Kocha wa zamani wa Simba, Jamhuri Kihwelo Julio ambaye yupo kwenye mipango ya kufundisha timu ya Mwadui FC.
KOCHA msaidizi wa zamani wa Simba, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, ameitwa katika kuinoa timu ya Mwadui FC inayoshiriki ligi daraja la kwanza, huku akisubiriwa kwa hamu kuona timu hiyo inapata tiketi ya kucheza Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
Habari zilizotufikia katika chumba chetu cha habari zinasema kuwa tayari Julio ameshawasili katika timu hiyo kwa ajili ya kuanza taratibu za kuinoa timu hiyo.
Julio alikuwa kocha msaidizi wa Simba, hata hivyo alienguliwa akiwa sambamba na kocha wake mkuu, King Abdallah Kibadeni, jambo linalomuumiza kichwa hadi leo.
Akizungumza kwa njia ya simu, Julio alisema kuwa ni mapema mno kuelezea maisha yake ya soka, ikiwa ni miezi michache tangu alipoenguliwa Simba kwa mizengwe.
“Naomba wadau wasiwe na haraka na mimi katika maisha yangu ya soka ndani na nje ya nchi, maana kama hizo habari za mimi kuinoa Mwadui zitakuwapo, basi kila mmoja atajua.
“Ni kweli nipo mkoani Shinyanga kwa mambo yangu binafsi, ila si kuinoa timu hiyo ya Mwadui kwakuwa ni mapema mno kutolea ufafanuzi jambo kama hilo, ukizingatia kuwa bado nina uchungu wa kusimamishwa timu ya Simba kwa mizengwe,” alisema Julio.
Kwa mujibu wa mtoa habari wetu, Julio Mameanza kuridhishwa na kiwango cha wachezaji wake mbali ya kutoa suluhu ya pili katika mechi za ligi kuu Tanzania Bara.
No comments:
Post a Comment