Thursday 6 November 2014

Messi avunja rekodi ya UEFA ampita Ronaldo

Lionel Messi amefikisha idadi sawa na Raul ya magoli 71 katika Klabu Bingwa Ulaya, baada ya kufunga mabao mawili wakati timu yake ya Barcelona ilipocheza na Ajax. Mchezaji huyo wa kimataifa kutoka Argentina alipachika bao la kichwa katika dakika ya 36. Goli lake la 71 lilifungwa katika dakika ya 76 wakati Barcelona ilipofuzu kuingia katika raundi ya timu 16. Messi kwa sasa amempita Cristiano Ronaldo wa Real Madrid, ambaye amefunga magoli 70, katika orodha ya wafungaji bora wa Champions League. Wakati ilimchukua Raul mechi 142 kufunga mabao 71, mechi ya Messi dhidi ya Ajax ilikuwa ya 90 katika michuano hiyo. Ronaldo ambaye alicheza katika mechi ya Liverpool siku ya Jumanne, amecheza mechi 107 na kufunga mabao 70.
Orodha ya wafungaji bora katika UEFA Champions League:
Lionel Messi magoli 71 mechi 90
Raul magoli 71 mechi 142
Cristiano Ronaldo magoli 70 mechi 107
Ruud van Nistelrooy magoli 56 mechi 73
Thierry Henry magoli 50 mechi 112

No comments: