Sunday 9 November 2014

Wanachama wa Alshabaab zaidi ya 70 wauawa

Wapiganaji wa Alshabba.Serikali ya Somali inasema kuwa imewaua wapiganaji 70 katika kisiwa cha kudha
Mamlaka kusini mwa Somali inasema kuwa zaidi ya wapiganaji 70 wa kundi la Alshabaab waliuawa katika mapigano siku ya jumamosi katika vita vya kukidhibiti kisiwa muhimu cha kudha.
Alshabaab limechukua udhibiti wa kisiwa hicho ,na linasema kuwa limewaua zaidi ya wanachama 60 wa jeshi moja la afrika mashariki,linasaidia serikali ya Somali.
Mamlaka katika jimbo la Juba nchini Somali imewashtumu wanachama wa Al shabaab kwa kuwaua raia.
Vikosi vya wanajeshi wa Afrika pamoja na wale wa Somali katika miezi ya hivi karibuni vimehusika katika kuwafurusha wanamgambo hao kutoka miji kadhaa na vijiji kusini mwa Somali.

No comments: