Friday 24 January 2014

B’moyo wapasua bomba


SHARE THIS STORY
0
inShare

Chalinze. Watu wasiojulikana wilayani Bagamoyo, wamepasua bomba kuu la kupeleka maji katika Vijiji vya Msolwa, Mindutulieni na Chamakweza.

Kitendo hicho kimesababisha hasara kubwa ya mamilion ya fedha na wananchi kuathirika kwa kukosa huduma za maji.

Akizungumza mbele ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya hiyo, mmoja ya wakazi wa Kijiji cha Chamakweza, Paul Samwel, tukio hilo limedumu kwa wiki moja sasa.

Alisema hata hivyo watu waliofanya uharibifu huo lazima watakuwa ni wakazi wa vijiji hivyo na kwamba wamefanya hivyo kutokana na hasira za kutopata huduma ya maji kwa wakati bomba hilo likipita katika makazi yao.

“Ni kweli tuna tatizo kubwa la kukosa huduma za maji safi huku tukiwa tunaona bomba linapita katika ardhi ya kijiji chetu kwenda Ruvu.

Nadhani hali hiyo ndiyo imekuwa ikiwakera sana wananchi na hatimaye kufikia uamuzi wa kuharibu bomba,” alisema Samweli.

Akizungumza katika vikao vya usuluhishi, Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya ya Bagamoyo, Ahmed Kipozi, aliwataka wananchi kuacha nara moja vitendo vya kuharibu miundombinu ya maji.

Alisema Serikali haitasita kuchukua hatua za kisheria dhidi ya watakaothibitika kufanya hujuma hizo. Alisema hiyo ni hasara kubwa kwa Serikali

No comments: