Sunday 23 November 2014

Wananchi watunisia wapiga kura leo kumchagua rais wao

Wananchi wa Tunisia wakipiga kura
Wapiga kura nchini Tunisia wanaelekea katika vituo vya kupigia kura hii leo kumchagua rais mpya.
Huu ndio uchaguzi wa tatu kuandaliwa tangu mwaka 2011 wakati wa mapinduzi yaliyomuondoa madarakani rais Zine el-Abidine Ben Ali.
Mgombea mkuu kati ya wagombea wengine zaidi ya 20 ni Beji Essebsi wa chama cha Nidaa Tounes ambaye pia ni afisa wa zamani kwenye serikali ya rais wa Ben Ali.
Mpinzani wake mkuu ni rais wa sasa wa mpito Moncef Marzouki
Chama cha kiislamu cha Ennahda ambacho kilichukua nafasi ya pili kwenye uchaguzi wa mwezi Oktoba hakina mgombea.

No comments: