Pacha waliozaliwa kwa kupishana dakika moja, wanashirikiana kila
kitu maishani. Maisha ya kawaida, gari, akaunti ya facebook, benki,
mshahara, kazi hata rafiki wa kiume, yote hayo wanafanya kwa
kushirikiana.
Mabinti hao raia wa Australia, Anna na Lucy
DeCinque (28), pia wanatumia kiasi kikubwa cha pesa kufanya upasuaji wa
kuondoa kitu chochote kitakachowafanya wasifanane.
Wamefanya upasuaji wa kuongeza matiti katika
kiwango kimoja ufanano wao ubaki kama ulivyo, wametengeneza midomo, kope
za kwenye macho na mambo mengine mengi ya kulinda namna wanavyotaka
kufanana.
Matumizi yao ya kukarabati mwili yamewagharimu kiasi cha Dola za Kimarekani 217,430 (Sh365.6 milioni).
Ni nadra sana pacha hawa kutembea kila mtu kwa
wakati wake, muda wote wanakuwa pamoja, wanalala muda mmoja, wanatumia
gari moja na kitanda kimoja pia.
Pacha hawa wanaoishi katika mji wa Perth,
Mashariki nchi ya Australia, bado wanaishi na mama yao anayeshuhudia
namna mabinti zake wanavyopatana.
Ingawa kila mmoja ana utashi na vitu anavyopenda
maishani, lakini wamechagua kuwa na rafiki wa kiume mmoja anayetoka nao
wote kwa pamoja na wakati mmoja.
Anna na Lucy, wanaamini kuwa na rafiki mmoja wa
kiume kunasaidia kujenga uhusiano wenye furaha tofauti kama kila mmoja
angekuwa na mtu wake kama ilivyo kwa pacha wengi.
Rafiki yao wa sasa wa kiume, Ben Byrne ni fundi umeme anayeishi katika mji wa Perth.
Anna anasema: “Tuna mwanaume mmoja kwa ajili yetu.
Katika uhusiano wetu, kuna watu watatu walioamua kufanya jambo moja
bila ubaguzi, chuki wala kinyongo.”
Lucy anaongeza: “Ni kama inafurahisha kwetu. Tuna
rafiki mmoja wa kiume tunalala naye kitanda kimoja. Kuna vijana
wangependa kuwa na marafiki wawili wa kike kama ilivyo kwa Byrne.”
“Tuna ladha na hamu zinazofanana kwa kila kitu,
hivyo siyo shida kumpenda mtu mmoja. Tuko pamoja kwa kila kitu,
tunashirikiana kwenye mapenzi pamoja, tuko chumbani pamoja kufurahi na
rafiki yetu,” anasema Anna.
Mwenzake Lucy anaongeza: “Byrne anafahamu kwamba anapotaka
kukutana na sisi, maana yake ni ‘double appointment’. Atakuwa na mimi
baadaye anakuwa na mwenzaku muda huohuo, wakati huohuo na chumba hicho
hicho.”
Ukaribu wa mabinti hao ambao unawakera wazazi wao,
ulianza muda mrefu tangu wakiwa shuleni. Wazazi wao wamejaribu
kuwatenganisha bila mafanikio.
Hali ilikuwa mbaya zaidi wakati walipojiingiza
kwenye mambo ya sanaa ya urembo na mitindo ya mavazi, kwani ugumu wa
kuwatenganisha ulianzia hapo.
Lucy anasema: “Mama yetu amekuwa akijaribu
kutushawishi kutengana ili kila mmoja afanye mambo yake, lakini baba
siyo sana...yeye atauliza mnafanana nani kati yenu, wewe ni Lucy au
Anna.”
Lucy anasema kuwa kama wamechoka kuendelea na rafiki yao wa kiume, wanatoa uamuzi wa pamoja na kutafuta mwingine.
“Kama ikitoke sitaki kuzungumza na Byrne kwenye simu, Anna atachukua simu na kujifanya ni mimi,” anasema Lucy.
Anaongeza: “Hatujawahi kuchoka kuwa pamoja katika maisha yetu, kila siku tuko pamoja na kufanya mambo pamoja.”
Walipofikisha miaka 24, waliamua kufanya upasuaji
wa kuongeza matiti, zaidi walishawishika kufanya hivyo baada ya kuvutiwa
na umbo la msanii wa vipindi halisi vya televishen, Kim Kardashian.
Kutokana na kushirikiana kila kitu, pia wanafanya
kazi moja kwa kushirikiana na cheo walichopewa ni kimoja, hivyo
wanalipwa mshahara mmoja siyo miwili.
No comments:
Post a Comment