Friday 24 January 2014

Rais Catherine Samba-Panzi aapishwa

Kaimu rais mpya wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Catherine Samba-Panza aapishwa mjini Bangu

Mashahidi wanaripoti uporaji mkubwa wa mali katika mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, huku kaimu rais mpya akianza rasmi kazi yake.

Mwandishi wa VOA Nick Long amabye yuko mjini Bangui, ameiambia Sauti ya Amerika kuwa maelfu ya watu walipora mali katika eneo linalojulikana kama PK13 lenye wakazi wengi Waislam.

Anasema majeshi ya Rwanda yaliwafukuza waporaji, lakini uporaji ukaanza tena baada ya walinda amani hao wa Rwanda kuondoka, kulinda sherehe za kuapishwa kwa kaimu rais mpya.

Rais huyo mpya wa muda Catherine Samba-Panza, ametoa mwito wa utulivu wiki hii kabla ya sherehe za kuapishwa kwake, ambako kumefanyika katika majengo ya bunge leo Alhamis

No comments: