Saturday 1 November 2014

Liverpool hoi , Chelsea ushindi kama kawaida

NEWCASTLE_UPON_TYNE_ENGLA
Ligi kuu nchini England imeendelea hii leo kwa michezo iliyopigwa kwenye viwanja kadhaa humo .
Katika mchezo wa kwanza uliopigwa kwenye uwanja wa St James Park Newcastle United walishinda mchezo wao wa tatu mfululizo wakiwafunga Liverpool kwa bao moja kwa sifuri .
Bao pekee la mchezo huo lilifungwa kwenye dakika ya 73 mfungaji akiwa Ayoze Perez .
Huu unakuwa mchezo wa nne kwa Liverpool kufungwa msimu huu matokeo ambayo yanawaacha kwenye nafasi ya saba baada ya kujikusanyia pointi kumi na nne zilitokana na michezo kumi waliyocheza .
Chelsea v QPR Barclays Premier League Stamford Bridge Stadium 1st November 2014
Katika michezo mingine Arsenal The Gunners waliwafunga Burnley mabao matatu bila katika mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Emirates .
Mabao ya Arsenal yalifungwa na kiungo mshambuliaji wa pembeni Alexis Sanchez ambaye alifunga mabao mawili kwenye dakika ya 70 na 90 huku Calum Chambers akifunga kwenye dakika ya 72.
Vinara wa ligi hiyo The Blues Chelsea walishinda mchezo wao dhidi ya wapinzani wao toka jiji la London Queens Park Rangers kwa matokeo ya mabao mawili kwa moja .
Wafungaji wa Chelsea walikuwa Oscar na Edin Hazard ambaye alifunga kwa mkwaju wa penati .
Arsenal v Burnley - Premier League
Katika michezo mingine Southampton waliwafunga Hull City 0-1 , West Brom nao wakawafunga  Leicester City 0-1 , Everton na Swansea wakatoka sare ya bila kufungana huku West Ham United na Stoke City wakitoka sare ya 2-2.

Newcastle1 – 0 Liverpool    FT

Arsenal   3 – 0    Burnley FT

Chelsea   2 – 1    QPR FT

Everton   0 – 0    SwanseaFT

Hull         0 – 1   Southampton FT

Leicester 0 – 1   West Brom FT

Stoke       2 – 2   West Ham  FT

Ligi hiyo itaendelea hapo kesho kwa michezo miwili ambapo Manchester City watakuwa wenyeji wa Manchester United huku Aston Villa wakiwa wenyeji wa Tottenham Hotspurs.

No comments: