Saturday 6 December 2014

ICC yatupilia mbali kesi dhidi ya Rais wa kenya Uhuru Kenyatta

Mahakama ya kimataifa ya ICC imetupilia mbali kesi ya jinai inayomkabili Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.
Mwendesha mkuu wa mashitaka Fatou Bensouda ameondoa kesi dhidi ya Kenyatta ambaye alidaiwa kutenda uhalifu dhidi ya binadamu wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi mwaka 2007/2008.
Mahakama ilikuwa imempa Bensouda wiki moja kuamua ikiwa ataendelea na kesi dhidi ya Kenyatta au la inagwa alisema muda huo haukutosha kwake yeye kuandaa ushahidi zaidi dhidi ya Kenyatta.
Kenyatta alishtakiwa kama mshukiwa mkuu wa ghasia za baada ya uchaguzi wa 2007/2008 akituhimiwa pamoja na William Ruto ambaye ni naibu Rais kwa kutenda uhalifu dhidi ya binadamu.
Zaidi ya watu elfu moja waliuawa wakati wa ghasia hizo. Uhuru alikuwa mtu maarufu zaidi kufikishwa mahakamani na pia mshukiwa mkuu kwani alifikishw amahakamani akiwa Rais aliye mamlakani.
Hili ni pigo kubwa kwa upande wa mashitaka, wengi wlaioana keshi dhidi ya Kenyatta kama mtihani mkubwa katika historia ya mahakama hio.
Upande wa mashitaka ulitaka mahakama kuupatia muda zaidi ili upate ushahidi zaidi,dhidi ya Kenyatta kama vile taarifa za akaunti yake ya benki.
Upande wa utetezi uliteta kuwa ikiwa hakuna ushahidi wa kutosha kesi hio inapaswa kutupiliwa mbali.

No comments: