Polisi nchini Kenya wamefanya msako
mkali dhidi ya misikiti inayotoa mafunzo ya itikadi kali za kidini mjini
Mombasa pwani ya Kenya.
Mtu mmoja ameuawa kwenye msako huo
ulioanzishwa Jumapili dhidi ya misikiti inayosemekana kutoa mafunzo ya
kuunga mkono harakati za kundi la wapiganaji wa kiisilamu la Al Shabaab
nchini Somalia.Misikiti ya kwanza kulengwa katika msako huo ni ile ya Masjid Musa na Sakina.
Watu 200 wamekamatwa ikiwemo washukiwa wakuu sita.
Polisi wanasema kuwa mtu mmoja aliuawa ingawa hawajatoa taarifa zaidi kuhusu kifo cha mtu huyo na kwamba uchunguzi utafanywa.
Viongozi kadhaa wa kidini wameuawa mjini Mombasa katika kinachodaiwa kuwa mauaji ya kiholela huku kukiwa na ushindani pamoja na uhasama kati ya makundi kinzani ya kiisilamu.
Makanisa pia yamekuwa yakilengwa kwa mashambulizi.
No comments:
Post a Comment