Basi la kampuni ya Wibonela aina ya Scania likiwa limepinduka eneo la Phantom mjini Kahama |
Katika ajali hiyo iliyotokea Kahama, mtu mmoja
ambaye jina lake halikuweza kufahamika, aliuawa kwa kupigwa na kisha
kuchomwa moto na wananchi waliombaini wakati akitaka kuiba kompyuta ya
mpakato kutoka kwa majeruhi.
Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Halmashauri ya Mji
wa Kahama, Joseph Ngowi alikiri kupokea majeruhi hao na kuongeza kuwa
hali za watu wanne kati ya majeruhi hao ni mbaya wanaandaa utaratibu wa
kuwapeleka katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando Mwanza.
Ngowi aliwataja waliokufa kuwa ni kichanga
Robinick Jordan, aliyekuwa na miezi mitatu na ambaye wazazi wake wote
wawili wamejeruhiwa na kulazwa katika hospitalini hapo.
Ngowi aliwataja wengine waliofariki na miili yao
kuhifadhiwa hospitalini kuwa ni Amina mkazi wa Kigoma na Salum ambaye
makazi yake hayakuweza kujulikana pamoja na mtu mmoja ambaye pia jina
lake halikuweza kupatikana. Alisema waliweza kupata jina mojamoja la
majeruhi hao wawili.
Pia Ngowi alisema majina ya majeruhi 40 yanapatikana katika Hospitali hiyo ya Kahama.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Jastusi
Kamugisha aliyefika eneo la tukio hilo, alisema chanzo cha ajali hiyo ni
mwendo kasi.
Alisema dereva wa basi hilo alikuwa katika mwendo wa kasi na baadaye gari kumshinda na kusababisha ajali hiyo.
No comments:
Post a Comment