Mechi hizo zinachezwa siku moja tu baada ya shirikisho la soka barani afrika CAF kuitaja Equitorial Guinea kama taifa litakalo andaa dimba hilo badala ya Morocco ambayo ilijiondoa kwa hofu ya maambukizi ya ugonjwa hatari wa Ebola.
Morocco pia imepigwa marufuku kushiriki katika dimba hilo na sasa Equitorial Guinea itashiriki licha ya kuondolewa katika mechi hizo kwa kuchezesha mchezaji asiyetakikana.
Mbali na Waandalizi wa kombe hilo,Algeria,Cape Verde na Tunisia tayari wamefuzu kushiriki katika kinyang'anyiro hicho.
No comments:
Post a Comment