Tuesday, 25 November 2014

Waziri wa Ulinzi wa marekani ajiuzulu

Waziri wa Ulinzi Chuck Hagel akipeana mkono na Rais Barack Obama baada ya kutangaza kujiuzulu kwake
Waziri wa Ulinzi Chuck Hagel akipeana mkono na Rais Barack Obama baada ya kutangaza kujiuzulu kwake
Waziri wa ulinzi wa Marekani, Chuck Hagel amejiuzulu baada ya takriban miaka miwili kuwepo katika wadhifa  huo.
Rais Barack Obama aliongea huko White House akiwa pamoja na Hagel na Makamu Rais, Joe Biden pembeni yake alisema Waziri wa Ulinzi alimueleza mwezi uliopita kwamba wakati umefika kwa yeye kukamilisha huduma zake katika serikali.
Chuck Hagel, Novemba 14, 2014.Bwana Obama alimuita Hagel ni “mtu madhubuti’ katika kuusaidia utawala kujibu changamoto za ugonjwa wa Ebola na kundi la Islamic State.
Chuck Hagel, Novemba
Rais alimuelezea Hagel kuwa ‘si waziri wa ulinzi wa kawaida’ na kusema alijitolea kwa usalama wa taifa la Marekani na kwa wanajeshi kwa miongo kadhaa.
Hagel ni mrepublican pekee katika baraza la mawaziri la bwana Obama. Alisema kutumika kama Waziri wa Ulinzi  ilikuwa ni ‘fursa kubwa sana katika maisha yake’. Hagel alisema atabakia katika wadhifa huo mpaka mrithi wake atakapothibitishwa.

No comments: