Sunday 26 January 2014

Nafasi ya nne si ya simba kamwe

Benchi la ufundi la klabu ya Simba limesema kuwa limesema 'litapigana' kuhakikisha linaitoa timu kwenye nafasi ya nne iliyopo sasa kwenye msimamo wa ligi na kuipandisha juu zaidi.
suleman matola

Kocha msaidizi wa Simba, Seleman Matola, amesema kuwa benchi la ufundi limejiwekea malengo maalum na moja wapo ni kuhakikisha timu inarudi nafasi za juu zaidi katika kipindi kifupi.

"Nafasi ya nne si ya chini sana, lakini kwetu kushika nafasi hiyo inatuuma na tutahakikisha timu inarudi nafasi za juu zaidi mapema iwezekanavyo...., najua ni changamoto ngumu kutokana na ukweli kuwa na wapinzani wetu wa juu wamejiandaa na hawatakuwa tayari kushuka ila na sisi tumejipanga," alisema Matola.

Aidha, Motola alisema kuwa kikosi chake kwa sasa wanaelekeza nguvu kwenye ligi kuu na wamepania kuhakikisha wanapata matokeo mazuri.

"Akili yetu kwa sasa ipo kwenye mzunguko wa pili, hatuna hofu na wachezaji wetu wapo tayari kupambana na tutaonyesha tunachokitaka kwenye mchezo wa Jumapili," alisema Matola aliyechukua mikoba ya Jamhuri Kiwhelu 'Julio'.

Alisema kuwa wachezaji wote wako fiti isipokywa beki wa kushoto Saidi Nassoro 'Cholo' ambaye bado ni majeruhi na hawezi kucheza katika mchezo wa kesho dhidi ya Rhino Rangers ya mkoani Tabora.

Mbali na Cholo, pia wekundu hao watamkosa kiungo aliyekwenye kiwango chake cha juu, Jonas Mkude ambaye anasumbuliwa na homa ya matumbo (Typhod).

Kwenye mchezo wa kwanza wa timu hizo kwenye mzunguko wa kwanza, Simba ililazimishwa sare ya kufungana magoli 2-2 kwenye uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.

No comments: