
Usiku wa kuamkia leo kindumbwe
ndumbwe cha michuano ya Klabu Bigwa barani Ulaya kiliendelea na
kushuhudia Chelsea ikitoa kipigo cha mbwa mwizi mbele ya mashabiki wa
Schalke 04 ya Ujuremani pale ilipoishindilia magoli 5 bila majibu.
Manchester
City ya England nao wakawabamiza wababe wengine wa Ujerumani Bayern
Munich kwa kwa kuwafunga magoli 3 - 2 na kufufua matumaini ya kusonga
mbele katika michuano hiyo huku magoli yote matatu ya Man City yakitiwa
kimiani Sergio Aguero.
Katika mechi nyingine Paris St. Germain ya
Ufaransa waliwashikisha adabu Ajax ya Uholanzi kwa kuifunga magoli 3 - 1
huku Becelona kwa upande mwingine wakiisasambua Apoel Nicosia ya Syprus
kwa kuishushia kichapo cha magoli 4 kwa yai.
CSKA Moscow ya Urusi na AC Roma zikatoka suluhu ya goli moja 1 - 1

Burudani
hiyo itaendelea leo ambapo Liverpool ya England baada ya kufanya vibaya
katika mechi zilizotangulia leo wanajaribu bahati yao wakiwa ugenini
dhidi Ludogorets ya Bulgaria.
Arsenal nao watawakaribisha Borusia
Dortmud ya Ujerumani huku vita vingine vikiwa ni kati ya FC Basel ya
Uswis watakaopopepetana na Real Madrid. Malmo FF ya Sweden watakuwa
wenyeji wa Juventus ya Italia
No comments:
Post a Comment