Mji mkuu wa Burundi, Bujumbura |
Wizara ya mambo
ya nje ya Marekani imewaonya Wamarekani wasiende Burundi, ikisema kuna
vitisho vya mashambulizi ya kigaidi kutoka kwa kundi la wanamgambo wa
Somalia-al Shabab.
Wizara ya mambo ya nje ya Marekani pia imewaonya raia wote wa
Marekani wasiende Burundi, ila kwa shughuli muhimu sana, ikisema kuwa
kuna vitisho vya mashambulizi ya kigaidi kutoka kwa kundi la wanamgambo
wa Somalia-al Shabab, pamoja na uhalifu wa hali ya juu ndani ya taifa
hilo maskini.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kundi la al-Shabab limetishia kufanya mashambulizi ya kigaidi ndani ya Burundi na huenda likalenga maslahi ya Marekani.
Onyo hilo linaonya Wamarekani walioko Burundi wasitumie barabara kuu kuanzia jioni hadi alfajiri. Inasema magenge yenye silaha huvizia magari kwenye barabara kuu zinazoingia mji mkuu Bujumbura.

No comments:
Post a Comment