Friday, 24 January 2014

Mtoto aliyepigwa hadi kufariki

Pemba. Mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja (jina tunalo) mkaazi wa Junguni Gando aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Wete akipatiwa matibabu baada ya kupigwa na baba yake mzazi kutokana na utofauti wa sura zao, amefariki dunia siku ya Jumatano alfajiri saa10.30 .

Taarifa zilizopatikana na kuthibitishwa na Daktari wa Wodi ya Watoto wa hospitali hiyo, Sada Juma Mbwana zinasema, mtoto huyo amefariki dunia kutokana na majeraha aliyoyapata.

“Mtoto alipofikishwa hospitalini tuliambiwa kwamba anasumbuliwa na kifua (anakohoa) lakini mambo yalikuwa mengine baada ya Polisi kufika wakiwa na PF3 na ndipo mama mzazi alipoeleza mwanawe amepigwa na baba yake,” alifahamisha Sada

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba,Shakhan Mohammed Shakhan amesema baba mzazi wa mtoto huyo anashikiliwa kutokana na tuhuma za kujeruhi,anatarajia kufikishwa mahakamini Jumatatu ijayo.
Post a Comment