Saturday 8 November 2014

Lulu; Sina mda wa kuwa na mpenzi

Lulu
MWIGIZAJI Bora wa Kike 2013, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amesema katika maisha yake hahusudu kitu mapenzi na hatumii muda na nguvu zake huko, bali anazielekeza katika kazi.
Lulu anayetamba filamu yake mpya ‘Mapenzi ya Mungu’, amesema kuliko kupoteza muda kwa mwanaume, bora atulie na kufikiria nini cha kufanya ili kuboresha kazi zake, kwani anaamini bado ana muda mwingi wa kujipanga kabla ya kufikiria mapenzi.
Nyota huyo wa filamu alisema kwa muda sasa ametafakari kuhusu uhusiano na kugundua ni kupoteza nguvu, ambazo anaamini ni heri azitunze zije kumsaidia baadaye.
“Kuliko kupoteza muda na nguvu kwa mwanaume, bora nizitunze kwa ajili ya kuwalea wanangu baadaye, bado nina muda sijaishia katika Foolish Age, Mapenzi ya Mungu, bali nina kazi nyingi ninazohitaji kuzifanya ili watu wajue kwamba Lulu ana kipaji katika kazi ya sanaa na si kwamba niliingia huku kwa bahati mbaya,” alisema Lulu.

No comments: