Ataanza kazi Jumatatu na mkataba wake kumalizika mwishoni mwa Februari 2017 - baada ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika.
Avram Grant alipokuwa mkufunzi wa timu ya Chelsea. |
Ghana, ambayo iliongoza katika kufuzu kwenye kundi lao ili kushiriki mashindana hayo mwaka ujao, itapata kujua wapinzani wao nchini Equatorial Guinea wakati droo itakapofanywa tarehe 3 Desemba.
Mashindano yatafanyika kati ya Januari 17 na 8 Februari.
Grant, ambaye alikuwa kocha mkuu wa timu ya Chelsea alishindwa na Manchester United katika fainali za mwaka wa 2008 katika Ligi ya Mabingwa, alipohudumu hadi hivi majuzi ambapo alichaguliwa kuwa mkurugenzi wa kiufundi katika klabu ya BEC Tero Sasana nchini Tahailand.
Jukumu lake la mwisho kama kocha lilikuwa katika klabu ya Partizan Belgrade kati ya mwaka 2012-2014, wakati ambapo aliongoza klabu hio kutwaa ubingwa wa ligi kwa mara ya tano.
Timu ya soka ya Ghana |
Kumekuwa na wale wamekuwa na wasiwasi kwamba utaifa wa Grant ungeweza kumzuia kuingia baadhi ya nchi za Afrika Kaskazini.
Rais wa shirikisho la kandanda nchini Ghana, Kwesi Nyantekyie aliiambia BBC Michezo "kwamba ni suala" lakini anasema kuwa pande hizo mbili zitakabiliana nalo.
"Mmiliki wa pasipoti ya nchi ya Israel hatakataliwa tu kuingia nchi za Afrika Kaskazini,bali pia atazuiliwa kuingia baadhi ya nchi za Kiarabu," alisema.
"Yeye ameleta njia mbadala ya kukabiliana nayo. Kuna utaratibu wa kuridhisha wa kukabiliana na tishio lake.
Hivi karibuni, katika miezi michache ijayo, tutashughulikia kikamilifu mambo hayo."
No comments:
Post a Comment