Serikali imetangaza watakaoingia kidato cha kwanza mwakani kutokana
na matokeo ya darasa la saba ambapo wanafunzi 427,60 kati ya 844,938
waliofanya mtihani huo mwaka huu wamefaulu ikiwa ni asilimi 50.61 huku
ikisisitiza hakuna asiyejua kusoma kuhesabu na kuandika .
Jumla ya wanafunzi 844,938 wamechaguliwa kujiunga
na kidato cha kwanza mwakani katika shule za serikali kati ya wanafunzi
867,983 waliofanya mtihani huo mwaka huu.
Akitangaza matokeo hayo katibu mkuu ofisi ya waziri
mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa Bw. Jumanne Sagini amesema
katika wanafunzi waliofaulu 16,482 wamekosa nafasi na kwamba watasubiri
chaguo la pili na kwamba katika mitihani hiyo vitendo vya udanganyifu
vilipungua tofauti na mwaka jana.
Kuhusu kuwepo kwa wanafunzi ambao wamemaliza darasa
la saba mwaka huu huku wakiwa hawajui kusoma wala kuandika katibu mkuu
huyo wa Tamisemi amesema hakuna mwanafunzi hata mmoja aliyemaliza darasa
hilo la saba hakiwa hajui kusoma na kuandika na kwamba hizo ni
propaganda za watu wasioitakia mema sekta ya elimu hapa nchini.
No comments:
Post a Comment