Saturday 23 April 2016

Msomi avua nguo kwa kufungiwa ofisi

Stella Nyanzi alikuwa akimuunga mkono mgombea urais Kizza Besigye
Hatua ya mwanamke mmoja msomi ya kuvua nguo nchini Uganda imezua mjadala mkali nchini humo.
Baada ya kukerwa na hatua ya kufungiwa nje ya ofisi yake na usimamizi wa chuo kikuu cha Makerere, Stella Nyanzi alivua nguo zote kama njia ya kupinga.
Hata hivyo mwishowe aliruhusiwa kuingia ofisini mwake. Wengi wa wafuasi wake wanasema kuwa alilazimishwa kufanya hivyo kutoka na yake alikuwa akitendewa.
Hata hivyo wale wanaomkosoa wanasema kwa amekiuka maadili na kwamba mwanamke hastahili kuwa uchi hadharani.

Chris Brown : Nilitaka kujiua kisa Rihana

Nilitaka kujiua kwa sababu ya Rihanna
Mwanamuziki Chris Brown amesema kuwa alitaka kujiua baada ya kumshambulia aliyekuwa mpenziwe Rihanna kabla ya tuzo za Grammy mwaka 2009.
Katika kipande kifupi cha makala yake ya 'Karibu katika maisha yangu',mwanamuziki huyo wa mtindo wa R & B amesema kuwa uhusiano wao ulikuwa kama ndoto lakini akajihisi kama hayawani.
''Nilikuwa katika kilele cha dunia,nyimbo zangu zikiongoza,nikapendwa na wengi nchini Marekani kabla ya kuanguka hadi kuwa adui wa uma'',alisema.
 
Chris Brown na Rihanna
Brown alihukumiwa kifungo cha miaka mitano jela kufuata shambulio hilo.
Kifungo hicho kilisitishwa mwaka jana baada ya jaji moja kusema kuwa nyota huyo amekamilisha mahitaji yake yote na kufunga kesi hiyo rasmi.
 
Rihanna
Makala hiyo inayowaonyesha Jennifer Lopez,Usher,Mike Tyson,Jamie Fox na Rita Ora,Chris Brown anasema kuwa ''Nilihisi kama nyota ,lakini nilijiharibia''.
''Nilikuwa nikilala.Sikuweza kula,nilijihisi maarufu'',alikiri.

matokeo ya Epl leo

Man City
Manchester City imepanda hadi nafasi ya tatu katika jedwali la ligi ya Uingereza baada ya kuicharaza Stoke City 4-0 huku ikitarajiwa kumenyana ana Real Madrid katika kombe la vilabu bingwa Ulaya siku ya Jumanne.

Marehemu ateuliwa kuchezesha mechi

NFFShirikisho la Soka la Nigeria linakabiliwa na mzozo wa uongozi
Mwanamume aliyefariki ameteuliwa kusimamia mechi ya soka nchini Nigeria ambayo itachezwa Jumapili, mwandishi wa BBC anayefuatilia masuala ya soka Oluwashina Okeleji anasema.
Wale Akinsanya aliteuliwa kuwa mwamuzi kwenye mechi baina ya Warri Wolves na Giwa FC katika mji wa Warri kusini mwa Nigeria, gazeti la Punch la Nigeria limeripoti.
Hii ni licha ya kwamba Akinsanya alifariki tarehe 22 Januari 2016 wakati wa kufanywa kwa mtihani wa Fifa Cooper Test, ambao hutumiwa kuamua iwapo marefarii wanatosha kuendelea kusimamia mechi.
Aliteuliwa kusimamia mechi hiyo na mrengo wa Shirikisho la Soka la Nigeria (NFF) unaoongozwa na

Mcheza mieleka na filamu za ngono afariki dunia

Mcheza miereka na nyota wa filamu za ngono Chyna afariki
Aliyekuwa mchezaji miereka na nyota wa filamu za ngono Chyna amefariki akiwa na umri wa miaka 45.
Meneja wake amethibitisha habari hiyo kupitia mtandao wake wa Twitter.
''Ni masikitiko makubwa kutangaza kwamba tumempoteza shujaa'',ulisema ujumbe huo,akiongezea kuwa:Ataishi kukumbukwa na mashabiki wake wengi na sisi sote tuliompenda.
Chyna alipatikana amefariki nyumbani kwake katika ufukwe wa bahari wa Redondo,mjini California,baada ya kurudi nyumbani kutoka Japan.

Sunday 17 April 2016

Hans awaonya waandishi wanaomchonganisha na Yanga

Kocha mkuu wa Yanga amelalamika juu ya waandishi ambao wamekuwa wakiandika vitu ambavyo yeye hajazungumza kwasababu vinamletea matatizo na waajiri wake.
Hans amesema hivyo baada ya gazeti moja kutoa habari ambayo inasababisha mazingira magumu, anasema yeye ni mwajiriwa hivyo anatarati zake  za kazi na badala yake amewaomba waandishi kuchukua na kufanyia kazi kile ambacho anakuwa amekizungumza mwenyewe
“Mimi huwa zizungumzi kuhusu kuhusu makocha, timu nyingine wala TFF, kuna gazeti linasema mimi nilienda TFF kujaribu kubadilisha tarehe za baadhi ya mechi lakini kulikuwa hakuna uwezekano juu ya hilo kwahiyo nikawa nimekasirishwa na TFF na kuanza kuwashutumu kwamba hawajui kufanya mambo yao, sijawahi kuzungumza kuhusu federation watu wanatakiwa kujua hilo”, amesema Hans ambaye anaonekana kuchukizwa na habari hiyo.

MAGAZETI YA LEO


SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumapili ya April 17

Mrembo ajioa mwenyewe baada ya kukosa mchumba

Yasmin Eleby hakupata mchumba wa kumuoa mtu ambaye alitaka awe mume wake atakapofikisha miaka 40--kwa hivyo akafanya kitendo ambacho kimewashangaza wengi, aliamua kujioa mwenyewe.

Kwa mujibu wa mtandao wa MySanAntonio.com,Eleby aliahidi kwamba ikiwa hatapata mchumba wakati atakapokuwa ametimiza miaka 40, basi atafanya harusi ya mtu mmoja yaani atajioa ili kusherehekea miaka yake 40.

Saturday 16 April 2016

Yanga kuipiga mtibwa na kurejea kilelen ?


Yanga vs Mtibwa -znz 1

MECHI Tatu za ligi kuu Tanzania bara zinataraji kuchezwa Jumamosi na siku ya Jumapili. Mabingwa watetezi Yanga SC walio nafasi ya pili ya msimamo wakiwa na alama 56 watawakaribia Mtibwa Sugar ya Turiani, Morogoro iliyo nafasi ya nne na pointi 43.
Mchezo huu utapigwa katika uwanja wa taifa siku ya leo Jumamosi. Mchezo mwingine siku ya leo utawakutanisha Coastal Union ya Tanga iliyo mkiani mwa msimamo na alama 19 baada ya kucheza michezo 26.
Coastal watakuwa nyumbani ( Mkwakwani) kuwakaribisha JKT Ruvu ya Pwani katika pambano kali kuepuka vita ya kuteremka daraja. Kikosi cha JKT Ruvu chini ya kocha mzoefu, Abdallah ‘King’ Kibadeni kipo nafasi ya 13 kikiwa na alama 24 katika michezo 24 waliyo kwishacheza.
Siku ya Jumapili, viongozi wa ligi hiyo, timu ya Simba SC watawakaribisha Toto Africans ya Mwanza katika pambano lingine linalokutanisha timu zenye malengo tofauti. Simba ina pointi 57 baada ya kucheza michezo 24, wakati Toto iliyo nafasi ya 11 ina pointi 27.
YANGA V MTIBWA
Haitakuwa rahisi kwa Mtibwa kupata walau pointi moja mbele ya Yanga katika mchezo huu. Yanga itakuwa na nafasi ya kuishinda Mtibwa Sugar katika game zote mbili za msimu kwa mara ya kwanza tangu msimu wa 2008/09.
Mtibwa ilijijengea tabia ya kutopoteza mchezo katika uwanja wa Jamhuri, Morogoro tangu mwaka 2009. Lakini msimu huu walipoteza kwa kuchapwa 2-0 (Magoli ya Donald Ngoma na Malimi Busungu,) na wata cheza uwanja wa Taifa wakiwa na rekodi ya kupoteza michezo minne iliyopita ya VPL.
Yanga wanashindania taji na ushindi dhidi ya Mtibwa yenye uhakika wa kubaki top 5 na nafasi finyu ya kumaliza top3 utawafanya vijana wa Mkufunzi, Hans Van der Pluijm kurejea kileleni mwa msimamo baada ya kuenguliwa takribani mwezi mmoja uliopita na mahasimu wao Simba.
Yanga wamecheza michezo 23, baada ya mchezo wa Jumamosi hii watabakiwa na michezo minne tu kabla ya kumalizika kwa msimu. Baada ya timu yake kuishinda Mwadui FC wiki mbili zilizopita kocha wa Mtibwa, Mecky Mexime alisema kwamba ‘wanacheza ligi ili kupata kipato tu cha kuendeshea maisha yao kwa kuwa ligi inachezeshwa katika utaratibu mbaya kwa baadhi ya timu.
Mtibwa haitakuja kushindana na Yanga bali itakuja kukamilisha ratiba na kucheza mchezo wao. Mecky tayari alishasema hilo wiki kadhaa zilizopita na mtazamo wake huo ndiyo unanifanya niamini Yanga watashinda na kurejea kileleni kwa kuwa wao wanashindania ubingwa na itawabidi wapambane hadi siku ya mwisho ya msimu kutimiza malengo yao.  Yanga kuifunga Mtibwa mara mbili mfululizo itakuwa ni rekodi mpya na ngazi yao nzuri kuelekea juu ya msimamo.
COASTAL V JKT RUVU
Kikosi cha King kinakwenda Tanga kikiwa na rekodi ya kutoshuka daraja tangu walipopanda mwaka 2002. Ushindi utawafanya JKT Ruvu kupanda hadi nafasi ya 11 na kuwapeleka Toto Africans nafasi ya 12 (timu zote zitakuwa na alama sawa 27 ikiwa JKT Ruvu itashinda dhidi ya Coastal.)
Kupoteza mchezo huu kwa Coastal itakuwa ni sawa na kuanza safari yao katika ligi daraja la kwanza msimu ujao. Pointi 19 walizonazo na 12 wanazoposwa kuzikusanya katika game zao nne za mwisho itawafanya vijana wa kocha Ally Jangalu kufikisha alama 31-pointi ambazo hata kihesabu zinawanyima nafasi ya kucheza VPL msimu ujao.
Stand Unite tayari wana alama 34, Majimaji FC wana pointi 33, wakati timu za Ndanda SC na Mbeya City FC zenyewe tayari zimekusanya pointi 30 kila timu. Toto, Kagera Sugar, JKT Ruvu, JKT Mgambo, na African Sports ndiyo timu pekee zisizofikisha alama 30 hadi sasa.
Coastal tayari wamechelewa lakini wanaweza kujaribu kushinda game zao zote nne zilizobaki ili kusubiri atma yao mwisho wa msimu. Sare au matokeo ya kupoteza mchezo dhidi ya JKT Ruvu yatawashusha daraja japo haitakuwa rasmi.
SIMBA V TOTO
Mechi ya kwanza baina ya timu hizi ilimalizika kwa matokeo ya sare ya kufungana goli 1-1 katika uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza. Simba wanafahamu jinsi timu hiyo ya Mwanza inavyowasumbua kila wanapokutana, na ili kuendelea kugombea ubingwa kikosi cha Jackson Mayanja kinapaswa kushinda game hii siku ya Jumapili katika uwanja wa Taifa.
Toto inayoundwa na wachezaji wengi vijana waliopata kufanya vizuri katika timu ya Simba B itakuwa ikicheza mchezo wake wa 27 wa ligi, pia itacheza na Yanga wiki chache zijazo.
Kushindwa kupata walau alama moja dhidi ya Simba watakuwa wamejipeleka katika ‘shimo’ hivyo watalazimika kupambana kwa kuamini pointi moja katika kila mchezo ulio mbele yao ina faida kubwa kama hawatapata ushindi. Hii itakuwa mechi nyingine kali wikendi hii.

Friday 15 April 2016

EPL kuendelea wikend hii

LeicesterLeicester watakuwa nyumbani dhidi ya West Ham
Ligi kuu ya England inatarajiwa kuendelea tena wikiendi hii kwa michezo kadhaa, Jumamosi Norwich itaikaribisha Sunderland, Everton wao watakuwa wenyeji wa Southampton, Man Utd watakuwa wenyeji wa Aston Villa katika dimba la Old Traford , Newcastlle itamenyana na Swansea city, West Brom watawaalika Watford na Chelsea watakuwa darajani Stamford dhidi ya Manchester City.
Jumapili Vinara wa ligi Leicester city watakuwa nyumbani na West Ham,Bournemouthwatawaalika Liverpool na Arsenal itamenyana na Crystal Palace.

Thursday 14 April 2016

Zaidi ya shilingi Bilioni 900 zatumika kwa ajili ya miradi itakayo zindulia na Mwenge.

Mwenge wa Uhuru unanarajiwa kuwashwa Kitaifa mkoani Morogoro mapema April18 Mwaka huu ambapo zaidi ya bilioni Miatisa na Milioni Miatatu zimetumika kwa matumizi ya miradi 41 ambayo itazinduliwa huku mingine ikiwekwa jiwe la Msingi.
Akizungumza wakati wa kupokea msaada wa sare za nguo za kuvaa watoto kwenye Mwenge zilizo tolewa na benki ya NMB kanda ya Mashariki mkuu wa mkoa wa Morogoro Stephan Kebwe amesema maandalizi ya Mwenge yako vizuri na viongozi mbalimbali wakiwemo wakuu wa wilaya wa mejipanga kuhudhuria uzinduzi huo.
 Zaidi ya shilingi Bilioni 900 zatumika kwa ajili ya miradi itakayo zindulia na Mwenge.

Wanawake 2 vikongwe wameuawa kinyama wilayani Rorya mkoani Mara.

Wanawake wawilivikongwe wameuawa kinyama kwa kupigwa na kukatwakatwa kwa mapanga kisha miili yao kuchomwa moto katika kijijicha Kenyamsana wilayani Rorya mkoani Mara kwa tuhumu za kujihusisha na ushirikina,tukio ambalo limesababisha hofu kubwa kwa wanawake wengi wenye umri mkubwa katika kijiji hicho.
Wakizungumzia tukio hilo la kwanza kutokea wilayan Rorya, baadhi ya ndugu wa marehemu hao, wamesema kuwa kundi la watu waliwakamata wanawake hao vikongwe    kisha kuwapiga katika sehemu mbalimbali za miili huku wakiwaingiza kwa nguvu ndani ya nyumba zao ambazo zimeezekwa kwa kutumia nyasi na kuwachoma moto. 

Diamond: Nilimpeleka mama ulaya kuondoa ushamba

Amesema ameona kuwa mziki wa bongo fleva umekuwa mkubwa sana duniani kwani alijaza kumbi ambazo hata baadhi ya wanamuziki wa Marekani wakifika wanafanyia kule kwa sababu sio kila msanii wa marekani anaweza kujaza Arena hizo.

Video ya Boko Haram yaonesha wasichana wa Chibok

WasichanaWanachama wa vuguvugu la Bring Back Our Girls waliandamana mjini Lagos Jumatano kutetea kuachiliwa kwa wasichana hao
Kanda ya video iliyotumwa kwa maafisa wa serikali ya Nigeria kutoka kwa kundi la wapiganaji wa Boko Haram inaonesha baadhi ya wasichana waliotekwa eneo la Chibok wako hai.
Ni miaka miwili tangu kutekwa kwa wasichana 276 kutoka shule moja katika mji wa Chibok.
Ni wasichana 15 wanaoonekana kwenye kanda hiyo ya video ambayo inaaminika ilipigwa Siku ya Krismasi.
Video hiyo imepeperushwa hewani na shirika la utangazaji la marekani la CNN.

Saturday 9 April 2016

Mrema amwomba Mh Magufuli akumbuke ahadi yake ya kumpatia kazi


Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour (TLP) taifa, Augustine Mrema amemuunga mkono Rais John Mgufuli kwa kasi yake ya kupambana na ufisadi na kumuomba ampe kazi ili amsaidie kutekeleza jukumu hilo.

Mrema alimuomba Rais Magufuli atambue uzoefu wake kwa kukumbuka jinsi alivyopambana na mafisadi wakati akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Naibu Waziri Mkuu.

Huku akieleza CV yake hiyo, Mrema alimkumbusha Rais kuhusu ahadi aliyompa wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka jana, ya kumpa kazi katika Serikali ya Awamu ya Tano ikiwa atashinda na kuwa Rais.

Akizungumza na waandishi wa habari wa blog yet kijijini kwake Kiraracha mkoani Kilimanjaro, Mrema alisema kuwa anasikitishwa na ukimya wa Rais Magufuli kwa sababu aliamini kuwa angetekeleza ahadi hiyo ya kumpa kazi muda mfupi baada ya kutangaza Baraza la Mawaziri, jambo ambalo hadi sasa hajalifanya.

Alisema, alikutana na Rais Magufuli mwaka jana katika kampeni jimboni Vunjo kwenye eneo la Njia Panda lililopo ndani ya mji mdogo wa Himo na kuambatana naye kwenye mkutano wa hadhara, ambapo alimwombea kura kwa wafuasi wake na kuahidiwa ajira.

“Katika kampeni, Dk Magufuli alifika kwenye mkutano wangu nikamwombea kura kwa kuwaambia watu wangu wamchague kwa kuwa ni mchapakazi na mwadilifu. Aliahidi kunipatia kazi katika Serikali na sasa namkumbusha na kumuuliza mbona yupo kimya?” Mrema alieleza na kuhoji.
Alipoulizwa ni kazi gani inayomfaa katika Serikali ya Magufuli, alisema yeye alishawahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Naibu Waziri Mkuu hivyo yuko tayari kufanya kazi yoyote itakayomfaa ila alitamani zaidi kupangwa sehemu nyeti ili amsaidie kutumbua majipu.

Mrema alimpongeza Rais Magufuli kwa jitihada binafsi za kutumbua majipu anazozifanya na alijigamba kuwa yeye ndio mwenye uzoefu wa kupambana na mafisadi kutokana na rekodi yake nzuri ya kipindi cha Rais wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi.

Katika hatua nyingine, Mrema alikanusha taarifa ya kuhongwa fedha ili kufuta kesi ya kupinga matokeo aliyoifungua dhidi ya Mbunge wa jimbo hilo, James Mbatia.

Alisema, taarifa hizo ni za kupuuzwa kwa sababu zinalenga kumpaka matope kwa wananchi wake wa Vunjo.

Mrema alieleza kuwa walifikia maridhiano ya pamoja kuhusu kuondoa kesi hiyo mahakamani na kwamba, hilo lilifanywa kwa kuzingatia maslahi ya wananchi. 

Pamoja na hayo, alikiri kumlipa Mbatia Sh mil 40 ikiwa ni sehemu ya kupunguza gharama alizotumia katika kesi hiyo, ikiwemo malipo ya mawakili wake.

Fatuma Karume: Wanzanzibar wanaishi kama wanyama

Mwanadada jasri na aliyejizolea umaarufu hivi karibuni Fatuma Karume AMELIPUKA, unaweza kusema. Akihojiwa na DW amesema sasa Zanzibar wanaishi kama wanyama maana hawafuati katiba. "Kama wameamu kuondoa utaratibu tuliyojiwekea sasa tuna tofauti gani na wanyama?"
Alipoulizwa kama vitisho vya Ccm havimtishi na kama baba yake hamdhibiti, amesema. "Mimi siyo mbwa wala paka, nina haki yangu ya asili ya kujieleza na kutoa maoni" Amesema babake hawezi kuondoa uhuru wake kisa Ccm.

Ukweli Kuhusu utoboaji wa pua kwa diamond huu hapa

Kwa masaa kadhaa picha ya Diamond Plutnumz akiwa na kipini puani, imekuwa gumzo katika mitandao ya kijamii na kuwaacha mashabiki wake njia panda.

Mashabiki wengi walionekana kumkosoa kwa uamuzi wake wa kubandika kipini puani huku wengine wakionekana kuwa waelewa wa kile alichokifanya.

Swali ambalo linazunguka kwenye vichwa vya mashabiki na wapenzi wengi wa muziki je, ni kweli Chibu katoga pua yake?

Mtoto wa Kizza Besigye ashinda kiti cha urais Oxford Universty

AnslemAnslem alitayarisha video ya kuwaomba wanafunzi wenzake wampigie kura
Mwana wa kiume wa kiongozi wa upinzani nchini Uganda Dkt Kizza Besigye amechaguliwa kuwa rais wa chama cha mijadala chuo kikuu cha Oxford.
Anslem Besigye alikuwa ametengeneza video fupi ya kuomba wanafunzi wenzake wampigie kura.
Mamake Winnie Byanyima amefurahia ushindi wa mwanawe na kuandika kwenye Twitter: “Ameshinda! Anslem amechaguliwa rais wa chama cha mijadala katika bewa lake. Najionea fahari kama mamake.”
Kwenye video aliyokuwa ameitengeneza alikuwa amesimulia mambo ambayo amefanyia chama hicho na uzoefu wake katika mijadala.

Wednesday 6 April 2016

Aliyekuwa nyota wa filamu za ngono Meghan Wren amefariki akiwa usingizini

Aliyekuwa nyota wa filamu za ngono Meghan Wren
Aliyekuwa nyota wa filamu za ngono Amber Rayne amefariki nyumbani kwake mjini Los Angeles ,maafisa wamethibitisha.
Marafiki na waliokuwa wafanyikazi wenzake walituma ujumbe katika mtandao wa Twitter wakimuenzi mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 31 ambaye alifariki usingizi wikendi iliopita.
Amber alikuwa nyota wa filamu za ngono kwa muongo mmoja kabla ya kujiuzulu mwaka 2015.
Alikuwa miongoni ,mwa kundi moja la wanawake ambao walidai kwamba James Deen,ambaye pia ni nyota wa filamu za ngono alimshambulia.

Mapigano ya Kikabila yazuka Kaskazini Mashariki mwa Ivory coast


Mapigano ya kikabila nchini Ivory Coast
Raia 12 wa Burkina Faso wameripotiwa kupoteza maisha kwenye mapigano ya kikabila yaliyozuka katika mji wa Bouma ulioko kaskazini mashariki mwa Ivory Coast.
Serikali ya Ivory Coast ilitoa maelezo na kubainisha kuuawa kwa raia 12 wa Burkina Faso kwenye mapigano huku wengine 1,550 wakilazimika kurudi nchini kwao.
Kwa upande mwengine, serikali ya Burkina Faso imewataka viongozi wa Ivory Coast kuwahakikishia usalama raia wake pasi na kuvunja udugu uliokuwepo kati ya nchi hizo jirani.
Mapigano hayo yanaarifiwa kuanza tangu wiki jana baina ya jamii za Peulhi, Lobi na Koulango mjini Bouna.

Mtu Aliyeungua na Moto Hadi Kufa Kwenye Gari Mbezi Ajulikana..Mi Mhadhiri wa Chuo Kikuu Dar es Salaam


Mhadhiri  wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Idara ya Sayansi na Uhandisi wa Kompyuta (CoICT), Dk Richard Mgaya amefariki baada ya teketea ndani ya gari lake jijini Dar es Salaam juzi.
Gari la Dk Mgaya liliteketea baada ya kugongana na lori katika eneo la Mbezi Africana, Wilaya ya Kinondoni usiku wa kuamkia juzi na kuwaka moto uliosababisha kifo chake.
Juzi picha mbalimbali zilisambaa zikionesha gari aina ya Toyota Prado lililopata ajali eneo hilo la Africana baada ya kugongana na lori, baadaye ilibainika kuwa aliyekuwa katika gari hilo ni Dk Mgaya.
Akizungumza  kwa njia ya simu, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Christopher Fuime alisema gari la Dk Mgaya liliteketea na hata kushindwa kujulikana dereva wa gari hilo.

Saturday 2 April 2016

Adhabu ya Diego Costa yaongezwa

Diego CostaDiego Costa alimkaripia Gareth Barry wa Everton tarehe 12 Machi
Mshambuliaji wa klabu ya Chelsea Diego Costa ameongezewa marufuku ya mechi ambazo hataruhusiwa kucheza pamoja na kutozwa faini zaidi kwa sababu ya utovu wa nidhamu.
Mshambuliaji huyo ameongezewa marufuku ya mechi moja na pia akapigwa faini ya £20,000 baada ya kukiri shtaka la utovu wa nidhamu.

Zuma akubali makosa kuhusu ukarabati Nkandla

Zuma
Mahakama ya Kikatiba ilimtaka Zuma alipe gharama ya ukarabati

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amekubali uamuzi wa Mahakama ya Kikatiba uliompata na hatia kuhusiana na ukarabati uliofanywa katika makao yake ya kibinafsi eneo la Nkandla.
Akihutubia taifa hilo moja kwa moja kupitia runinga, Bw Zuma amesifu mahakama hiyo na kusema imedhihirisha kuwepo kwa uhuru wa mahakama nchini humo.
Amesema uamuzi wa mahakama hiyo ni wa kihistoria kuhusu uamuzi wa mkaguzi wa hesabu za umma aliyewasilisha kesi dhidi yake mahakamani.
"Mahakama imeamua kwamba uamuzi wa mkaguzi wa hesabu za umma ni wa mwisho na anayetaka kubadili hilo lazima apitie kwa mahakama," amesema Bw Zuma.
Kiongozi huyo amesema atakubali kulipia ukarabati uliofanyiwa makao hayo ya Nkandla kama ilivyoamua mahakama.