Friday 28 November 2014

Wauza mihadarati Mexiko wawekwa kitimoto

Raisi wa Mexico Enrique Pena Nieto
Rais wa Mexico Enrique Pena Nieto ametangaza mpango wa utaokasambaratisha mahusiano kati ya mamlaka ya serikali za manispaa ya nchi hiyo na magenge ya wauza mihadarati. Bwana Pena Nieto ambaye pia serikali yake inashutumiwa kufuatia kupotea kwa wanafunzi arobaini 43 katika jimbo la Guerrero amesema Mexico haiwezi kuendelea kama ilivyo sasa.
"Jumatatau ijayo nitatuma mpango wa kubadili katiba katika bunge la Congress kupitisha sheria inayopinga wanajihisisha na uhalifu wa kupanga katika mamlaka ya manispaa. Sheria hii mpya itaanzisha mikakati kwa shirikisho kuanza kazi ya kusimamia shughuli za manispaa au kuziondolea mamlaka kama kuna dalili zinazoonyesha mamlaka hizo zimejihusisha na uhalifu wa kupanga. " Amesema Rais Pena Nieto

watu 25 wauliwa katika shambulio la bomu Nigeria

Watu wapatao ishirini na watano wamekufa kufuatia shambulio la bomu katika jimbo la Adamawa Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.
Imetaarifiwa kwamba wote waliouawa katika shambulio hilo ni raia na watano askari.tukio hilo limetokea karibu na mji wa Mubi ambao mwezi huu ulikuwa ukishikiliwa na vikosi vya serikali ya nchi hiyo baada ya kuukomboa kutoka katika himaya ya wanamgambo wa kikundi cha kiislam cha Boko Haram.
Kuna matukio kadhaa ya mashambulizi yanayofanywa na kundi la Boko Haram katika siku za hivi karibuni ikiwemo na matukio mawili ya kujitoa muhanga kaskazini Mashariki mwa mji wa Maiduguri,shambulio ambalo liligharimu uhai wa watu nane.

Thursday 27 November 2014

Arsenal yainyamazisha Dortmund kwenye champions league

Champions League Arsenal London vs Dortmund 26.11.2014
Magoli mawili ya kiustadi kutoka kwa Alexis Sanchez na Yaya Sanogo yaliipa Arsenal ushindi wa mabao mawili kwa sifuri dhidi ya Dortmund. Wakati Leverkusen ikifungwa goli moja kwa sifuri na Monaco
Mjini London, wenyeji Arsenal waliutawala mchezo na kuwanyamazisha kabisa Dortmund kuanzia mwanzo: wakati Yaya Sanogo akifunga baada ya sekunde 72 tu. Lilikuwa goli la kasi zaidi kuwahi kufungwa dhidi ya Dortmund katika mchuano wa Champions League, hata kama kulikuwa na uwezekano mdogo wa mchezaji huyo kuwa katika nafasi ya kuotea.
BVB iliiruhusu Arsenal kushambulia kwa kasi ambapo Alexis Sanchez alikuwa na uhuru wa kutamba na kuuchezea mpira anavyotaka kwa ushirikiano na washambuliaji wengine wa Arsenal kama vile Alex Oxlade Chamberlain. Katika kipindi cha pili, Sanchez alifunga bao safi sana kwa kuipinda shuti yake hadi langoni kutoka nje ya eneo la hatari.
Kocha wa Dortmund Jurgen Klopp amesema baada ya mchezo kuwa “walistahili kushindwa, hata ingawa walikuwa na nafasi kadhaa za kufunga goli”. Amesema sasa lazima wawashinde Anderlecht na kisha kumaliza katika nafasi ya kwanza kwenye Kundi lao.
Champions League Leverkusen vs Monaco 26.11.2014Monaco waliunyamazisha uwanaja wa BayArena licha ya Leverkusen kuumiliki mpira mara nyingi
Leverkusen yabumburushwa
Mjini Leverkusen, timu yake kocha Roger Schmidt kwa mara nyingine – kama tu katika mechi ya mkondo wa kwanza dhidi ya Monaco – iliutawala mchuano dhidi ya mpinzani wake lakini ikaambulia patupu.
Monaco walianza mchezo kwa kujikinga, kama tu ilivyotarajiwa, na kuwaruhusu Leverkusen kufanya shambulizi baada ya jingine. Ila hakuna mafanikio yaliyopatikana. Katika kipindi cha pili, mambo yalikuwa hay ohayo, hadi pale mchezaji wa zamani wa Leverkusen ambaye sasa anachezea Monaco, Dimitar Barbetov alipokimbia kwa kasi na kumwandalia pasi Nabil Dorar, ambaye naye akaandaa krosi safi katika eneo hatari ambayo ilimpaka mshambuliaji wa Argentina Lucas Ocampos aliyetikisa wavu bila kupoteza wakati.
Kwingineko Ulaya
Katika mechi nyingine zilizochezwa jana, mabingwa mabingwa watetezi Real Madrid walipata ushindi wa bao moja kwa bila dhidi ya Basel, wakati makamu bingwa Atletico Madrid wakiwabumburusha Olympiakos kwa kuwazaba mabao manne kwa sifuri. Nchini Bulgaria, Liverpool walitoka sare ya mabao mawili kwa mawili na Ludogorets. Juventus, iliipiku Malmo mabao mawili kwa bila, wakati Anderlecht ikipata ushindi kama huo dhidi ya Galatasaray. Awali, Zenit St Petersburg iliishinda Benfica goli moja kwa bila.

Waziri Mkuu atakiwa Kujiuzulu kutokana na sakata la ESCROW

Ripoti ya Kamati ya bunge ya Hesabu za Serikali imewataja baadhi ya vigogo wanaohusika na kashfa ya IPTL Nchini Tanzania akiwemo Waziri Mkuu na kuwataka kuwajibika kisiasa na kisheria.
Sakata hiyo ya IPTL inahusihswa na upotevu wa mamilioni ya fedha na kwa muda mrefu umezusha mjadala mzito katika bunge la Tanzania.
Katika ripoti hiyo iliyowasilishwa na mwenyekiti wa kamati hiyo Zitto Kabwe na makamu mwenyekiti Deo Filikunjombe, imethibitisha kuwepo mazingira ya udanganyifu na ufisadi katika mchakato wa malipo yaliyofanyika na kueleza kuwa upotevu huo wa fedha ungeweza kudhibitiwa kama kungekuwa na uwajibikaji wa kutosha kwa baadhi ya viongozi.
Mizengo Pinda waziri mkuu wa Tanzania ametajwa kwenye ripoti hiyo iliyowasilishwa bungeni
Kamati hiyo imewataja viongozi wengine wanaotakiwa kuwajibika kutokana na kashfa hiyo kuwa ni mwanasheria,Waziri wa nishati na Madini, Naibu Waziri wa Nishati pamoja na viongozi wengine wa bodi.
Ripoti hiyo ilitokana na ukaguzi uliofanywa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ambayo ilianika ukiukwaji mkubwa wa taratibu wakati wa uchotaji wa fedha hizo pia mahojiano na mkurugenzi mkuu wa Takukuru na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Waziri Pinda amelimbikizwa lawama ikidaiwa kuwa alijua kuwapo kwa ufisadi huo na matamshi yake kuwa fedha hizo hazikuwa mali ya umma, wakati Mwanasheria Mkuu Jaji Frederick Werema ameonekana kutoishauri vizuri Serikali na pia kuagiza fedha hizo zitolewe kwenye akaunti hiyo.
Waziri Sospeter Muhongo amelaumiwa kwa kukosa kuchukua hatua wakati akijua kuwapo kwa sakata hilo, huku naibu wake, Stephen Masele akitiwa hatiani kwa kulidanganya Bunge.
Kashfa nyingine zilizowahi chukua uzito mkubwa katika bunge la Tanzania na kusababisha viongozi kuwajibika wakiwemo Waziri Mkuu ni pamoja na kashafa ya Richmond,EPA na sasa hii ya ESCROW ambayo kwa mara nyingine kamati hiyo imeonyesha wazi mapendekezo yake ya kutaka kuwajibika kwa waziri mkuu, Mawaziri na viongozi wengine.

Sakata la Siti Mtevu lafika mbali

Hatima ya kashfa ya kudanganya umri inayomkabili aliyekuwa mrembo wa Tanzania mwaka 2014, Sitti Mtemvu bado ipo kizani baada ya polisi kuikana kauli ya Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (Rita)
Rita, kwa upande wao ilieleza wiki moja iliyopita kuwa imekabidhi polisi vielelezo kuhusu uchunguzi wa kashfa hiyo kwa lengo la kuchukua hatua.
Jana, Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alikana kupokea taarifa za vielelezo hivyo vilivyotumiwa kuombea cheti cha kuzaliwa cha Sitti Mtemvu.

Wiki mbili zilizopita, Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo kupitia Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) ilijivua lawama katika kashfa hiyo na kuiachia Rita.
Akizungumza  jana, Kova alisema, “Jeshi la Polisi halijapokea vielelezo vyovyote kutoka Rita, wamepeleka wapi? Iwapo waliviwasilisha katika kituo chochote cha polisi watoe taarifa iliyo sahihi, iwapo vielelezo hivyo vitatufikia tutachukua hatua stahiki,” alisema Kova.

Kwa upande wao, Rita waliahidi kuwasilisha vielelezo hivyo wiki hii na kwamba vilicheleweshwa kutokana na kukamilisha upekuzi wa taarifa za kuombea cheti pamoja na cheti cha awali kilichokuwa kikitumiwa na Sitti Mtemvu.

Mkurugenzi wa Idara ya Sheria wa Rita, Emmy Harrison alisema jana kuwa idara yake imekamilisha taratibu zote zinazotakiwa na vielelezo hivyo vitakabidhiwa rasmi polisi.
“Haya ni masuala ya kisheria, hivyo sisi tumeshakamilisha kile tulichotakiwa kukifanya na mchakato huu bado unaendelea, tupo katika maandalizi ya mwisho kwa ajili ya kuripoti polisi, wiki hii vielelezo vya Sitti vitapelekwa kwenye vyombo vya usalama kwa ajili ya hatua zaidi,” alisema Harrison.

Aliyekuwa kocha wa Chelsea kuinoa Ghana

Mkufunzi wa zamani wa Chelsea Avram Grant ameteuliwa kuwa kocha mpya wa Ghana.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 59 alitia saini kandarasi ya kufunza kwa miezi 27 na kuchukua uongozi kutoka kwa Maxwell Konadu, ambaye amekuwa kocha wa muda tangu Kwesi Appiah alipoondoka mwezi wa Septemba.
Ataanza kazi Jumatatu na mkataba wake kumalizika mwishoni mwa Februari 2017 - baada ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika.
Avram Grant alipokuwa mkufunzi wa timu ya Chelsea.
Raia huyo wa Israeli ana wiki sita tu kuiandaa Black Stars kwa ajili ya kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2015 nchini Equatorial Guinea.
Shirikisho la kandanda nchini Ghana limetoa ruzuku kwake kwa "kufanya vizuri" katika mashindano hayo na amepewa muda mfupi na timu hiyo na kuwa atashinda kombe hilo miaka miwili ijayo.
Ghana, ambayo iliongoza katika kufuzu kwenye kundi lao ili kushiriki mashindana hayo mwaka ujao, itapata kujua wapinzani wao nchini Equatorial Guinea wakati droo itakapofanywa tarehe 3 Desemba.
Mashindano yatafanyika kati ya Januari 17 na 8 Februari.
Grant, ambaye alikuwa kocha mkuu wa timu ya Chelsea alishindwa na Manchester United katika fainali za mwaka wa 2008 katika Ligi ya Mabingwa, alipohudumu hadi hivi majuzi ambapo alichaguliwa kuwa mkurugenzi wa kiufundi katika klabu ya BEC Tero Sasana nchini Tahailand.
Jukumu lake la mwisho kama kocha lilikuwa katika klabu ya Partizan Belgrade kati ya mwaka 2012-2014, wakati ambapo aliongoza klabu hio kutwaa ubingwa wa ligi kwa mara ya tano.
Timu ya soka ya Ghana
Kando ya kuviongoza vilabu vya Uingereza vya Portsmouth na West Ham, Grant ana uzoefu wa kimataifa kwani aliifunza timu ya taifa ya Israeli kwa miaka minne.
Kumekuwa na wale wamekuwa na wasiwasi kwamba utaifa wa Grant ungeweza kumzuia kuingia baadhi ya nchi za Afrika Kaskazini.
Rais wa shirikisho la kandanda nchini Ghana, Kwesi Nyantekyie aliiambia BBC Michezo "kwamba ni suala" lakini anasema kuwa pande hizo mbili zitakabiliana nalo.
"Mmiliki wa pasipoti ya nchi ya Israel hatakataliwa tu kuingia nchi za Afrika Kaskazini,bali pia atazuiliwa kuingia baadhi ya nchi za Kiarabu," alisema.
"Yeye ameleta njia mbadala ya kukabiliana nayo. Kuna utaratibu wa kuridhisha wa kukabiliana na tishio lake.
Hivi karibuni, katika miezi michache ijayo, tutashughulikia kikamilifu mambo hayo."

Wednesday 26 November 2014

wezi wavunja nyumba ya Victor wanyama na kumwibia huko Uingereza

Maafisa wa polisi wanachunguza kisa kimoja ambapo wezi walivunja na kuingia katika nyumba ya mchezaji wa kilabu ya Southampton Victor Mugubi Wanyama nchini Uingereza na kumuibia mali yake usiku wa jumatatu.
Shati moja la kiungo wa kati wa timu ya Barcelona Andres Iniesta ,pamoja na nguo za wanamitindo kadhaa pamoja na jozi 20 za viatu ni miongoni ya vitu vilivyoibwa.
Wezi hao pia waliiba gari la mchezaji huyo aina ya Land Rover lenye thamani ya shilingi millioni 8.4 fedha za kenya,fanicha,Runinga pamoja na vifaa vyengine vya kielektroniki .
Mkenya huyo mwenye umri wa miaka 23 anaishi katika nyumba ndogo na polisi wameshangazwa kwamba majirani zake hawakuamshwa na kelele za uvunjaji huo.
Kikosi cha timu yake ya Southamptom kilikuwa kimesafiri hadi Villa ambapo bao la dakika za mwisho liliifanya mechi hiyo kuwa na sare ya 1-1.
Wanyama ameshiriki katika mechi 14 msimu huu na kufunga mabao matatu huku Southampton ikiendelea kupigania nafasi ya kufuzu katika mechi za UEFA.
Ni mchezaji aliyeuzwa kwa kitata cha juu kutoka Uskochi baada ya Celtic kumuuza kwa pauni 12.5 mnamo mwaka 2013.

Makamu wa rais wa Zimbabwe afukuzwa ZANU-PF

Vyombo vya habari vya Serikali nchini Zimbabwe vinaripoti kuwa Makamu wa Rais,Joyce Mujuru, ameondolewa kwenye halmashauri kuu ya chama cha ZANU-PF.
Mujuru anashutumiwa kupanga mauaji dhidi ya Rais wa nchi hiyo,Robert Mugabe.
hatua hiyo imekuja baada ya Kampeni dhidi ya Mujuru iliyofanywa na Mke wa Rais Mugabe, Grace ambaye kwa kiasi kikubwa anaamini anataka kumrithi Mumewe atakapotoka madarakani.
Viongozi kadhaa wa ZANU-PF wameshindwa kutetea nafazi zao katika Chama hicho.

Kenya yaitaka dunia kuingilia machafuko ya kisiasa nchini Somalia

Kenya imetoa wito kwa Jumuiya ya Kimataifa kuingilia kati mgogoro wa kisiasa ndani ya uongozi wa Somalia, ambao umeathiri amani ya kanda hiyo.
Kauli hiyo imetolewa na naibu rais wa Kenya William Ruto alipokuwa na mazungumzo na naibu waziri mkuu ambaye pia waziri wa mambo ya nje wa Jamhuri ya Slovakia Miroslav Lajcak. Amesema tofauti zilizopo kati ya rais Hassan Sheik Mohamud wa Somalia na waziri mkuu Abdiweli Ahmedi zinarudisha nyuma juhudi za nchi za kanda hiyo kuleta utulivu nchini humo. Naibu Ruto amesema wana wasiwasi na mpasuko kati ya viongozi hao wawili, na kwamba hali bado ni tete ndani ya nchi hiyo.
Waziri mkuu wa Somalia Ahmed, Oktoba 25 aliripotiwa kutangaza uamuzi wa kuvunja baraza la mawaziri bila kushauriana na rais. Hata hivyo rais Mahmud baadaye alipinga mabadiliko hayo na kumfukuza kazi Ahmad kwa "kutoa uamuzi wa kufedhehesha" na kutangaza kitendo cha kuvunja baraza la mawaziri ni batili, pia aliwataka mawaziri walioondolewa kuendelea na kazi zao kama kawaida.

Uwanja wa ndege mjini Tripoli washambuliwa

Ndege za kivita za jeshi la Libya jana zilishambulia uwanja wa ndege wa Mitiga huko Tripoli na kusababisha safari zote za ndani na nje ya nchi kusitishwa.
Kamanda wa jeshi la anga Brigedia Saqr Jeroshi amesema shambulizi hilo lililenga kukikatia usambazaji wa vifaa kikundi cha kigaidi cha Libya Dawn, na kuongeza kuwa anga za magharibi na mashariki za Libya sasa zinalindwa na ndege za jeshi la taifa.
Aidha amesema mbali na uwanja wa ndege wa Mitiga, bandari za Sirte, Misrata na Zuwarah zinaweza kuwa sehemu nyingine zitakazolengwa kushambulia wapiganaji wa kiislamu. Mitiga ni uwanja wa ndege pekee unaofanya kazi, baada ya kundi la Libya Dawn kuharibu uwanja wa ndege wa kimataifa wa Tripoli na kuudhibiti mwezi Agosti. Muungano wa wanamgambo wa kiisalamu umeweka utawala wake ili kupambana na ule unaotambulika kimataifa, ambao sasa upo uhamishoni mji wa mashariki wa Tobruk.

Chelsea, barca zaua man city yaponea dakika za Mwisho

Usiku wa kuamkia leo kindumbwe ndumbwe cha michuano ya Klabu Bigwa barani Ulaya kiliendelea na kushuhudia Chelsea ikitoa kipigo cha mbwa mwizi mbele ya mashabiki wa Schalke 04 ya Ujuremani pale ilipoishindilia magoli 5 bila majibu.
Manchester City ya England nao wakawabamiza wababe wengine wa Ujerumani Bayern Munich kwa kwa kuwafunga magoli 3 - 2 na kufufua matumaini ya kusonga mbele katika michuano hiyo huku magoli yote matatu ya Man City yakitiwa kimiani Sergio Aguero.
Katika mechi nyingine Paris St. Germain ya Ufaransa waliwashikisha adabu Ajax ya Uholanzi kwa kuifunga magoli 3 - 1 huku Becelona kwa upande mwingine wakiisasambua Apoel Nicosia ya Syprus kwa kuishushia kichapo cha magoli 4 kwa yai.
CSKA Moscow ya Urusi na AC Roma zikatoka suluhu ya goli moja 1 - 1
Lionel Messi celebrates scoring against Apoel NicosiaBurudani hiyo itaendelea leo ambapo Liverpool ya England baada ya kufanya vibaya katika mechi zilizotangulia leo wanajaribu bahati yao wakiwa ugenini dhidi Ludogorets ya Bulgaria.
Arsenal nao watawakaribisha Borusia Dortmud ya Ujerumani huku vita vingine vikiwa ni kati ya FC Basel ya Uswis watakaopopepetana na Real Madrid. Malmo FF ya Sweden watakuwa wenyeji wa Juventus ya Italia

Messi ndiye mchezaji bora wa kandanda

Lionel Messi celebrates scoring against Apoel NicosiaNyota wa Barcelona Lionel Messi amesifiwa kuwa "mchezaji bora zaidi katika historia ya kandanda", anasema rais Josep Maria Bartomeu.
Raia huyo wa Argentina,mwenye umri wa miaka 27,ndiye mfungaji bora wa muda katika ligi ya Hispania La Liga na mabao 253 kufuatia yeye kufunga mabao matatu Jumamosi waliposhinda 5-1 dhidi ya Sevilla.
Bartomeu alisema: "Tutakuwa naye Leo hapa kwa miaka mingi ijayo, tuna furaha na kile amepata.
"Tulijua rekodi ingelikuja. Imenifurahisha sana kumwona akiisawazisha, kwa ajili yake na kwa ajili ya klabu."
Messi aliyetuzwa mchezaji bora zaidi duniani kwa miaka minne amefunga mabao 368 kwa jumla akiichezea Barcelona, klabu yake ya pekee kama mwandamizi, na mabao 45 akichezea Argentina.
Messi - ambaye pia anashikilia rekodi ya mfungaji bora katika historia ya Ligi ya Mabingwa na mabao 71 - hivi karibuni alisema kuwa mustakabali wake ni "mgumu", lakini baba yake akakataa.
Bartomeu alisema: "Hakuna maneno ya kuelezea kile anachokifanya.Anafurahi kuchezea Barcelona ambapo amekuwa kwa miaka mingi, na anapatana vizuri na wachezaji wenzake.
"Ana wasiwasi kuhusu masuala yasiyo ya michezo lakini klabu inamsaidia. Watu wanapaswa kuzungumza naye kuhusu kandanda badala ya mambo mengine."
Baada ya mchezo,kocha mkuu wa Barcelona Luis Enrique alisema anadhani Messi atapanua rekodi, ambayo hapo awali alisimama tangu mwaka wa 1955, kiasi ya kwamba itakuwa ngumu kufikiwa na mtu mwingine.

Misri; Watu 10 wamepoteza Miasha baada yjengo la ghorofa kuanguka

Watu kumi wamepoteza maisha baada ya jengo la ghorofa kuanguka mjini Cairo nchini Misri, maafisa wameeleza.
Watu saba wamejeruhiwa baada ya jengo la ghorofa nane kuanguka usiku.
Mkuu wa Idara ya dharula Jenerali Mamdouh Abdul Qader amesema vikosi vya uaokoaji vinawasaka Watu 15 wanaokisiwa kunasa kwenye kifusi.
Mara kadhaa majengo yameanguka nchini humo, sababu kubwa ikiwa ujenzi usiofuata kanuni na Sheria pia usimamizi mbovu wa taratibu za ujenzi.
Jenerali Qader ameliambia shirika la Habari la Ufaransa kuwa hawajui chanzo cha ajali hiyo,lakini walipatiwa taarifa kuwa ghorofa mbili za juu zilijengwa kinyume cha sheria.
Wakazi wa majengo ya karibu na lilipoanguka jengo hilo wameondoka katika makazi yao kwa nia ya kujihadhari.
Mwezi Januari Mwaka jana,Watu 28 walipoteza maisha baada ya jengo la ghorofa nane kuanguka mjini Alexandria.

Boko haramu waua 78 tena Nigeria

Watu 78 wameuawa katika mashambulio mawili ya kujitoa mhanga yaliyofanywa sokoni, katika mji wa Maiduguri kaskazini mwa Nigeria.
Watu walioshuhudia tukio hilo wamesema mlipuko wa kwanza ulitokea wakati washambuliaji hao walipomuwekea mlipuko mwanamke mmoja mwenye matatizo ya akili.
Wakati umati wa watu wakienda kutoa msaada, mwanamke mwingine alijitoa mhanga.
Kundi la kiislamu la wapiganaji la Boko Haram ambalo linadhibiti maeneo mengine ya miji ya kaskazini mwa nchi hiyo na vijiji, linadhaniwa kuhusika na shambulio hilo.
Wanaigeria wamekosa Imani na jaribio la serikali ya nchi yao kufanya mazungumzo na Boko Haram, kutokana an kuongezeka kwa ghasia hizo.

Tuesday 25 November 2014

House Girl aliyempiga mtoto wa boss wake aUganda atiwa kizuizini

Kuanzia mwishoni mwa wiki iliyopita kulikua na stori imesambaa sana kwenye mitandao ya kijamii kama instagram, facebook na twitter kuhusu msichana wa kazi ambae alitegeshewa na Baba mwenye nyumba kamera nyumbani na baadae video iliyorekodiwa ikamuonyesha akimpiga mtoto wa mwenye nyumba.
ugando housegirlBaadae zilitoka stori mbalimbali kwamba Mtoto mwenyewe ambae ana umri wa miaka miwili amefariki, ni stori ambazo ziliambatana na taarifa nyingine zisizo na ukweli 
Msichana huyu wa kazi anaitwa Tumuhairwe ana umri wa miaka 22 na sio 25 kama ilivyoripotiwa ambapo ana siku 26 tu toka aanze kufanya kazi kwenye familia ya mtoto huyo. - Kwa sasa yuko rumande kwenye gereza la Luzira Uganda na atafunguliwa mada ya kutaka kuua.
Unaambiwa haya yote yasingejulikana kama Polisi isingemkamata baba mzazi wa mtoto huyu, yani baba alipoona ile video ndio akampiga Msichana huyu wa kazi ambae baada ya kipigo alikwenda kumshitaki baba wa mtoto Polisi.
Polisi walipomchukua Erick Kamanzi (Baba wa mtoto) nyumbani kwa ke na kumfikisha Polisi ambako alieleza sababu za kumpiga Msichana huyu na kuwaonyesha Polisi hii video hapa chini ambayo ni ya tukio la mtoto wake kupigwa. uganda 3- Baada ya hapo Polisi ndio wakamwachia na kumkamata Msichana huyu wa kazi.
Erick ambae ndio baba mzazi wa mtoto huyu amesema wanashukuru Mungu mtoto kuwa hai bila matatizo na sasa mtoto amekua karibu na baba yake zaidi.Tarehe 8 December ndio atapandishwa Mahakamani kusomewa mashitaka yake.November 24 2014 Waziri wa mambo ya vijana wa Uganda aliitembelea familia ya mtoto huyu baada ya watu kuanza kusambaza habari kwamba mtoto huyu alifariki, taarifa ambazo sio za kweli.

Mchezaji wa Kriket wa Australia ,Hugher yuko mahuturi baada ya kupigwa gongo la Kichwa

MCHEZA Kriketi wa Australia, Phil Hughes anapigania maisha yake hospitalini mjini Sydney baada ya kugongwa kichwani na gongo la kuchezea mchezo huo wakati wa mechi ya Sheffield Shield leo.
Nyota huyo ambaye amecheza mechi 26 Australia ikiwemo michuano mitatu ya Ashes, amefanyiwa upasuaji na yupo kwenye kitengo cha wagonjwa walio katika uangalizi maalum.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25, aliyeichezea Australia Kusini dhidi ya Wales Kusini mpya katika michuano ya Sydney Cricket Ground (SCG), alipigwa na gongo hilo akiwa helmet kichwani na Sean Abbott kabla ya kupoteza fahamu na kukimbizwa hospitali.
Hughes underwent surgery at St Vincent's Hospital in Sydney and remains in a critical condition
Phil Hughes amefanyiwa katika upasuaji katika hospitali ya St Vincent mjini Sydney na bado ana hali mbaya
Batsman Phil Hughes collapsed and hit the ground face first at the Sydney Cricket Ground this afternoon after being struck in the head by a bouncer during a Sheffield Shield match
Phil Hughes alipoteza fahamu uwanjani baada ya kugongwa na gongo hilo la Kriketi

Mwakezaji ajeruhi watu 6 kwa risasi zanzibar

Zanzibar. Jeshi la Polisi Zanzibar linamshikilia mwekezaji kutoka Ufaransa, Ivan Kodeh kwa tuhuma za kuwajeruhi watu sita wakiwamo waandishi wa habari kwa risasi baada ya uongozi wa Hoteli ya Cristal kudaiwa kugoma kukabidhi madaraka kwa uongozi mpya huko Paje, Mkoa wa Kusini Unguja.
Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai Zanzibar (DDCI), Salum Msangi aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi saa tano asubuhi katika hoteli hiyo.
Aliwataja waliojeruhiwa kuwa ni waandishi wa habari, Munir Zakaria wa Channel Ten na Kuruthum Ali wa TBC ambao walikuwa kazini. Wengine ni Ramadhani Mohammed (25), Wadi Ame Khamis (35), Ashraf Suleiman (36) na Nadir Ali Juma (28).
Alisema mwekezaji huyo anashikiliwa pia kwa kumiliki silaha inayodaiwa kutumika katika shambulio hilo aina ya Gamo yenye namba 04-4L-720/70-07 ambayo imetengenezwa Hispania.
Alisema kwa mujibu wa Kifungu cha 6 (3) cha Sheria ya Silaha namba 2 ya mwaka 1991 na Kifungu namba 19 cha Sheria ya Silaha Tanzania Sura ya 223, mtu yeyote akiwa Tanzania na Zanzibar haruhusiwi kutumia au kumiliki silaha pamoja na risasi. Alisema taratibu za kumfikisha mahakamani zimeanza.
Katika tukio jingine, Msangi alisema polisi pia inamshikilia raia wa Poland, Artur Miarka (52) kwa tuhuma za kukutwa na bunduki aina ya BSA air Rifle na risasi zake pamoja na darubini ya kumsadia kuona mbali.
Alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa katika eneo la Pwani Mchangani, Mkoa wa Kaskazini Unguja na baada ya kuhojiwa alisema amekuwa akitumia silaha hiyo kwa muda wa miaka mitatu Visiwani hapa.
Alisema kutokana na matukio hayo, polisi imetoa wiki moja kwa wawekezaji wote wanaomiliki silaha Zanzibar kuzisalimisha katika vituo vya polisi kabla ya kuanza kwa msako katika hoteli zote Unguja na Pemba.

Waziri wa Ulinzi wa marekani ajiuzulu

Waziri wa Ulinzi Chuck Hagel akipeana mkono na Rais Barack Obama baada ya kutangaza kujiuzulu kwake
Waziri wa Ulinzi Chuck Hagel akipeana mkono na Rais Barack Obama baada ya kutangaza kujiuzulu kwake
Waziri wa ulinzi wa Marekani, Chuck Hagel amejiuzulu baada ya takriban miaka miwili kuwepo katika wadhifa  huo.
Rais Barack Obama aliongea huko White House akiwa pamoja na Hagel na Makamu Rais, Joe Biden pembeni yake alisema Waziri wa Ulinzi alimueleza mwezi uliopita kwamba wakati umefika kwa yeye kukamilisha huduma zake katika serikali.
Chuck Hagel, Novemba 14, 2014.Bwana Obama alimuita Hagel ni “mtu madhubuti’ katika kuusaidia utawala kujibu changamoto za ugonjwa wa Ebola na kundi la Islamic State.
Chuck Hagel, Novemba
Rais alimuelezea Hagel kuwa ‘si waziri wa ulinzi wa kawaida’ na kusema alijitolea kwa usalama wa taifa la Marekani na kwa wanajeshi kwa miongo kadhaa.
Hagel ni mrepublican pekee katika baraza la mawaziri la bwana Obama. Alisema kutumika kama Waziri wa Ulinzi  ilikuwa ni ‘fursa kubwa sana katika maisha yake’. Hagel alisema atabakia katika wadhifa huo mpaka mrithi wake atakapothibitishwa.

Baadhi ya wasichana kenya watumia miili yao kujipatia kipato

Sextourismus Prostitution Kenia Wasichana wadogo nchini Kenya wamekuwa wakilazimika kujiingiza katika unywaji pombe na uuzaji wa miili yao kama njia ya kujipatia chakula wao na familia zao.
Brittanie Richardson binti wa kimarekani mwenye umri wa miaka 27 ameanzisha kampeni ya kupinga hali hiyo baada ya ziara yake iliyoshuhudia vitendo hivyo vya mara kwa mara kwa familia zilizo na hali ngumu ya maisha.
Mjini Nairobi kuna msongamano mkubwa wa makazi duni, watoto wenye njaa mara nyingi wanafanya biashara ya miili yao ili kujipatia pesa kidogo au chakula, mji huo wenye wakazi milioni 3.1, ni nyumbani kwa watu milioni 2 wanaoishi katika makazi duni na idadi ya watu katika makazi duni katika mji huo mkuu wa Kenya inakua kwa asilimia 6 kwa mwaka.

Eneo la fukwe za utalii nchini Kenya
Kulingana na shirika la kuwahudumia watoto la umoja wa Mataifa Kenya ina watoto wanaofanya kazi ya ngono 30,000 waliogawanyika katika pembe zote za fukwe za utalii, huku ukahaba miongoni mwa watoto likitambuliwa kama tatizo linalohitaji kukabiliwa kwa utekelezaji wa sheria kali na kuwapa wasichana hao ncji mbadala ya kujikwamua kutokana na mtego huo.
Richardson kutoka mji wa Atlanta, katika jimbo la Georgia nchini Marekani hakuwa na wazo juu ya kiwango cha tatizo nchini Kenya mpaka pale aliponza kusafiri mara kwa mara Afrika wakati akiwa chuoni. Awali alikuwa akisaidia nchi ya Afrika Kusini kupambana na kukosekana haki ya kijamii na kisha nchini Msumbiji.
Mkutano na mwanamke wa Canada nchini Msumbiji ambaye alihitaji msaada wa kuanzisha makaazi ya kuwaokoa watoto walionasa katika ukahaba, ulimfanya Richardson kuelekea katika mji wa Mtwapa nchini Kenya, ambao umekuwa na sifa mbaya ya ukahaba katika eneo la pwani.
Richardson alisema, na hapa ninamunukuu, "Ulikuwa ni wakati wa kuhuzunisha na kushitusha kuona binti wa miaka 15 kiasi kidogo mwenye miaka minane akiinieleza kuwa analazimika kufanya ngono ili aweze kupata chakula kiukweli nilishituka.
Richardson alijiona yeye mwenyewe nakuwa mmoja wa watu wanaongoza harakati za kuendesha kampeni ya ngazi za chini kupambana na umasikini kuacha kuwapeleka watoto wanaotoka katika makazi duni katika biashara ya ngono.
Uwanja wa ndege wa Kimataifa Kenya
Lakini baada ya miaka miwili ya harakati za kituo cha Mtwapa, Richardson anataka kufanya kazi zaidi ya kusaidia na mwezi wa nne mwaka huu aliweka kitengo cha sanaa na kukomesha unyanyasaji chenye lengo la kusaidia watumwa wa ngono kupitia kufanya sanaa ambayo anaona itakuwa tiba na dawa.
Kwa kusaidiwa na mfanyakazi wa kijamii, Richardson aliwachagua wasichana 10 wenye umri kati ya miaka minane na 16 waliokuwa wakiishi katika makazi duni ya Sinai kuwa sehemu ya mpango wake. Sinai ni moja ya makazi 200 duni mjini humo.
Richardson alisema Kati ya wasichana hao 10 kati yao ama wamebakwa au wamelazimishwa na umasikini au wazazi wao kufanya ngono ili kujipatia fedha Aliongeza kuwa majukumu yake katika kazi hiyo inatokana na uzoefu wake kutokana na kufanyiwa unyanyasaji wa kingono wakati wa utoto wake na ndugu wa karibu katika familia yake lakini kila mtu amejaribu kupuuza jambo hilo.
Anaipongeza asasi ya vijana ya michezo ya kuigiza ya Freddie Hendricks ya mjini Atlanta, iliyoanzishwa na mwanamuziki wa muziki wa miondoko ya jazz kwa kuyaokoa maisha yake. Alisema aliona upendo wa kweli waliomuonyesha kama mwathirika na anataka kufanya vivyo hivyo kwa wasichana wengi.
Lakini kazi yake itafanikiwa kwa gharama na Richardson ameweza kufanikisha uungwaji mkono kutoka idadi kubwa ya wasanii, wanaharakati mjini New York ambao wamekuwa wakiendesha jitihada za kuchangisha kwa ajili ya onyesho lenye kupinga na kukemea vitendo vya unyanyasaji wa ngono dhidi ya wasichana.