Sunday 2 November 2014

Rais Jonathan amrudisha Stephen Keshi tena super eagle

Stephen Keshi amerejeshewa tena ukufunzi wa timu ya soka ya super eagles wiki mbili tu baada ya shikisho la Nigeria kumpiga kalamu na badala yake Shaibu Amadu kuchukua nafasi yake.
Anarejea katika ukufunzi wa kikosi hicho baada ya rais Goodluck Johnathan kuingilia kati.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 52 alifutwa kazi baada ya matokeo mabaya katika mechi za kufuzu kwa fainali za kombe la bara Afrika mwaka ujao,lakini sasa amepewa fursa ya kurekebisha.
Nigeria itachuana na Congo na Afrika kusini mnamo mwezi Novemba ,ikitarajia kushinda mechi hizo mbili ili kupata fursa ya kufuzu kwa michuano hiyo ya Morrocco.
Rais wa shirikisho la soka nchini Nigeria Amaju Pinnick na mkuu wa kamati ya ufundi wa shirikisho hilo Flexi Anyansi-Agwu walithibitisha katika taarifa kwamba Keshi ataiongoza timu hiyo katika mechi hizo mbili za mwisho.
Keshi aliiongoza timu hiyo kushinda kombe la bara Afrika mwaka 2013 na pia kuisadia Super eagles kufika katika robo fainali ya michuano ya dimba la dunia kule Brazil.

No comments: