini.

Akizungumza katika mfululizo wa mikutano ya chama hicho iliyopewa jina la M4C- Operesheni Pamoja Daima jana katika maeneo ya Uyovu (Bukombe), Kakola, Ushetu (Ubagwe, Nonwe) na Shinyanga mjini, Dk. Slaa aliitaka Serikali ya CCM kuacha anasa za matumizi ya fedha ambazo zingeweza kuboresha miradi ya maendeleo, zikiwemo huduma za jamii kama maji, elimu na afya.

Alisema ni jambo la kushangaza na la kusikitisha kuona Rais akitumia fedha nyingi kiasi hicho katika safari za nje tu, wakati wananchi na watumishi wake kila siku wanalia na maisha magumu.

“Serikali inaingia katika anasa ya kutumia fedha katika safari za nje, wakati wananchi ni maskini, watumishi wa umma nao wanalia na maisha magumu, wamepigika, vikongwe nao wanauliwa kwa sababu wana macho mekundu ambayo yanatokana na kutumia kuni kwa ajili ya kupikia, hii inasikitisha sana.”

“Serikali inasema hakuna fedha za kutosha za kuboresha maisha ya Watanzania na ya kuongeza mishahara ya watumishi wake ambao wanalia kila siku mishahara yao midogo, lakini eti fedha za safari za nje zenyewe zipo, ni jambo la kushangaza sana,” alisema Dk. Slaa.

Aliongeza kuwa safari za nje kwa kiongozi wa nchi zina umuhimu wake, lakini ni lazima masuala kadhaa, ikiwemo tija inayopatikana katika safari hizo na kuona kipaumbele cha matumizi hasa kuboresha maisha ya Watanzania kwanza, badala ya kutumia fedha nyingi katika safari hizo.

CHADEMA kinaendelea kufanya ziara zake hizo za M4C- Operesheni Pamoja Daima, ambapo jana Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dk. Slaa, walibadilishana maeneo ya ‘kushambulia’ ambapo Mbowe alitoka Geita kwenda Iringa, akiungana na Halima Mdee na Peter Msigwa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini na Kati, huku Dk. Slaa akitoka Iringa kwenda Geita kuendelea na mikoa ya Kanda ya Ziwa Mashariki na Magharibi.

Ziara za viongozi hao wa Chadema zimegawanyika katika makundi matatu, huku kaulimbiu ikiwa M4C- Pamoja Daima ambapo imebeba ajenda kadhaa ikiwa ni pamoja na mchakato wa Katiba Mpya, daftari la wapiga kura, rasilimali za nchi, kupanda kwa ugumu wa maisha, uchaguzi wa ndani wa chama hicho unaondelea katika ngazi ya msingi na uchaguzi mdogo wa madiwani katika kata 27 nchini.

Mchina akiona cha moto kenya

Mahakama nchini Kenya imemtoza faini ya shilingi milioni 20 au dola laki mbili na thelathini raia mmoja mchina kwa kuhusika na biashara haramu ya pembe za ndovu.

Adhabu hii inatokana na sheria kali za kudhibiti uwindaji wa wanyama pori.

Tang Yong Jian alikamatwa wiki jana akiwa na Pembe za Ndovu zenye kilo 3.4 katika sanduku lake katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta.

Ikiwa atashindwa kulipa faini hiyo huenda akafungwa miaka saba gerezani.

Kenya iliharamisha biashara ya pembe za Ndovu mwaka 1989, lakini kumekuwa na ongezeko la biashara hiyo haramu katika miaka ya hivi karibuni.

Kuna hitaji kubwa la pembe hizo barani Asia kwa matumizi ya mapambo huku wahifadhi wa mazingira wakishuku kuwa pembe za Vifaru hutumiwa kama dawa Mashariki mwa Bara Asia.

Nchini Kenya kilo moja ya Pembe za Ndovu, inaweza kukugharimu kati ya shilingi 12,000-18,000.

Uwindaji haramu umetajwa kama bishara haramu ya kimataifa ambapo wawindaji hasa huwawinda ndovu na vifaru kwa wingi. Ni hapo jana tu ambapo kifaru mmoja aliyetambulika kwa jina Josephina, aliuawa katika mbuga ya wanyama ya Nairobi.
Kenya inakabiliwa na changamoto ya kuwindwa kiharamu kwa Ndovu zake

Alikuwa kifaru wa kike mwenye umri wa miaka minne. Maafisa wa kulinda wanyama pori wanasema kuwa, kuuawa kwa Joeshina ni mfano mbaya kwani Vifaru wa kike wana umuhimu mkubwa katika kuongeza idadi ya wanyama hao wanapozaana.

Kwa muda wa wiki moja nchini Kenya, kimeripotiwa matukio manne ya uwindaji haramu katika mbuga tofauti tofauti.

Mkuu wa shirika la kulinda wanyama pori nchini Kenya, bwana William Kipsang, anasema kuwa tatizo la uwindaji linachangiwa na maswala ambayo hawawezi kudhibiti kama shirika.

''Serikali ya Kenya imetumia mamilioni ya fedha kuhifadhi wanyama pori , lakini nchini Kenya na kwingineko barani Afrika raia wengi wangependa kuona usalama wa binadamu ukishughulikiwa kwanza badala ya wanyama pori. Vile vile watu wengi huishi katika miji iliyo mbali na misitu na wanyama hao,'' alisema Kipsang

Mashirika ya kulinda wanyama wanasema ikiwa tatizo la uwindaji haramu halitatatuliwa, basi kwa muda wa miaka ishirini, ndovu na vifaru barani Afrika hawatokuwepo tena.

Asilimia kumi ya uchumi wa Kenya hutegemea utalii, ikiwa Kenya itapoteza Ndovu na vifaru wake, basi sekta ya utalii itaathirika pakubwa.

Mauaji yazidi kutikisa Tarime

Hali ya usalama Tarime imezidi kutoweka baada ya jambazi lisilofahamika likiwa na bunduki ambayo haijafahamika aina yake kuendelea kuua watu kwa risasi hasa wa jinsi ya kiume, ambapo idadi ya waliouawa imefikia saba hadi sasa na inadaiwa huwaua watu na kupotea bila kutambuliwa.

Jambazi hilo lisilofahamika liliua watu hao usiku wa Januari 27, mwaka huu katika maeneo ya Nkende likianza na kumuua Mwendesha Bodaboda, Juma Marwa Mkazi wa Nkende mjini Tarime akiwa anaelekea nyumbani kwake ambaye alikufa akiwa hospitali akipatiwa matibabu.

Mganga wa Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Tarime, Marco Nega alisema tangu Januari 27 hadi sasa hospitali imeendelea kupokea watu waliouawa na majeruhi ambao wamefanyiwa uchunguzi na kugundulika wakiwa wamejeruhiwa kwa risasi katika sehemu mbalimbali za mwili na kwamba watu wapatao 7 wamekwisha kufa mpaka sasa.

“Tumepokea maiti za watu na majeruhi na tumewafanyia uchunguzi wakagundulika wana majeraha ya risasi sehemu mbalimbali za mwili, ambapo tayari watu saba wamekufa wengine wamekufa wakiwa njiani wakienda kwenye matibabu Musoma, marehemu hadi ni saba,” alisema Nega.

Waliojeruhiwa wakosa huduma ya X-ray

Watu waliojeruhiwa wameshindwa kupatiwa huduma ya X-Ray kutokana na Hospitali ya Wilaya kutokuwa na huduma hiyo kwa muda wa zaidi ya miezi 3 na kusababisha wagonjwa kusafirishwa kwenda Musoma na Mwanza kwa matibabu, ambapo Samweli Richard amekufa akiwa njiani kuelekea Musoma kwenye matibabu ikiwamo huduma hiyo ya X-ray.

Hospitali ya Wilaya yashindwa kutoa huduma

Huduma kwa wagonjwa mbalimbali katika Hospitali ya Wilaya imeshindwa kuendela vilivyo baada ya kupatwa na misiba miwili ya watumishi wawili, ni baada ya waume zao kuuawa na jambazi hilo lisilofahamika.

Awali Januari 26 jambazi hilo lilimuuwa Robert Kisiri (45) mkazi wa Mugabiri ambapo Mstaafu wa JWTZ Zacharia Mwita(58) na Erick Makanya (25)wote wakazi wa Kijiji cha Mogabiri Kata ya Kitare Wilayani Tarime walikutwa wakiwa wameuawa na miili yao ikiwa na majeraha ya risasi mbavuni kushoto na mgongoni.

Pia jambazi hilo liliwajeruhi watu watano kwa risasi ambao ni Mgosi Marwa Mkazi wa Mogabiri, Joseph Richard Mkazi wa Rebu, Gastor Richard Mkazi wa Rebu, Juma Mwita Mkazi wa Mogabiri na Mkandarasi Binafsi wa ujenzi, Mwasi Yomami ambao kati ya hao wawili wamefariki wakati wakipatiwa matibabu.

Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Tarime/Rorya, Justus Kamugisha amesema wamemkamata mtu mmoja anayeshukiwa kuwa mhusika wa mauaji ambaye yuko chini ya ulinzi kwa mahojiano na kwamba anazidi kuongeza vikosi vya doria kuimarisha ulinzi na usalama na kuwasaka wahalifu.

Nape hajui anapambana na nani CCM

Dar es Salaam. Mwaka 2010 ulikuwa mgumu mno kwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, kwani alikuwa akiwania nafasi ya ubunge katika Jimbo la Ubungo.

Kati ya vigogo aliokuwa akipambana nao ndani ya CCM ni pamoja na aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Shamsa Mwangunga na aliyekuwa mkuu wa wilaya kadhaa, Hawa Ng’umbi ambaye ndiye alishinda.

Hata hivyo, Ng’umbi alibwagwa na John Mnyika wa Chadema. Lilikuwa ni pigo kubwa mno kwa CCM na hasa kwa Nape ambaye alishajipambanua kama mpenda mageuzi ndani ya chama.

Alishajiwekea rekodi ya kufichua ufisadi ndani ya chama hicho hasa ule wa ujenzi jengo la Umoja wa Vijana pale Lumumba.

Hapo ndipo zikaanza kusikika tetesi kuwa Nape alitaka kuhamia Chadema, mara wengine wakimhusisha na chama kipya wakati huom cha CCJ (sasa CCK) kilichokuwa kikidaiwa kuanzishwa na baadhi ya vigogo wa CCM wasioridhishwa na mwenendo wa chama hicho tawala.

Lakini CCM nao walionekana kuushtukia mchezo huo. Siku chache kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 mara Nape akafutwa machozi na Rais Jakaya Kikwete alipoteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Masasi. Ilikuwa kama gia ya kumshikilia asije kukimbilia vyama vingine.

Aliishikilia nafasi hiyo hadi mapema Machi, 2011 ambapo CCM ilifanya mabadiliko ya sekretarieti. Hapo Nape akapewa nafasi ya Katibu wa Itikadi na uenezi anayoishika hadi sasa, huku nafasi ya Katibu Mkuu akipewa Wilson Mukama.

Mabadiliko hayo yalikwenda sanjari na mkakati wa kujivua gamba. Hapo mhemko tena wa Nape na viongozi wenzake kukisafisha chama na ufisadi ukaanza pale waliposisitiza kuwa lazima wale wanaochafua sura ya chama wawajibishwe.

Sote ni mashahidi, hadi leo hakuna aliyevuliwa gamba. Chama kinaendelea kusonga mbele na magamba yake.

Juzi juzi tena baada ya sekretarieti ya chama kubadilishwa na Abdulrahman Kinana kuwa Katibu Mkuu, Nape akabebeshwa mzigo la kutaja mawaziri mizigo. Wakawashikia kidedea hadi Kamati Kuu ya CCM ili wahojiwe. Wamehojiwa lakini baadaye wamerejeshwa barazani.

Mara Nape kaibuka tena mbele ya waandishi wa habari akisema eti CCM hakitasita kuchukua hatua kali dhidi ya mawaziri na watendaji wengine watakaoshindwa kurekebisha upungufu unaopigiwa kelele.

Itachukua hatua gani, wakati Mwenyekiti wa chama Rais Kikwete amesharidhika na mizigo yake? Ni kama vile Nape anatamani yeye ndiye angekuwa rais ili awafurumushe mawaziri hao, lakini basi hawezi….!
Hiyo ndiyo CCM. Utamaduni wa kuwajibishana na kufukuzana haupo. Mwenzako akifanya kosa unamezea. Kama Nape anaona kasi yake haiendani na CCM, bora atafute chama kingine ahamie.

Vinginevyo atakuwa anapiga kelele za bure huku wenzake wakiendelea kuchukua vyao mapema.

Tuesday 28 January 2014

Maadhimisho ya miaka 50 TICD -TENGERU ya vuruga na ATC

hii n timu ya mpira TICD_Tengeru
Chuo cha maendeleo ya jamii Tengeru (TICD) kimeanza vibaya maadhinisho ya miaka 50 ya chuo,wakiona cha mtema kuni wachapwa 1 0 na timu ya ATC ,Timu yampira wa miguu ya chuo hicho yanyolewa bila maji na Arusha Technical college (ATC)
Mchezo huo ulikuwa wakuvutia huku kila timu ikitafuta goli la mapema. Mnamo dakika ya 25 ya mchezo timu ya ATC ilijipatia kona ya kwanza katika mchezo lakin ilishindwa kuza matunda baada ya golikipa wa TICD Paul kuokoa mpira huo wa hatari , lakin baada ya dakika mbili tu nusura TICD wajipatie goli la mapema baada ya mshamuliaji wake machachari Godson Lema kupiga shuti kali lakin mlinda mlango wa ATC alikuwa makin na kuokoa shuti hilo .
Mchezo ulikuwa mzuri kipindi cha kwanza timu zote zilikuwa zina shambuliana kwa zamu lakin hadi mapumziko kipindi cha kwanza “Half Time” hakuna timu iliyo fanikiwa kuona lango la wenzie

Baada ya dakika moja tu kipindi cha pili kuanza dakika ya 46 mabeki wa TICD walifanya uzembe kwa kutegeana mpira na kumfanya mshambuliaji hatari wa ATC aliyekuwa amevalia jezi nambari 9 Musa alifanikiwa kumpokonya beki wa TICD na kupiga shuti kali lililo mshinda mlinda mlango wa TICD Paul john na kumwacha njia panda bila kujia la kufanya.
Mnamo dakika ya 60 timu ya TICD ililisakama lango la ATC bila mafanikio . Dakika ya 70 ya mchezo Mwamuzi ALLEN alilazimika kumwonyesha kadi ya njano mshambuliaji wa TICD Godbles Lema baada ya kumlalamikia mwamuzi kwa kuwanyima penalti baada ya mchezaji mwenzake alimaarufu kama “CHICHARITO” kufanyiwa madhambi ndani ya box
Mnamo dakika ya 79 timu zote mbili zilifanya mabadiliko kwa kuwatoa wachezaji wawili wawili kila timu lakim mabadiliko hayo hayakozaa matunda katika timu ya TICD , hadi mwamuzi wa kati Allen akipuliza kipenga cha mwisho TICD(Tengeru Instutute of community development) 0 1 ATC (Arusha technical college )

Monday 27 January 2014

Ney wa mitego aachwa na mchumba wake

UCHUMBA wa staa wa wimbo wa Muziki Gani, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ na mpenzi wake anayefahamika kwa jina moja la Siwema umedaiwa kuvunjika.
Nay akiwa na mpenzi wake Siwema.

Kwa mujibu wa chanzo makini, chanzo cha kumwagana ni baada ya Siwema kukuta meseji za watoto wa kike tofauti katika simu ya Nay wa Mitego katika nyakati tofauti.
Chanzo hicho kimeeleza kuwa, wawili hao walimwagana tangu Januari 2, mwaka huu, nyumbani kwa Nay wa Mitego, Manzese jijini Dar es Salaam baada ya Siwema kujiridhisha kuwa mpenzi wake huyo anamsaliti kutokana na ushahidi wa meseji alizozifuma.
Hata hivyo, chanzo kilizidi kumwaga ‘ubuyu’ kuwa, wapendanao hao wamekuwa wakizinguana mara kwa mara na kilichomuuma zaidi Siwema ni baada ya mkali huyo kuachia video yake mpya ya Nakula Ujana ambayo ameonekana katika pozi za kimahaba na warembo kibao.
“Imemuuma sana video ya Nakula Ujana, warembo wale inasemekana hakuishia katika video, sasa aliendelea kuwasiliana nao na Siwema akagundua ndipo mtiti ulipoibuka, Siwema akarudi kwao Mwanza,” kilisema chanzo.
Baada ya kunyetishiwa habari hizo, paparazi wetu alimtafuta Siwema ambaye alikiri kugombana na Nay na kusema ameshindwa kuvumilia na ameona ili kujiepusha na presha zisizo za lazima arudi kwao Mwanza.
“Kweli tuna ugomvi na Nay na haswa kuna mambo yananikera sana ila kubwa zaidi kwa sasa ni ile video yake mpya kuna parties mle sijazipenda...mchumba wa mtu ufanye video ujiachie vile, unashikwa shikwa ovyo,” alisema Siwema.
Alipotafutwa Nay, alikiri kutokea kwa ugomvi huo na kudai yupo katika jitihada ya kumaliza tofauti hizo kwa kuzungumza na Siwema.

Hatian kwa kumwita Rais Kiazi

MWANASIASA wa Chama cha upinzani nchini Zambia cha Alliance for a Better Zambia (ABZ), Frank Bwalya, amekamatwa na polisi na kufunguliwa mashtaka kwa madai ya kumkashifu rais wa nchi hiyo, Michael Satta, kwa kumwita kiazi.
Bwalya anadaiwa kumwita Rais Satta kuwa ni ‘Chumbu Mushololwa’, akimaanisha kiazi, kupitia kituo kimoja cha redio nchini humo.
Katika lugha ya Kibemba, maneno hayo yana maanisha kiazi kitamu, ambacho humegeka kinapopondwa, akimaanisha kuwa rais huyo hasikilizi ushauri wa wengine.
Aidha, taarifa kutoka nchini humo zinasema kuwa iwapo itathibitika kiongozi huyo wa ABZ kutoa matamshi hayo, atatiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo cha miaka mitano jela.

Bwalya anakuwa mwanasiasa wa pili kuingia matatani baada ya mwanasiasa mwingine wa upinzani, Nevers Sekwila Mumba, wa Chama cha Movement for Multiparty Democracy kuhojiwa na polisi mwaka jana kwa kumwita Rais Satta muongo.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Stephen Kampyongo, alisema Bwalya alikamatwa kwa kutoa matamshi ya kumharibia sifa Rais Satta.

Kutokana na kukamatwa kwa kiongozi huyo, kambi ya upinzani imetaka Bwalya aachiwe huru huku ikisisitiza kuwa kiongozi huyo ni mwanasiasa asiyemuogopa mtu yeyote.
Aidha, wanasiasa wa upinzani wamesema kuwa matamshi ya Bwalya si matusi kama inavyotafsiriwa. Hali ya kisiasa si shwari kwa sasa nchini Zambia kutokana na mvutano kati ya upinzani na utawala.

MNYIKA nae atajiuzulu?

Jana mitandao ya kijamii ilijazwa taarifa kwamba jana jioni, John Mnyika (Mb) alimwandikia barua ya kujiuzulu Katibu Mkuu wa CHADEMA.

Ofisa Habari Mwandamizi wa CHADEMA, Tumaini Makene (0752 691569) alijibu kwa kukanusha kuhusu taarifa hizo na kuongeza kuwa kwa muda uliotajwa, Mhe. Mnyika alikuwa katika shughuli za chama akitimiza majukumu yake.

Akasema taarifa hizo ni mradi wa kutengeneza uongo unaofadhiliwa na watu kwa sababu ya, “kuwasumbua wanachama na

Watanzania, lakini pia kutaka kuonesha kuwa kundi la wasaliti na wanafiki ndani ya chama linaungwa mkono na watu makini ndani ya chama ambao kama wangekuwa upande wao, wangesaidia kundi hilo kuondoa taswira hasi linalopata mbele ya jamii. Wanatafuta uhalali walioupoteza kwa kufanya harakati za kusaliti mapambano.


Mioyoni mwao wanaumia kweli kweli kuonekana wanaungwa mkono na watu wasio wanachama wa CHADEMA, ambao wengine wanalazimika kwenda kuwanunua pale feri Posta na Kariakoo ili waje kuwashangilia Mahakamani na kukimbia barabarani.

Tunajua wanaumia kutumia mamilioni kukodi watu kuja kulia kwenye msiba wasioujua wala usiokuwa wa kwao, huku wakidai ujira hadharani.” aliandika Makene

Kubenea katika tovuti hiyo aliandika, “Nathibitisha ifuatavyo: Nimeonge na Mnyika muda huu, amenihakikishia kuwa habari hiyo siyo ya kweli. Hajajiuzulu na wala hana sababu ya kujiuzulu. Anasema, hawezi kuungana na watu wanaokivuruga chama. Anaipenda Chadema na anaamini ndiyo chama bora kwa sasa.”

Nigeria na zimbambwe zatinga Nusu fainali CHAN

Beki wa Zimbabwe 'Warriors', Kudakwashe Mahachi, aliwapa wakati mgumu Mali baada ya kuwatoka mabeki wao wanne na kufunga bao safi la pili lililoifanya nchi kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani 'CHAN' katika mechi ya robo fainali iliyochezwa juzi.
Mbele ya macho ya washabiki wengi wa Zimbabwe, beki huyo aliyebarikiwa kutumia mguu wa kushoto alikimbia na mpira akiwatoka mabeki hao kuelekea golini kwa Mali katika dakika ya saba ya kipindi cha pili kabla ya kuachia shuti lililompita kipa Diakite ambaye alishindwa la kufanya kuisaidia nchi yake ya Mali isifungwe bao hilo.
Zimbabwe imetinga hatua hiyo kwa ushindi wa mabao 2-1 huku katika mechi zake tatu zilizotangulia katika michuano hiyo ikiwa haijaruhusu bao hata moja kwenye goli lake.
Mchezaji Ibourahima Sidibe wa Mali alipata nafasi nzuri ya kufunga bao ndani ya dakika tatu za mwanzo za mechi hiyo, lakini George Chigova alienda chini kifundi kuzuia mpira usitinge kwenye nyavu za nchi yake.
Zimbabwe ilipata bao lake la kwanza katika dakika ya 11 wakati Simba Sithole alipompita Souleymane Konate kabla ya kupiga shuti la chini lililompita kipa Soumaila Diakite.
Katika dakika ya 24, Diakite alifanya kazi nzuri kuzuia shuti la mpira uliosafiri umbali mrefu usiingie golini kwake ambapo kidogo ungeipatia Zimbabwe bao la pili kupitia kwa Peter Moyo.
Zimbabwe iliendelea kuongeza mashambulizi kwa wapinzani wao, lakini hawakuweza kuongeza bao la pili katika dakika 45 za kwanza kutokana na jitihada kubwa za kipa wa Mali, Diakite.
Lassan Diara alipoteza nafasi murua ya kusawazisha katika muda uliokaribia mapumziko wakati shuti lake kali lilipopiga juu ya mwamba wa goli.
Lakini vijana wa Ian Gorowa waliamka na kuanza kushambulia zaidi kipindi cha pili walipopata bao la pili kupitia kwa beki Mahachi.
Viungo wa Zimbabwe walifanikiwa kumiliki sana mipira katika mechi hiyo, lakini Mali hawakukatishwa tamaa ya kuendelea kutafuta mabao.
Hata hivyo, Mali walipoteza nafasi nzuri zaidi katika dakika ya 75 baada ya Hamidou Sinayoko alipojaribu kupiga mpira ulioenda pembeni akiwa na nia ya dhati kabisa ya kummaliza kipa Chigova wa Zimbabwe.
Diakite aliendelea kuiokoa nchi yake isioge mabao baada ya kuokoa mchomo dakika ya 84 wakati alipopangua mpira wa Masimba Mambare na kusababisha kona ambyo haikuzaa bao.
Mali wangeweza kusawazisha tena dakika ya 88, lakini mpira wa chini uliopigwa na Sinayoko ulizuiwa kifundi na Chigova na kuwa kona ambayo Sinayoko aliipatia bao la kufutia machozi Mali.
Kwa ushindi huo, Zimbabwe imefuzu nusu fainali katika michuano hiyo inayofanyika Afrika Kusini pamoja na Nigeria ambapo, washindi wengine wawili wa kuungana nao hatua ya nusu fainali walitarajiwa kujulikana jana, usiku baada ya mechi kati ya Gabon na Libya na nyingine kati ya Ghana dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrais ya Congo (DRC).
Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan, ameipongeza 'Super Eagles' kwa ushindi wa kishujaa ambapo, walifanikiwa kuzawazisha mabao matatu na kushinda kwa mabao 4-3 dhidi Morocco katika mechi nyingine ya robo fainali iliyochezwa juzi mjini Cape Town.
Hadi mapumziko, Morocco walikuwa wakiongoza kwa mabao 3-0 katika mechi hiyo.
Rais Jonathan kupitia maelezo yake yaliyosainiwa na Reuben Abati ambaye ni Mshauri Maalumu wa Rais (habari na uchapishaji), alipongeza ushindani uliooneshwa na wachezaji wa nchi yake ambapo, Super Eagles walishindana na kufanikiwa kuzawazisha mabao 3 hadi kuongeza bao la nne na kufanikiwa kutinga nusu fainali.
Katika pongezi hizo, Rais Jonathan aliwamwagia sifa Super Eagles kwa moyo wao wa kujituma, uzalendo na kujitolea kwa taifa lao.
Alisisitiza kwamba, wachezaji hao waendelee na moyo huo kwa ajili ya taifa lao mpaka ushindi wa mwisho upatikane katika michuano hiyo inayoshirikisha wachezaji wanaocheza ligi za ndani barani Afrika.
Pia, Rais Jonathan aliwahakikishia Super Eagles kwamba, wataendelea kupata mchango wa kila hali kutoka kwa serikali ya shirikisho pamoja na Wanigeria wote wakati wakiendelea kupambana kuhakikisha kuwa, wanaongeza taji hilo baada ya kushinda lile Fainali za Mataifa ya Afrika mwaka jana.
Rais huyo aliungana na wananchi wote wazalendo waliofurahishwa na ushindi huo kuwaombea washinde mechi inayofuatia ya nusu fainali ya michuano hiyo.
Katika mechi hiyo, mabao ya Nigeria yalifungwa na U. Uzochukwu (dakika ya 49), R. Ali (dakika ya 55), E. Uzoenyi (dakika ya 90) na A. Ibrahim (dakika ya 111).
Mabao ya Morocco yalifungwa na M. Moutouali (dakika ya 33), M. Iajour (dakika ya 37) na M. Mouto
(dakika ya 40).
Hadi tunakwenda mitamboni, Gabon ilikuwa nguvu sawa na Libya kwa bao 1-1 dakika ya 75 katika mechi ya robo fainali nyingine iliyoanza saa 12 jioni, jana huku DRC ikitarajiwa kupambana na Ghana katika mechi kali nyingine ya robo fainali iliyotatarajiwa kupigwa kuanzia saa 3:30 jana pia.
Mechi za nufu faiinali zimepangwa kuchezwa Januari 29.

Uwanja wa Arsenal watia aibu England nzima

ARSENAL Ijumaa iliyopita iliichapa Coventry City na kusonga mbele kwenye Kombe la FA, lakini kali zaidi ilifanywa na mashabiki wao kwenye Uwanja wa Emirates.

Kwenye mchezo huo, baadhi ya taa kwenye majukwaa ya Uwanja wa Emirates zilizima na kuonekana giza jambo lililowafanya mashabiki kuwasha tochi za kwenye simu zao na kupatikana mwanga uliotosha kutambuana na kuendelea kutazama mechi hiyo.

Kilichovutia zaidi, wakati mashabiki wa Arsenal wakiwasha tochi kwenye simu zao ili kupata mwanga, mashabiki wa Coventry City walikuwa wakiimba nyimbo za kuitaka Arsenal kulipa bili ili umeme usiwe unakatika kama ilivyotokea siku hiyo.

Arsenal ilishinda mabao 4-0, shukrani kwa mabao mawili ya Lukas Podolski, Santi Cazorla na Olivier Giroud.

Mwombeki aitia Simba aibu

KOCHA wa Simba, Zdravko Logarusic amesema aliamua kumtoa straika Betram Mwombeki dakika 20 baada ya kumuingiza dhidi ya Rhino Rangers ili kumsitiri kwa aibu ambayo angeipata kutoka kwa mashabiki.

Katika mchezo huo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa jana Jumapili Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na Simba kuibuka na ushindi wa bao 1-0, Logarusic alimuingiza Mwombeki dakika ya 65 kuchukua nafasi ya Amissi Tambwe.

Dakika chache baada ya kuingia uwanjani, Mwombeki alipoteza pasi tatu ndani ya dakika nane hali iliyomfanya Logarusic ampigie kelele za kuelekeza kila anapokosea.

Mara kadhaa Mwombeki alipokuwa akikosea alionekana kujutia kosa lake kwa kujaribu kukaba ili apokonye mpira aliopoteza, lakini Logarusic alikuwa akishika kichwa kuonyesha kutopendezwa na makosa hayo. Uvumilivu ulimshinda kocha huyo kwani dakika 85 alimtoa Mwombeki na kumuingiza Henry Joseph. Wakati anatoka straika huyo alisalimiana na Logarusic ikiwa ni ishara ya kutokuwepo kwa tatizo baina yao.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Logarusic alisema alilazimika kumtoa Mwombeki kutokana na kushindwa kutimiza alichotumwa uwanjani akitokea benchi pia kumsitiri kwa aibu ya kuzomewa na mashabiki.

“(Mwombeki) alikuwepo benchi kuona makosa ya wenzake, lakini alipoingia kila mtu ameona alichokuwa anafanya, mashabiki wakaanza kumpigia kelele ndipo nikaona nimsitiri kwa kumtoa maana angebaki angepata aibu zaidi,”

Tuzo ya Tanzania Boxing Award' yaangukia kwa CHEKA

NGULI wa masumbwi nchini, Francis Cheka ameng'ara katika tuzo za Ngumi za 'Tanzania Boxing Award' baada ya kunyakua tuzo mbili katika hafla hiyo.
Cheka bondia pekee aliyeonekana kivutio katika tuzo hizo amenyakua tuzo ya bondia bora wa mwaka 2013 na bondia bora wa ngumi za kulipwa kwa mwaka huo.
Akizungumza mara baada ya kunyakua tuzo hizo, Cheka ameushukuru uongozi wa BFT kwa kuandaa tuzo hizo na kufanyika kwa mara ya kwanza kwa kuwa hapo awali zilikuwa zikitangazwa huku wahusika wakiingia mitini.
Cheka alisema amefarijika sana kutwaa tuzo hizo kwani inaonesha wazi wadau wanatambua mchango wake katika tasnia hiyo ya masumbwi nchini.
Alisema endapo utoaji tuzo hizo ukiendelea kufanywa utahamasisha mabondia wachanga waweze kushiriki kwa wingi katika mchezo huo kwani wataona mchango wao unathaminika tofauti na zamani.
Naye Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia alisema tuzo hizo zimekuja wakati mwafaka kwa kuwa yeye ni kipenzi cha wanamichezo na amefanikiwa kuwa Naibu waziri wao.
Nkamia alisema atatoa ushirikiano kwa BFT kwa kuwa wameonesha moyo wa kufufua mchezo huo kwa kasi kubwa.
Waziri huyo amesikitishwa na ulingo unaotumiwa na mabondia wa Tanzania katika kufanyia mashindano mbalimbali kwani hauna hadhi kabisa ya kutumika katika michuano hiyo.
"Tanzania ina mabondia wengi wazuri ambao wanawakilisha nchi kimataifa, ni aibu kuona ulingo wanaotumia kupata mabondia hao haukidhi vigezo vyovyote," alisema Nkamia.
Nkamia ameahidi kutatua matatizo ya wanamichezo pale inapobidi kwa kuwa hata yeye ana uchungu mkubwa anapoona wanamichezo wa Tanzania wanafanya maandalizi katika mazingira magumu.
Naye Makamu Mwenyekiti wa tuzo hizo, Mutta Lwakatare ambaye pia ni Rais wa BFT, amewaahidi wanamasumbwi kuendelea kuboresha tuzo hizo mwaka hadi mwaka na kwamba mapungufu mengi yaliyojitokeza katika tuzo hizo hayatajirudia kwa kuwa huo ulikuwa ni mwanzo tu.
Lwakatare alisema uongozi wake utajipanga kuboresha masumbwi kwa kuwa wanachama hai wa shirikisho hilo kwa sasa ni wachache hivyo kuhakikisha wanafufua uhai wa wanachama wao.
"Tuna klabu nyingi sana za ngumi kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara lakini klabu hai zilizosajiliwa ni chache sana hivyo ipo haja ya kuhakikisha uhai wa klabu tulizonazo unakuwepo kwa kila mkoa ili iwe rahisi kupata mabondia kutoka mikoa yote Tanzania Bara," alisema Lwakatare.

Lipumba ‘awalipua’ mawaziri wa JK

MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, amedai kutilia shaka uwezo alionao Waziri wa Fedha, Bi. Saada Mkuya, katika kuiongoza Wizara hiyo na kudai sifa zake kitaaluma, zimegubikwa na utata mkubwa.
Prof. Lipumba aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Alisema kwa mujibu wa tovuti ya Bunge, haioneshi vyuo vya kitaaluma alivyosoma Bi. Mkuya hali inayotia shaka uwezo wake wa kuongoza Wizara nyeti kama hiyo.
Aliongeza kuwa, kama wasifu wa Bi. Mkuya uliopo katika tovuti hiyo upo sahihi ni wazi kuwa Waziri huyo hana uzoefu wa kisiasa, kitaaluma, kiutawala hata kuongoza Wizara hiyo.
"Sina hakika kama ana uelewa wakutosha kuhusu Menejimenti ya fedha za umma, upembuzi yakinifu wa miradi ya umma, athari za nakisi ya bajeti katika mfumuko wa bei, deni la Taifa, sera ya kukuza na kubadilisha mfumo wa uchumi.
"Pia sina hakika kama ana uzoefu wa kuendeleza viwanda vya ndani, kuongeza uuzaji bidhaa zetu nje ya nchi ili kuongeza ajira na ushindani katika soko la dunia," alisema Prof. Lipumba
Alisema Waziri wa Fedha anapaswa kuwa na uwezo mkubwa wa kuchambua sera za uchumi, kujenga hoja wakati wa majadiliano na mashirika ya kimataifa, kwenye mijadala na Mawaziri wenzake pamoja na asasi nyeti.
Prof. Lipumba alisema Serikali inakabiliwa na tatizo kubwa la fedha ambapo matumizi yanaongezeka kuliko mapato hivyo kupunguza uwezo wa Serikali kuchangia Bajeti ya Maendeleo.
Alisema nakisi (makisio) ya bajeti yameongezeka kutoka sh. bilioni 389 mwaka 2007/08 sawa na asilimia 1.7 ya pato la Taifa na kufikia sh. bilioni 2,992 mwaka 2012/13, sawa na asilimia 6.2.
Aliongeza kuwa, nchi ikiendelea na kasi ya kukopa Rais Jakaya Kikwete akiondoka madarakani, Taifa litakuwa na deni kubwa hadi kutoka nje.
"Katika sekta ya ujenzi wa barabara, makandarasi walio wengi hawajalipwa kwa wakati hivyo miradi mingi imekuwa ikisuasua, wakati mwingine Wizara husika inasaini miradi mipya wakati hakuna fedha zilizotengwa katika bajeti, Waziri wa Fedha ana wajibu wa kuweka nidhamu katika matumizi ya Serikali," alisema Prof. Lipumba.
Alisema, wakati Rais Kikwete anaingia madarakani mwaka 2005, alisema hakuna chuo kinachofundisha Uwaziri hivyo mtu yeyote anaweza kuwa Waziri ambapo mtazamo huo unachangia kuteua Mawaziri wasio na sifa za kutekeleza majukumu yao.

Chelsea ya zamisha meli ya Stock city

Chelsea imeifunga Stoke City katika mechi ya Kombe la FA iliyochezwa kwenye Uwanja wa Stamford Bridge jana.
Alikuwa ni mshambuliaji Mbrazil, Oscar ambaye aliweza kuitoa kifua mbele timu yake hiyo wakati alipoukwamisha mpira wavuni katika dakika ya 27.
Hadi mapumziko, Chelsea walikuwa mbele kwa bao hilo moja.
Chelsea ilicheza mechi hiyo siku moja baada ya kiungo wao mahiri, Juan Mata kuhamia Manchester United.
Baadhi ya washabiki wa timu hiyo walikumbuka namna ambavyo mchezaji huyo aliposhirikiana na wachezaji wengine wa kikosi hicho kuleta ubingwa wa Ulaya ambapo, walibeba mabango yenye ujumbe wa kumshukuru.
Katika mechi nyingine ya michuano hiyo jana, Fulham ilitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Sheffield United kwenye Uwanja wa Bramall Lane.
Hadi mapumziko, Fulham ilikuwa ikiongoza 1-0 kwa bao lililofungwa na C. Porter dakika ya 31 kabla ya H. Rodallega kusawazisha dakika ya 75.

Majambazi wampiga risasi mfanyabiashara nyumbani

Mbeya. Watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi, wamemvamia na kumjeruhi kwa risasi, mfanyabiashara maarufu wa simu jijini Mbeya, Obadia Mtawa (41).

Vitendo hivyo vimefuatiwa na kumpora mamilioni ya fedha, simu na gari la kutembelea.

Tukio hilo lilitokea juzi jioni, muda mfupi baada ya Mtawa kurejea nyumbani kwake katika Mtaa wa Isyesye, akitokea katika shughuli zake katika eneo la Ilomba.

Alikuwa na gari lake lililokuwa na kasha lenye fedha na simu za aina mbalimbali.

Akizungumzia mkasa huo akiwa katika wodi ya Mifupa katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya, Mtawa alisema akiwa njiani kurejea nyumbani aliona pikipiki mbili zilizokuwa nyuma yake, zikiwa zimewashwa taa.

Alisema pikipiki hizo zilikuwa na watu waliokuwa wamepakizana.

Alisema baada ya kushuka kwenye gari lake akijiandaa kuingia ndani, alisikia sauti za watu wapatao wanne wakimwambia kuwa yuko chini ya ulinzi na kwamba mmoja wao aliipiga panga lake kwenye gari lake.

“Niliposhuka kwenye gari wakaingia ndani na kusema nipo chini ya ulinzi na baadaye wakapiga risasi ambazo moja ilinipiga mguuni kisha wakaniuliza fedha ziko wapi,” alinena.

Alisema aliwajibu kuwa fedha zilikuwa kwenye gari na kuwataka wazichukue. “Wakachukua funguo za gari na kisha wakaingia kwenye gari na kuoondoka nalo likiwa na fedha na simu,” alisema.

Alisema kiasi cha fedha kilichochukuliwa hakijui lakini zilikuwa za mauzo ya siku nzima ya juzi na kwamba kwa wastani maduka yake yanakusanya Sh50 milioni.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba polisi walikuwa wakiwasaka watu hao.

Msangi alisema juhudi za wananchi na polisi zilifanikiwa kuliona gari la Mtawa katika maeneo ya Uyole na kwamba hadi jana hakuna mtu aliyekamatwa.
Kamanda huyo alisema uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa kuna watu waliokuwa wakimfuatilia Mtawa kwa muda mrefu.

Mrema aanza jitihada kutoa TLP ‘ pangoni

Moshi. Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Vunjo, mkoani Kilimanjaro, kimepata pigo baada ya wanachama wake 28 akiwamo Mwenyekiti wa Kijiji cha Komalangoye, Israel Mtui na viongozi wengine saba kujiunga na Chama cha Tanzania Labour (TLP).

Licha ya mwenyekiti huyo wa chama, wamo Katibu wa CCM wa kijiji hicho, Thomas Matemu, Katibu wa vijana, Jofrey Minja, Mwenyekiti wa vijana, Sabas Minja na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake, Felister Matemu.

Wengine ni Paul Alex ambaye ni Balozi wa CCM Kitongoji cha Ikunda, Balozi wa Kitongoji cha Majengo, Estak Minja, Mwenyekiti wa CCM Kitongoji cha Liwari, Baltazari Minja, Mwenyekiti wa Kitongoji cha Masoi Aqulin Kombe na Grace Mamiro Mwenyekiti Kitongoji cha Kiala chini ambao wote kwa pamoja walisema wamechoshwa na sera zisizotekelezeka za CCM.

Akiwapokea Mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema alisema hiyo ni filimbi kwa CCM kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwaka huu. Alisema chama kipo imara kamwe hawapo tayari kuendelea kukaa na chama kisichowaletea maendeleo.

SIMBA SC YAANZA MZUNGUKO WA PILI KWA KUWAFUMUA RHINO - MESSI AENDELEZA MAKALI

Ramadhani Singano 'Mess' (kulia), akishangilia bao pekee aliloifungia timu yake katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara dhidi ya Rhino Rangers ya Tabora katika mchezo uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.


Ramadhani Singano akiipangua ngome ya Rhino Rangers ya Tabora.
Kipa wa Rhino Rangers, Charles Mpinuki akidaka pelnati ya mshmambuliaji wa Simba, ramadhani Singano 'Mess' katika mchezo wa Ligi Kuu.
Beki wa Rhino Rangers, Julius Masunga akitafuta mbinu za kumtoka Haruna Chanongo wa Simba.

Mwamuzi wa pembeni, Frank Komba kutoka Pwani alilalamikiwa na wachezaji wa Simba baada ya kukataa moja ya goli lililofungwa na timu hiyo.

Beki wa timu ya Rhino Rangers, Julius Masunga akiusindikiza mpira wavuni katika harakati za kuokoa, hata hivyo mwamuzi wa mchezo huo alilikataa bao hilo na kulalamikiwa na wachezaji wa Simba, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara kuliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Simba ilishinda 1-0.

FA yafika patamu sasa , Arsenal vs Liverpool, Man city vs Chelsea

Droo ya michuano ya kombe la FA imefanywa punde kwa mechi za mchujo wa raundi ya tano.

Chelsea wamepangiwa kucheza na Manchester City katika mchezo unaotazimiwa na ushindani wa hali ya juu.

Chelsea ambao wamefuzu kwenye raundi ya tano kwa kuiondosha Stoke City katika mchezo ambao ulimalizika kwa ushindi wa bao moja kwa bila.

Kocha wa Chelsea Jose Mourinho akizungumza punde baada ya droo hii amesema, "Iwapo unataka kuwa bora lazima ucheze na timu bora."

Nao Manchester City wao walijikatia tiketi ya kufuzu michuano hiyo hatua ya tano kwa kuiadhibu Watford kwa mabao 4-2.

Liverpool wao watakuwa wageni wa Arsenal kwenye mchezo wa raundi ya tano.

Roberto Martinez ataiongoza Everton kukutana na timu yake ya zamani ya Swansea, ilihali Sunderland wao watacheza na Southampton ikiwa ni mechi liyokutanisha timu zote za ligi ya England.

Cardiff watakuwa nyumbani kuwakaribisha Wigan na Hull watacheza na Brighton. Sheffield Wednesday watapamabana na wenzao walioko kwenye ligi ya Championship, Charlton FC.

Mechi zote zitachezwa jumamosi na jumapili ya tarehe 15 na 16 mwezi wa pili.

Mshindi wa mechi kati ya Fulham ama Sheffield United atapambana na mshindi kati ya Nottingham Forest au Preston kwenye hatua ya raundi ya tano ya kombe hilo ambalo fainal yake itachezwa kwenye uwanja wa Wembley.
Droo kamili ni kama ifuatavyo;
Manchester City v Chelsea
Sheffield United au Fulham v Nottingham Forest au Preston North End
Arsenal v Liverpool
Brighton & Hove Albion v Hull City
Cardiff City v Wigan Athletic
Sheffield Wednesday v Charlton Athletic
Sunderland v Southampton
Everton v Swansea City

Sunday 26 January 2014

Dada zetu badiliken hii ni Dunia ya Digital

Siku hizi dada zetu wengi wanamiliki magari. Ujio wa mabenki na utolewaji wa mikopo imewafanya dada zetu wengi kumiliki magari na hivyo kuondokana na usumbufu wa kuparamia daladala.

Lakini kuna tatizo moja ambalo nimeligundua kwa baadhi ya dada zetu wanaomiliki magari, usije ukaona Mdada ameshuka ndani ya gari lake amependeza ukadhani na gari lake ni nadhifu, utakuwa unajidanganya, hebu lisogelee kisha uchungulie ndani utashangaa.

Yaani utakuta gari hilo limegeuka kama nyumba:

Humo humo utakuta kuna containers za kubebea vyakula, na huenda ukakutana na left overs a.k.a kiporo ambacho kinasubiri kupashwa moto kwenye microwave ya ofisini.

Humo humo utakuta Wardrobe yaani ndani ya gari utakutana na pair kadhaa za viatu, mikoba, pair kadhaa za mawani, make ups, mateitei, Magagulo, shumizi na vikorokoro vingine.....

Mimi huwa najiuliza kama hiyo ni nyumba au ni gari.

Msije mkanitia vidole vya macho, naomba mjirekebishe.........

Jorge Mendez: Wakala aliyeanzia kuuza baa sasa anapiga fedha chafu kupitia kwa kina Ronaldo

AS Monaco iliweka mezani kwake Pauni 10 milioni kuhakikisha anamshawishi Cristiano Ronaldo hadi anatua klabuni kwao. Lakini, Real Madrid ikamwambia atavuna pesa nyingi zaidi kama atamfanya staa huyo wa Ureno asaini mkataba mpya wa kubaki Santiago Bernabeu.

Akatazama masilahi, akamshawishi Ronaldo asaini na kubaki Bernabeu. Huyo ni Jorge Mendes, wakala makini wa wanasoka mwenye hadhi kubwa duniani.

Wakati hilo likitokea, Mendes, tayari alikuwa ameweka kibindoni pesa za maana kwa kuwezesha uhamisho wa wachezaji James Rodriguez, Joao Moutinho, Radamel Falcao na kocha Jose Mourinho.

Baada ya kufanikiwa kuliteka soka la Ureno kwa muda mrefu, Mendes amejijengea umaarufu mkubwa kwa wachezaji na makocha na hivyo kukubali kuwa chini yake.

Mendes, ambaye jina lake halisi Jorge Paulo Agostinho Mendesm alizaliwa Januari 7, 1966 huko Lisbon, Ureno anazungumza Kiingereza, Kifaransa, Kitaliano na Kihispaniola kwa ufasaha mkubwa. Anatembea na lundo la simu na shughuli yake inamfanya kulala saa chache sana.

Mendes mtaji wake ni wachezaji na anawamiliki zaidi ya wachezaji 100 wenye thamani zaidi ya Euro 500 milioni. Anavuna mamilioni ya pesa kila mwaka. Mendes ni tajiri mwenye pesa za maana.

Jinsi anavyopiga pesa

Mendes anamiliki kampuni yake ya uwakala wa wachezaji, GestiFute ambayo aliianzisha mwaka 1996. Wanasoka anaowamiliki ni Jose Mourinho, Luiz Felipe Scolari, Carlos Queiroz, Simao Sabrosa, Anderson, Fabio Coentrao, Pepe, Angel Di Maria, Cristiano Ronaldo, Radamel Falcao Garcia, Ricardo Carvalho, Nani, Ricardo Quaresma, Burak Yilmaz, Joao Moutinho, James Rodriguez, David de Gea na Victor Valdes Joao Pedro Oliveira.

Kwa kuwamiliki tu wanasoka hao unaweza kuona fursa za kipesa ambazo wakala huyo anakabiliana nazo. Mendes pia ndiye mtu aliyewafanya Wareno Ronaldo, Carvalho na Nani kupata mafanikio makubwa nje ya uwanja.

Dili lake la kwanza la uhamisho lilikuwa la Nuno wakati alipohama kutoka Vitoria de Guimaraes na kutua Deportivo de La Coruna. Alikutana na kipa huyo kwenye baa huko Guimaraes na uhamisho huo ulimpa heshima na kuwanasa wachezaji wa Kireno akiwamo Jorge Andrade.

Hugo Viana alipohama kutoka Sporting kwenda Newcastle United kwa Euro 12 milioni mwaka 2002, huo ulikuwa uhamisho wake wa kwanza mkubwa wa kimataifa na baada ya hapo akawahamisha Cristiano Ronaldo na Ricardo Quaresma.
Mwaka 2004, alimhamisha Mourinho kutoka FC Porto na kutua Chelsea, uhamisho huo ulimwingizia pesa nyingi. Dili hilo lilimpa pesa nyingi kwa sababu awali Mourinho aliripotiwa kutua Liverpool.

Chelsea walinogewa na Mendes na kumpatia pesa za maana baada ya kufanikisha pia uhamisho wa wachezaji Ricardo Carvalho, Paulo Ferreira, Tiago na Maniche klabuni hapo. Kwenye dili hizo, Mendes alivuna pesa pande mbili kutoka kwa wachezaji na klabu ya Chelsea.

Kampuni yake inamiliki haki za kiuchumi za wanasoka hao. Mwaka 2014, aliiuzia FC Porto asilimia 20 ya hisa ya umiliki wa mchezaji Deco na hilo limemfanya kuingiza Euro 2.25 milioni na asilimia tano ya hisa za Ricardo Carvalho na Paulo Ferreira.

Baadaye, GestiFute ilipiga bei hisa nyingine 15 za Deco na kuingiza Euro 1.25 milioni na hisa asilimia 10 za straika Benni McCarthy. Kwenye uhamisho wa Ferreira na Thiago, Mendes aliingiza Euro 2.9 milioni na Euro 2.25 milioni ikiwa pamoja na gharama za afya za wachezaji hao na gharama nyingine za mahitaji yao ya nje ya uwanja.

Mendes alivuna Pauni 4 milioni kwenye uhamisho wa Anderson alipotoka Porto kuhamia Man United sawa na kiwango alichovuna mwaka 2009 kwenye uhamisho wa Ronaldo kwenda Real Madrid kwa Pauni 80 Milioni.

Wakala huyo alifunga Euro 3.6 milioni pia kwenye uhamisho wa Bebe alipotua Man United.

Agombana na wakala wa Figo

Mendes alijikuta kwenye ugomvi mkubwa Uwanja wa Ndege wa Portela mjini Lisbon, Ureno dhidi ya wakala wa Luis Figo, Jose Veiga, baada ya kuona umaarufu wake unafunikwa.

Mwaka 2011 kampuni ya Mendes ya Gestifute ilijikuta kwenye ugomvi mkubwa na Kampuni ya Formation inayoongozwa na wakala wa Wayne Rooney, Paul Stretford. Formation ilipeleka kesi mahakamani ikiishtaki Gestifute kwa kucheza rafu kwenye uhamisho wa wachezaji nchini England.

Mendes aliingia kwenye ugomvi na mawakala wenzake kutokana na umahiri wake wa kudaka dili safi na wanasoka wake mara zote amekuwa akiwahamisha kwa pesa za maana na kuhakikisha wanavuna mishahara minono ili kuendelea kupata faida.

FC Porto ilipomuuza Falcao kwenda Atletico, GestiFute ilivuna Euro 3.7 Milioni, pesa ambazo zilimnufaisha Mendes moja kwa moja.
Mendes alikuwa mwanasoka, lakini hakuwa na bahati kwenye hilo baada ya kukataliwa na klabu mbalimbali za Ureno kipindi hicho alikuwa na umri wa miaka 20.

Baada ya kukwama kwenye soka kama mchezaji, Mendes alifungua sehemu ya kukodisha kanda za video kabla ya kufanya kazi kama DJ na baadaye alifungua baa na klabu ya usiku huko Caminha.

TWIGA STAR inatia huruma jamani

TIMU ya soka ya taifa ya wanawake ‘Twiga Stars’ inacheza mechi yake ya kwanza ya mchujo wa kuwania kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake dhidi ya Zambia Februari 15 mwaka huu, lakini hali ya maandalizi ya timu hiyo inatia aibu.

Kocha wa timu hiyo, Rogasian Kaijage aliteua wachezaji 30 ambao wanaendelea na mazoezi yao kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam wakisubiri kuingia kambini keshokutwa Jumatatu kwenye kambi ya jeshi iliyopo Ruvu, Pwani.

Lakini kwa hali ilivyo kwenye timu hiyo tangu ianze mazoezi hakuna dalili yoyote ya umakini wa timu ya taifa inayojiandaa kwa mashindano.

Mpaka sasa benchi la ufundi limepwaya, halina kocha wa makipa licha ya umuhimu wa kocha huyo na badala yake makipa wenyewe ndiyo hupeana mazoezi baada ya kumaliza mazoezi yao ya kawaida.

Benchi hilo lina kocha mkuu na msaidizi wake, Nasra Juma ambaye mpaka sasa hajaanza kazi, daktari wa timu hiyo, Christine Lwambano, mtunza vifaa na meneja wa timu hiyo, Furaha Francis.

Mazoezi hufanyika Uwanja wa Karume, kila siku jioni lakini yamekuwa yakisuasua kwani si wachezaji wote wanaofika kwa muda unaopangwa kutokana na hali ya kiuchumi.

“Wachezaji wanatoka nyumbani, kuna shida ya usafiri na wengine huwezi kujua matatizo ya familia zao hivyo ni vigumu kumchukulia mchezaji hatua labda wangekuwa kwenye kambi ya pamoja, huwa nazungumza nao tu,” anasema Kaijage ambaye analalamika hajaridhishwa na hali ilivyo lakini hana jinsi.

“Ngoja tuone itakavyokuwa kwani tulitakiwa kuanza kambi mapema, niliwapa mapema programu yangu, haya mashindano ni makubwa na mchezo huo ni mgumu,” anasema Kaijage na kuongeza kuwa hata wachezaji wake hawafurahii hali inavyokwenda.

Nahodha wao, Sophia Mwasikili anasema: “Wanachoka ila tunajitahidi kuzungumza nao ili wasikate tamaa, mechi na Zambia ni ngumu lakini naamini tutaingia kambini wiki ijayo na tutafanya vizuri tu.”

Kipa namba moja wa kikosi hicho Fatuma Omary anayetoka timu ya Sayari Queens ndiye hupewa jukumu la kuwanoa makipa wenzake watatu Maimuna Seif, Belina Julius na Najiat Abbas kutokana na uzoefu wake ingawa bado wadau wamedai kwamba Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) haliko makini na timu hiyo.

Daktari wa Twiga, Christine Luambano, anasema kwamba wachezaji wawili Flora Kayanda na Semeni Abeid ni wagonjwa hivyo watakuwa nje mpaka watakapopona.

“Flora anaweza kuanza mazoezi Jumatatu ila Semeni bado sana kidonda chake kitachukuwa muda kidogo.”Kipa Maimuna Said na Eto Mlezi ambao wote wanatoka timu ya JKT bado hawajaripoti mazoezini, bado hawajapewa ruhusa na mwajiri wao.

TFF haiweki wazi tatizo linaloikabili Twiga Stars zaidi ya kusisitiza kwamba lipo nje ya uwezo wao.

Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura anasema: “Kambi ilitakiwa ianze Jumatano kama tulivyotangaza lakini kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu tuliamua kuisogeza ila wataingia kambini.”

Upinzani wapata afueni UKRAINE

Shinikizo zamfanya Rais Victor Yanukovych kujumuisha upinzani katika serikali yake

Rais wa Ukraine Victor Yanukovych ameupa upinzani baadhi ya nyadhfa muhimu za serikali katika juhudi za kumaliza maandamano ambayo yamekuwa yakiendelea nchini humo kwa majuma kadhaa sasa.

Lakini viongozi hao wa upinzani wamesema kuwa hawako tayari kuchukua nyadhfa hizo huku makabiliano kati ya waandamanaji na polisi yakiendelea katika mji mkuu wa Kiev.

Kiongozi wa chama cha Ukrain Fatherland Arseniy Yatsenyuk amesema kwamba yeye na viongozi wengine wa upinzani wako tayari kuichukua serikali,lakini akasisitiza kuwa uamuzi huo utafanywa na wapiga kura na wala si rais.

Muhariri wa maswala ya kibiashara katika gazeti la Kiev post Mark Rechkevych amesema kuwa wapinzani hao hawakutaka kuhalilisha mamlaka ya rais huyo.

Upinzani umekuwa ukisisitiza kufanyika kwa uchaguzi wa mapema.

Wakati huohuo waandamanaji wamelizunguka jumba moja mjini Kiev ambapo polisi wa kukabiliana na ghasia wamewekwa.