Rais wa Mexico Enrique Pena Nieto
ametangaza mpango wa utaokasambaratisha mahusiano kati ya mamlaka ya
serikali za manispaa ya nchi hiyo na magenge ya wauza mihadarati. Bwana
Pena Nieto ambaye pia serikali yake inashutumiwa kufuatia kupotea kwa
wanafunzi arobaini 43 katika jimbo la Guerrero amesema Mexico haiwezi
kuendelea kama ilivyo sasa.
"Jumatatau ijayo nitatuma mpango wa
kubadili katiba katika bunge la Congress kupitisha sheria inayopinga
wanajihisisha na uhalifu wa kupanga katika mamlaka ya manispaa. Sheria
hii mpya itaanzisha mikakati kwa shirikisho kuanza kazi ya kusimamia
shughuli za manispaa au kuziondolea mamlaka kama kuna dalili
zinazoonyesha mamlaka hizo zimejihusisha na uhalifu wa kupanga. "
Amesema Rais Pena Nieto
No comments:
Post a Comment