KLABU ya Manchester City, juzi imeinyuka Blackburn Rovers mabao 5-0 katika
mechi ya Kombe la FA.
Kwa matokeo hayo Manchester City, imepata nafasi ya kucheza mzunguko wa nne wa michuano hiyo, ambapo sasa itakutana na
Warford.
Katika mechi hiyo mshambuliaji raia wa Argentina, Sergio Aguero dakika ya 73 alipachika bao lake la kwanza tangu kurejea uwanjani akitokea kutibu majeraha ya mguu
yaliyokuwa yakimsumbua.
Mshambuliaji huyo wa Argentina amekuwa nje ya uwanja kutokana na maumivu ya mguu, lakini aliingia kipindi cha pili na kuwasha moto wa mabao.
Hadi mshambuliaji huyo anaingia uwanjani tayari, Manchester City walikuwa wakiongoza kwa mabao 3-0 baada ya Alvaro Negredo, kupachika mabao mawili dakika za 45 na 47 huku, Edin Dzeko akipachika bao dakika ya 67.
Baada ya Aguero kupachika bao wavuni, dakika ya 79 Dzeko, aliunganisha vizuri krosi ya Jesus
Navas na kufunga bao lake la pili.
Ulikuwa ni ushindi mwingine mnono wa vijana hao wa Manuel Pellegrini, ambao walitoka sare ya bao 1-1 katika mchezo wa awali uliopigwa Uwanja wa Ewood Park.
Timu hiyo sasa imefunga jumla ya mabao 99 katika mashindano yote msimu huu.
No comments:
Post a Comment