MATOKEO ya wikiendi iliyopita ya Ligi Kuu ya Vodacom yaliwaacha
mashabiki wa soka katika mshangao. Iko hivi Ndanda FC waliichapa Azam FC
bao 1-0. Simba wakatoa sare nyingine ya bao 1-1 na Mtibwa na Yanga
ikapigwa bao 1-0 na Kagera Sugar.
Sababu kuu ya Simba ni kuingia katika rekodi ya
kipekee hapa nchini baada ya kucheza mechi ya sita mfululizo ikipata
matokeo ya sare. Jumamosi iliyopita ilitoshana nguvu na Mtibwa kwa sare
ya 1-1.
Wana Msimbazi hao wana magoli sita ya kufunga na
sita ya kufungwa,matokeo haya yamezidi kuwanyong’onyesha mashabiki wa
Simba, mwanya uliotumiwa na wale wa Yanga kuficha aibu yao ya kipigo
huko Kaitaba.
Wakati Wekundu wa Msimbazi wakijiuliza kwa
yanaoendelea, Simba imejikuta ikiingia kwenye orodha ya timu
zilizoambulia sare nyingi za mfululizo. Timu za Manchester City,
Southampton na Norwich City kwa miaka tofauti zilijikuta katika historia
ya miongoni mwa timu ambazo zilitoa sare nyingi za mfululizo katika
Ligi Kuu England.
Timu hizo tatu za England ziliambulia sare saba
katika misimu tofauti. Kumbukumbu zinaonyesha kuwa, Norwich City
ilicheza michezo kati ya 38 hadi 42 katika msimu wa 1993-1994 na
kujikuta ikipata sare saba mfululizo.
Msimu uliofuata, 1994-1995, Southampton nayo ilicheza idadi kama hiyo ya mechi na kujikuta ikiambulia sare saba mfululizo.
Kama hiyo haitoshi, Manchester City nao walijikuta katika orodha hiyo ya sare saba mfululizo katika msimu wa 2009-2010.
Manchester City pia wamo katika orodha ya timu
zinazoongoza kwa kutoa sare nyingi kwa msimu mzima wa ligi kwani katika
msimu wa 1993-1994 ilicheza mechi 42 jumla na kupata sare 18.
Simba inapaswa kushinda mechi inayofuata la Ligi
Kuu Bara ili kukwepa kuzifikia timu hizo za England kwa idadi kubwa ya
sare za mfululizo.
No comments:
Post a Comment