Saturday 1 November 2014

Yanga yaonja joto la jiwe simba Droo kama Kawaida

YANGA-MPYA-2014
Ligi kuu ya soka Tanzania Bara imeendelea hii leo huku ikishuhudia matokeo ya kushangaza kwa baadhi ya timu .
Katika michezo iliyopigwa hii leo Dar-es-salaam Young Africans walipoteza mchezo wao dhidi ya Kagera Sugar kwa bao moja kwa sifuri, bao lilolofungwa na mshambuliaji Paul Ngwai aliyeingia kwenye kipindi cha pili .
Katika mchezo huo Yanga walimaliza wakiwa tisa uwanjani baada ya nahodha na beki wa kati wa timu hiyo Nadir Haroub Canavarro kuonyeshwa kadi nyekundu baada ya kuonekana kumpiga kiwiko mchezaji wa kagera Sugar.
Huko Mjini Morogoro Wekundu wa Msimbazi Simba Sports Club walitoka sare yao ya sita mfululizo baada ya kufungana bao moja kwa moja na vinara wa ligi hii Mtibwa Sugar .
simba phiri
Katika mchezo mwingine uliopigwa mjini Tanga , Wenyeji Coastal Union waliwafunga Ruvu Shooting kwa bao moja bila bao lililofungwa na mshambuliaji raia wa jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo Itum Imbeh .
Matokeo yaliyoshangaza wengi yalikuwa kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona huko Mtwara ambako wenyeji Ndanda Fc walipata ushindi wao wa kwanza kwenye uwanja wa Nyumbani baada ya kuwafunga mabingwa watetezi Azam Fc kwa bao moja bila .
Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea hapo kesho kwa mchezo mmoja utakaowakutanisha Mgambo Shooting na Mbeya City kwneye uwanja wa Mkwakwani huko Tanga .

No comments: