Tuesday 25 November 2014

Rufaa ya Ndumbaro sasa laanza kuwachanganya TFF

Makamu mwenyekiti wa Kamati ya Rufaa ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Hammidu Mbwezeleni amesema TFF isipotoshe umma kwa vile bado haijawasilisha rufaa ya Damas Ndumbaro kwenye kamati yao.
Kauli ya Mbwezeleni imekuja baada ya katibu mkuu wa TFF, Celestine Mwesigwa kusema kuwa tayari wamewasilisha suala hilo la Ndumbaro kwenye kamati husika, lakini kamati hiyo ndiyo inayochelewesha.
Akizungumza na gazeti hili kuhusu suala hilo, Mbwezeleni alisema hakuna rufaa yoyote iliyowasilishwa kwenye kamati yetu. Kwa kawaida rufaa ikikatwa, TFF wanatuandikia kutujulisha, lakini hakuna chochote ambacho wameshatuambia mpaka sasa zaidi ya kusikia kwenye vyombo vya habari.
“Ninavyoongea na wewe narudi zangu Zanzibar nilikuja Bara mara moja, na sijaambiwa lolote mpaka muda huu. Hatuwezi kukutana wakati TFF hawajaileta rufaa hiyo mezani mwetu.”

No comments: