Thursday, 23 January 2014

man city ya toa onyo, FA ya tinga fainali

TIMU ya Manchester City, imepenya hatua ya fainali ya kuwania Kombe la Ligi kwa mara ya kwanza kwa zaidi ya miaka 38, baada ya kuilaza West Ham kwa jumla ya mabao 9-0.
Katika mechi ya raundi ya kwanza Manchester City, iliinyuka West Ham mabao 6-0 kabla ya kuinyeshea mabao 3-0 juzi.
Alvaro Negredo aliifungia Man City bao la kwanza na la pili kabla ya Sergio Aguero kuongeza la tatu katika mechi hiyo ya juzi.
Manchester City sasa itachuana na Manchester United au Sunderland katika fainali itakayochezwa katika Uwanja wa Wembley machi 2 mwaka huu.
United jana usiku waliwakaribisha Sunderland katika hatua ya nusu fainali ya pili na watakuwa na kibarua kigumu, kufuzu kwa fainali hizo baada ya kulazwa kwa mabao 2-1 katika awamu ya kwanza.
Mapema mwezi huu kocha wa Manchester City, Manuel Pellegrini alisema watajaribu kushinda mataji yote manne wanayopigania kwa sasa, Kombe la Ligi Kuu, FA, Kombe la Ligi na Klabu Bingwa Ulaya.
Post a Comment