Aguero apiga Hart trick
Magoli matatu ya Sergio Aguero na moja la Kolarov kwenye uwanja wa Etihad, yameisaidia Manchester City kuvuka raundi ya nne ya michuano ya kombe la FA.
Shuti dogo la Fernando Forestieri lililozaa goli na lile la Troy Deeney yaliifanya Watford kuongoza hadi kipindi cha kwanza kinamalizika katika matokeo ambayo hayakutarajiwa na wengi katika mechi hiyo ambayo City walipanga kikosi mchanganyiko.
Ilikuwa ni mechi ambayo iliwachukua Man City saa moja kuweza kuziona nyavu za uwanja wao wa nyumbani pale Aguero alipomalizia krosi ya Aleksandar Kolarov.
Baadaye Aleksandar Kolarov tena aliachia shuti kali ambalo lilimshinda kipa wa Watford Jonathan Bond kabla ya Aguero hajautumbukiza mpira wavuni na kufanya matokeo kuwa 2-2 dakika ya 79.
Wakati Watford wakijuliza namna ya kurejesha mabao hayo Aleksandar Kolarov aliifungia bao la tatu Man City kwa shuti kali nje ya eneo la hatari na kuweka matumaini ya miamba hiyo ya Kaskazini mwa kisiwa cha England kuuendelea na mbio zao za kunyakuwa taji la FA msimu huu.
Ni Aguero kwa mara nyingine aliyeibuka shujaa wa mchezo kwa Man City baada ya kupiga kichwa mpira uliomkuta upande wa kushoto wa eneo la ndani ya kumi na nane,krosi pasi nzuri kutoka kwa Jesus Navas.
Liverpool waliifunga Bournemouth kwa mabao mawili kwa bila, mabao ya Victor Moses na Daniel Sturridge.
Katika mchezo huo, kocha wa Liverpool Brendan Rogers alishusha kikosi kamili cha majogoo wa Anfield katika mchezo huo wa ugenini.
Katika michezo mingine, Birmingham ilikubali kichapo cha mabao1-2 kutoka kwa Swansea.
Bolton wao wakiwa nyumbani walilala kwa 0-1 dhidi ya Cardiff bao likifungwa na Fraizer Campbell kinda la zamani wa Manchester United.
Huddersfield ikafungwa 0-1 na Charlton.
Port Vale yenyewe ililala 1-3 mbele ya Brighton.
Rochdale ikafungwa na Sheff Wed1 - 2 katika mchezo uliokuwa mgumu.
Southampton imeifunga Yeovil 2-0 na kujihakikishia tiketi ya kucheza raundi ya tano ya michuano ya kombe hilo la FA.
Southend timu kutoka maeneo ya karibu na pwani ya England yenyewe ilikubali kichapo cha 0-2 kutoka kwa Hull.
Wakati Sunderland ambao wamekwishajikatia tiketi ya kucheza fainal ya kombe la ligi baada ya kuitoa Manchester United kwenye nusu fainal, wao waliichapa Kidderminster 1-0 kwenye uwanja wa Stadium of Light.
Wigan timu iliyoshuka daraja msimu uliopita yenyewe ilionyesha makali yake na nia yao ya kurejea ligi kuu kwa kuitandika Crystal Palace 2-1.
NA Everton wakiwa ugenini waliiadhibu Stevenage kwa kuichapa mabao 4-0 kwenye uliokuwa mwepesi kwa kikosi cha Roberto Martnez.
No comments:
Post a Comment