Chelsea imeendelea kujiimarisha kileleni mwa Ligi Kuu England
ikiwa na pointi 32 bila mpinzani baada ya kuilaza West Brom kwa mabao
2-0.
Nao, Manchester City waliilaza Swansea kwa mabao 2-1 katika mchezo mwingine wa ligi hiyo kwenye Uwanja wa Etihad.
Mabao ya Diego Costa na Eden Hazard, kipindi cha
kwanza yaliiwezesha Chelsea kuibuka na ushindi dhidi ya West Brom
iliyocheza muda mrefu na wachezaji 10 baada ya Claudio Yacob kutolewa
kwa kadi nyekundu.
Swansea walitangulia kufunga bao kupitia kwa
Wilfried Bony kabla ya Steven Jovtric kusawazisha na Yaya Toure kumaliza
kazi, kipindi cha pili.
Kwingineko matokeo yalikuwa:
Everton 2-1 West Ham, Newcastle 1-0 QPR, Stoke 1-2 Burnley, Leicester 0-0 Sunderland
Wakati huohuo, nahodha wa zamani wa Manchester
United, Paul Ince anaamini kuwa klabu yake hiyo ya zamani haikutakiwa
kumruhusu Danny Welbeck kuondoka.
Welbeck, ambaye sasa ana miaka 23, aliyekuwa Old
Trafford akiwa na miaka minane, alijiunga na Arsenal kwa ada ya uhamisho
ya Pauni 16 milioni.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa England alipangwa
kuivaa timu yake ya zamani katika mchezo wa jana usiku wa Ligi Kuu
England kwenye Uwanja wa Emirates.
“Alipoondoka Manchester United ilikuwa ni
mshituko. Alikuwa na uwezo wa kucheza nyuma ya mshambuliaji wa mwisho na
kutengeneza nafasi kwa wengine kufunga.
No comments:
Post a Comment