Timu ya soka ya Ivory Coast huenda ikakabiliwa na vikwazo baada ya
mashabiki wake kuvamia uwanja mjini Abidjan baada ya kuweza kufuzu
kuiwakilishwa nchi katika michuano ya mataifa ya bara la Afrika mwakani.
Tukio hilo lilitokea baada ya timu hiyo kuondoka na sare ya bila
kufungana dhidi ya Cameroon siku ya Jumatano na kujihakikisha kuwa
wanamaliza wakiwa nafasi ya pili katika kundi lao D. Shrikisho la soka
barani Afrika CAF limesema linasubiri ripoti ya refa kuhusu tukio hilo.
Tukio hilo huenda likashughulikiwa na kamati ya maandalizi mnamo Disemba
mosi. Polisi walihangaika kuhakikisha wanarejesha utulivu, baada ya
mashabiki kuvamia uwanja. Picha zilizochukuliwa wakati mashabiki
wakivamia uwanjani zinaonesha kuwa mashabiki walitandikwa viboko na
askari wa usalama, huku wengine wakijaribu kuchana kaptula ya Gervinho.
No comments:
Post a Comment