Friday 31 January 2014

35 wauawa CAR mapigano yakichacha

Rais mpya wa muda nchini CAR, Catherine Samba Panza

Kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu imesema kuwa watu 35 wameuawa katika mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Bangui katika kipindi cha siku tatu zilizopita

Msemaji wa kamati hiyo ya Red Cross mjini Bnagui ,Nadia Dibsy,amesema kuwa mji huo sasa unakumbwa na vita vibaya.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Associated Press, miili ilionekana ikiwa imekatakatwa kwa mapanga na kutapakaa kote.

Vita inasemekana vimekithiri huku wanajeshi 1,600 wa Ufaransa na wengine 5,000 wa Muungano wa Afrika wakiwa nchini humo kujaribu kutuliza hali.

Mgogoro wa kisiasa ulianza mwezi Machi mwaka jana kutokana na mapinduzi ya kijeshi yaliyotokea wakati huo ambapo waasi waisilamu walimsaidia aliyekua Rais Djotodia kuingia mamlakani kwa nguvu.

Tangu hapo vita vimekuwa vikichacha kati ya waasi waisilamu na wakristo.

Na sasa kwa kuwa waisilamu wameondoka mamlakani, wakristo nao wameanza kulipiza kisasi.

No comments: